Anayosema Kigwangalla kuhusu uaminifu wa Watanzania kuna tatizo?



Kanipa somo zuri, ila mwanaume alii mbele ya watoto, Mama na Mke, hata kama anauliwa, Gambush blal glash.
 
Hapo sijaona tatizo la huyo kijana.
Tatizo halipo kwa vijana wa kitanzania.
Tatizo lipo kwa kigwangala. 100%

Mimi ni mjasiriamali pia.

Tatizo alikuwa anafanya biashara ya keyboard, unaletewa mahesabu mezani na unaweka pesa.

N:B nimetembelea wakulima wakubwa wa south africa,zambia,ukraine,dutch.

Mkulima ofisi yake ni shambani kwake anahandle kila kitu na ana accountant na kaajili. Sio hii upo mjini dar unatuma pesa kijijini wakulimie hujui miundombinu ya hapo matatizo ya day to day etc
 
Hata investor anayetuma pesa katika biashara hampi mtu pesa ,anaitoa katika proper and skilled management. Kama angekua ameajili :

1: Bwana shamba -2
2: farm meneja -1
3: accountant -1
4: Internal auditor -1
5: Sales/marketing executives- 5

So nafasi zote hizo kampa mtu mmoja na unamlaumu. Not fair angemuweka awe farm manager na angeajili hao wengine pia.
 
Nilikuwa nawaza kuandika uzi wa namna hii kutokana na changamoto na uzoefu niliokutana nao katika harakati za kutaka kutengeneza maisha bora KWa familia yangu na jamii KWa ujumla. Lakini kwakuwa bwana kigwa kaandika ujumbe umewapata wahusika...

Nakumbuka katika harakati za maisha kuna biashara nilianzishisha,, nikamuweka mdogo wangu.. aiseh SAsa sijui alichoka au hakuitaka... Aliharibu sana aiseh...! Kwakuwa ni ndugu nikaona nipotezee tu nimepata elimu fulani katika hilo... Haya kuna ndugu wa pembeni alikuja kunitembelea akaniambia e bana nitakaa wiki 2 tu! Nikasema haina shida njoo... Alivyo kuja siku hiyo nilikuwa nasimamia biashara yangu mwenyewe.. alivyo fika akaona hakuamini maana alikuwaga na dharau sana... SAsa sijui iliwasa tu moyoni kuwa ana hakikisha ananifilisi... E bwana eeh! Ile mdogo wangu alivyo maliza dharula yake nami nikawa naendelea na mengine jamaa KILA day anakwenda pale ofisini atashinda asubuhi hadi jioni na atafosi atumie bajeti ya ofisi... Nilikuwa sijui kuja kugundua ni siku napitia hesabu nikajua nikashangaa wewe inakuaje unatumia chakula gharama hii namuuliza SAsa yule mdogo wangu nilie mwachia... Tumboni una mapipa ya lita 200? Kanyamaza tu SAsa hadi vicha unaweka KWa kutumia pesa ya ofisi kwani sikupagi pesa? Kanyamaza tu.... Nilimindi sana nikaona nikwambia ukweli hunikomoi tu mimi hadi wewe unajikomoa bila kujua mambo maana hayatoniharibikia tu mimi... BAdo wewe na wadogo zako na wazazi wetu maana kidogo mimi nina kahaueni badala muwe na bidii na uaminifu mnasikiliza ndugu wengine we haya... Kwakuwa baada ya kupiga hesabu nikaona hapa hadi nifanye haki itakuwa tete tu labda nikope... Nikaona niipotezee tu ijifie taratibu... Nilivyo ipotezea yule jamaa nae akawa ana kazana kwenda halafu ikifika jioni anasikia naongea na simu kama nimepagawa nakaripia watu hovyo KWa sababu ya mishe nilizo wapa nikawaamini na zikafeli yeye kumbe akisikia vile ana furahi.. na KWa upande wa pili wa mdogo wangu alivyo ona nimeicha biashara ijifie nae baadhi ya mambo yakawa magumu akaona amwambie mama kuwa yule ndugu ndo kasabisha yeye tokea aje kutwa hapa anafosi matumizi yake yaingizwe kwenye bajeti ya ofisi... Mama akamjibu kwanini ulinyamaza hana majibu... Mama kanitonya... Ikabidi nimchane tu jamaa kuwa aondoke kwangu maana SAsa ni miezi 3 na ulisema wiki 2.... Daahh! Nilisikitika sana..

Kuna mwengine nae kaomba chombo ya moto KWa ajili ya biashara akasema mimi nitakupa faida.. fulani yule hawezi sijui anakusumbua... Haya Sawa chukua chombo hii... Mwezi umepita mtu kimya unamuuliza vipi chombo mbovu hii namuuliza KWa nini usiniambie? Hana majibu yanayo elewaka( Hapo kuna mtu ananiambia chombo inapiga Kazi vibaya mno) nikamwambia leo jioni ilete(huwa ananielewa nikongeaga kitu huwana nahakikisha nakitekeleza au kinatekelezwa)... Imefika jioni naona muamala... Nikampigia hii ndo jioni ilete chombo majibu yake SAsa! Oohhh! Najua kwako hii biashara kwahiyo mambo yasiwe magumu nimeazima nikutumie... Nikamwambia hiyo si mbovu SAsa unakaa nayo ya nini? Ilete nikipata pesa nitairekebisha, jibu lake ooh! Nitairekebisha.... Nikaona isiwe tabu kesho irekebishe... SAsa sijui ndo alienda kuharibu? Ila hesabu anatuma lakini kumbe sijui anamipango yake... Imefika wakiti ananipa taarifa chombo ipo KWa Fundi naenda KWa Fundi chombo haitamaniki... Na sijui walipanga na Fundi? Nikapiga hesabu ya vifaa original pesa niliyo toa na ni zaidi hata ya hesabu aliyonipa KWa siku zote... Naye Fundi kama ilivyo destri ya Vijana wengi wa kitanzania pia kafanya udhulmati wake (aliyo yafanya itoshe tu kusema sio Fundi mtengenezaji ni Fundi muharibifu). Nikaona ataniumiza kichwa pamoja na kuingia hasara nikaona nichukue siklepa langu maana lishakuwa siklepa kwanguvu nikaondoka nalo likae tu home maana linafanya Kazi badala linipe faida linanitia hasara tu...

Nakubaliana na baadhi ya wanajamvi humu somo la maadili muhimu... Kokote kwenye mikusanyiko lisemwe, na Katika familia lisemwe na kutendwa na pia liwekwe mashuleni kuanzia chekechea hadi university.......

Japan wamefanikiwa sana katika hilo.. somo la maadili lipo mashuleni... Kuna jamaa mmoja mbongo alikuwa anafundisha shule ya Kati huko nchini japani unaweza sema KWa bongo huku ni kama sekondari... Siku kuna Mwanafunzi alisahau kamera darasani ile kamera ilikaa wiki nzima pale pale hadi yule Mwanafunzi anafika darasa lile anaikuta vile vile..... Bongo SAsa hata uangushe bahasha iliyo tuna watu hata hawajui kuna nini watatembea nayo... Watafungulia hukohuko... Kama wakikuta makaratasi ambayo hayana faida kwao watayatupa bila kujali wewe uliye yaangusha unafaida nayo hata kama wanakujua...
 
Unatafuta namna ya kumlaumu bwana kigwa... Mtu ndo anaanza SAsa hao watu atawalipaje na kasema kabisa ikifika kipindi anakopa.. pengine kapiga hesabu kaona hao wataalamu gharama yake tu ni tractors na skavetors kadhaa.... Be positive somtimes
 
Unatafuta namna ya kumlaumu bwana kigwa... Mtu ndo anaanza SAsa hao watu atawalipaje na kasema kabisa ikifika kipindi anakopa.. pengine kapiga hesabu kaona hao wataalamu gharama yake tu ni tractors na skavetors kadhaa.... Be positive somtimes
Ndio ukweli huo halisi nakuambia. Either uufuate ufanikiwe ama ubaki kulalamika.
Eg: crdb,nmb,tbl,tcc,nk kampuni hizo wanaofanya kazi ni vijana wazungu ama wajapani? No ni watanzania, ishu ni system hakuwa nayo. Kwa capital yake hakutakiwa kuwa mchuuzi. 100% blaming ni juu yake
 
Unatafuta namna ya kumlaumu bwana kigwa... Mtu ndo anaanza SAsa hao watu atawalipaje na kasema kabisa ikifika kipindi anakopa.. pengine kapiga hesabu kaona hao wataalamu gharama yake tu ni tractors na skavetors kadhaa.... Be positive somtimes
(, kila kijana mmoja nalipia gharama ya kuanzia kumlimia na kumtunzia shamba lake; ekari 30 (huyo mkubwa wao), ekari 15 wale wasaidizi wake wawili. Kwenye ekari 15 unapata kati ya 30 - 40m kwa mwaka. Matukio ya hivi ni mengi kwenye story za wajasiriamali wengi hapa nchini)

Kama ana uwezo wa kumlipia milioni 30-40 kwa msaidizi kwa mwaka, maana yake kwa watatu anatumia zaidi ya milioni 100.
Mwenye uwezo huo maana yake ana uwezo wa kuajiki professional (wataalamu wa kilimo,acxountant,sales and marketing)- 10 ,akawalipa take home laki 7 ambapo ni sawa na milioni 84 kwa mwaka na kazi yake ikaenda vizuri.
 
Imani za dini zinatupumbaza mno watanzania. Mno. Wewe mtu anakutendea uovu huo, unamwacha. Ni dhambi kwa sababu unapomwacha hujamsaidia. Mhalifu ni mhalifu tuu, peleka kwenye vyombo vya sheria aadhibiwe, akirudi mpokee. Atakuwa GM mzuri kabisa maana amefundishwa huko maana ya kufanyakazi na uadilifu. Watanzania wengi wanadhani kumfunga mtu jela ni dhambi. Hamna. Gereza ni vyombo vya Mungu pia kuifanya dunia mahala pa amani. Ona sasa, mtu anafikia hatua ya kutaka kuteketeza mali za mamia ya mamilioni! Kweli? Huyo anakuua pia, tena mchana kweupee!
Nina mtoto alijifanya ameshindikana; Peleka shule, tena hizi za gharama, wapi! Geuza na kugeuza, wapi! Wananchi wakanishauri kuwa nisimlazimishe hataki shule, kwani wote lazima wasomee? Nikawaelewa. Nikampeleka kusomea udereva, nikampatia motokaa, akashirikiana na mafundi anaiba vipuri, gari mwisho wa siku likakaa juu ya mawe. Navumilia ila moyo unaniuma kwelikweli. Akakwiba kwa mtu akafungwa, Nikamtoa. Si unajua Bongo ukiwa na "kitu kidogo" hakuna jambo gumu. Nikamweka dukani, akapora. Aah, akili zikanirudi. Utu wangu ukanirudia. Utu wa ndani kabisa. Nikahisi kuwa na hatia kwa kuendelea kumdekeza wakati Serikali imeajiri vyombo vyenye vijana wasomi waliosomeshwa hadi shahada juu ya kurekebisha tabia za watu. Nikampeleka gerezani. Mapolisi, mahakimu, maafisa magereza walinipongeza sana, walisema, Bongo tungekuwa na wazazi kama wewe tungetengeneza kizazi cha vijana kilicho bora bora kabisa. Kijana alifundishwa adabu kule. Watu wamesomea mambo haya bwana. Tena alikaa miezi mitatu tu. Aliporudi sikuamini. Jambo la kwanza alitubu kwa machozi mengi Nimsamehe. Nilimsamehe. Ni mtoto, kama mzazi sikuwa namwadhibu ili ateseke bali a-reform. Baada ya hapo Akaokoka. Aliomba shamba, nikampatia na vitendeakazi vyote. To cut story short, sasa hivi ni kijana mzuri, mzuri mno na ndiyo tegemeo langu.
Mhe: Kigwangala, ulikosea kijana huyo ulitakiwa kumpeleka jela. Ange-reform na kuwa chombo chenye kufaa. Kwa kumwacha ataendeleza ujinga wake. Polisi, mahakama, na gereza, vipo kwa ajili ya watu kama hao, ukimwacha atakufa ktk dhambi zake na akifa anakwenda Jehanamu. Damu yake mwenyezi Mungu ataitaka mikononi mwako mhe. Kigwangala.
Over.
 
Ukileta emotion ama undugu katika biashara basi hutoboi.
Biashara ina rules zake. Ni either ufanye 100% ama achana nayo.
Wananifata wengi ambao wameajiliwa nachowashauri msiingie ktk biashara sababu kuna vitu vingi sana underground. Nawashauri wajenge nyumba za kupangisha kama hawana akili nzuri zitawalipa in the long run.
 
Tom alikuwa mjinga sana alipora mke wa mtu pale chimala anaitwa d akawa anatanua naye
Baada ya kigwa kumfunga pale gereza la uhamila na kutoka,akaja mbeya life likampiga amechoka yupo mwanza,huko
Tom alichezea tshs chooni

Sent from my SM-N960U using JamiiForums mobile app
 
Anafanya shughuli gani nowdays

Yule dogo kigwangala ilitakiwa akaze kamba ampige gerezan hata miaka 10
ili aisome namba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…