Ancestral Curse: Ujerumani iliwaua Wayahudi zaidi ya Milioni 6, lakini ndio nchi yenye nguvu zaidi Ulaya. Je, hii dhana ya laana ya asili ipo sahihi?


Nitatoa jibu langu kutoka kwenye perspective ya Biblia Takatifu. Ulimwengu wa roho una kitu kinaitwa madai ambayo lazima yalipwe ili hali fulani mbaya inayokabili mtu/ ukoo/ kabila/ nchi itulie. Sio kila uovu unatoka kwa kukemewa kwa jina au damu ya Yesu.

Kwa mfano kama ukoo wenu ulikuwa na miungu yake na mkaiacha kienyeji bila utaratibu sahihi wa kiroho kufuatwa, hiyo miungu ya ukoo itainua madai kwenye ulimwengu wa roho dhidi ya wanaukoo huo na madai hayo ni sahihi katika muktadha wa kiroho. Ikumbukwe kuwa ancestors wa ukoo huo walijikabidhi kwa hiari kwa miungu hiyo, hali ambayo iliunda agano halali la kiroho katika ulimwengu wa roho. Kwahiyo, ili kujiachanisha na miungu hiyo, kuna utaratibu wa kiroho lazima uufuate kwa usahihi kabisa, na ukikosea hata kama wewe ni mlokole kindakindaki, huwezi kujitoa katika vifungo au laana za miungu hiyo. Lazima uingie deep kwenye ulimwengu wa roho ujue tatizo lilipo ili ujue sehemu sahihi ya kupeleka damu ya Yesu kwa ajili ya kulipa fidia ya kukukomboa (ransom) kutoka kwa miungu hiyo na laana zote.

Kwenye agano la kale, wayahudi ndio taifa pekee ambalo lilikuwa na agano na Mungu wa mbinguni, agano ambalo lilikuwa na kifungo cha kiroho tangu Ibrahimu. Kila wakati walipomwasi Mungu walipata adhabu kali kwa kulivunja agano lao na Mungu. Mfano Mungu aliwauza wayahudi kwa falme za Babeli, Uajemi, na Rumi walipomwasi Mungu.

Hii vita ya kiroho ya maagano ya kimungu iko very perfectly principled, bila kujali wazee wako walikuwa wakimuabu mungu yupi! Hoja ya msingi ni kwamba lazima agano lolote la kimungu cha shetani livunjwe kwa utaratibu sahihi wa kiroho na kulipa fidia sahihi kwa miungu unayotaka kuachana nayo kabla ya kuambatana na Mungu wa mbinguni. Walokole wengi wameshindwa kutegua huu mtego wa shetani, kwani wengi wao wanadhani kila roho ya shetani inatolewa kwa kukemewa kwa jina la Yesu, kumbe roho nyingine zinatolewa kwa kulipwa fidia kwanza.

Sasa tuje kwa Germany. Kama unasoma historia vizuri na kwa umakini, utagundua kwamba vita kuu ya pili ya dunia ambayo wajerumani waliianzisha, imechochewa na mambo makuu matatu.

Moja, ni dhuluma waliyofanyiwa na Uingereza na washirika wake wakati wa vita vya kwanza vya dunia, ambapo Ujerumani alilazimika kupigana ili kulinda maslahi yake Ulaya na duniani baada ya kupata mbinyo mkubwa kutoka Uingereza. Uingereza alikuwa na hofu kwamba masive expansion ya Germany ilikuwa inahatarisha usitawi wa maslahi yake duniani. Kwahiyo, ikabidi ianzishwe conspiracy ya kumdhibiti Germany mapema. Ndiyo vita ya kwanza ya dunia ikaanza, ambapo Germany alishindwa na kunyang'anywa makoloni yake yote, ikiwemo Tanganyika, Rwanda na Burundi. Kwahiyo, Germany ni kama alikatwa miguu yote miwili, kwahiyo ilibidi lazima apigane ili arudi kwenye chati tena.

Pili, Wajerumani walikuwa na chuki na wayahudi kwani walikuwa wamehodhi uchumi wao kwa kiasi kikubwa. Mbaya zaidi, wayahudi ni wabinafsi kwa asili yao, hali iliyowafanya wayahudi wajione watumwa ndani ya nchi yao. Kwahiyo, Hitler alikuwa na ndoto kubwa kuwashughulukia jews for that reason. Hata mauaji ya kimbari ya wayahudi wakati wa second world war, yalichochewa na chuki hii ya wajerumani kwa wayahudi.

Tatu, Hitler na genge lake waliwaaminisha wajerumani kwamba wao ni super race duniani, kwahiyo, wao wanapaswa kutawala na sio kutawaliwa na yeyote yule duniani. Huu ulaghai wa Hitler ndio ulimfanya Hitler na genge lake wawe na adhma ya kutaka kuitawala dunia wakati wa vita vya pili vya dunia.

Aidha, baada ya vita vya pili vya dunia, Germany alishindwa tena, na kupewa adhabu kali sana na mataifa washirika waliokuwa upande wa ushindi yaani USA, USSR, Uingereza na Ufaransa. Kwanza miundombinu yake yote ya viwandani ilikuwa sehemu ya vitu vilivyoporwa na mataifa hayo baada ya vita. Vilevile, wanasayansi wabobezi wa Ujerumani katika nyanja zote walichukuliwa mateka na mataifa yaliyoshinda vita. Ikumbukwe kuwa technology ya Ujerumani katika mambo kama silaha, ndege za kivita, U-Boats ili kuzamisha meli na nyambizi za Uingereza, na techhnology za uzalishsji mali kama viwanda zilikuwa tayari ziko juu sana kwa quality kipindi hicho. Pia Ujerumani iligawanywa vipande viwili: East Germany na West Germany, na kuasisi vita mpya ya dunia iitwayo Cold War. Vilevile, Ujerumani alilazimishwa kulipa fidia kwa nchi zote ambazo zilikuwa wahanga wa vita aliyoianzisha.

Ukisoma Daniel sura ya 9 na Maombolezo 5:7, utaona uovu na dhambi lazima vilipiwe ili kukomesha laana. Kwa kutazama adhabu alizopewa Ujerumani baada ya WW2, ni dhahiri kabisa kwamba alilipia uovu wake wote kwa zile adhabu alizopewa na mataifa washindi. Ukiisoma torati ya Musa utaona kwamba torati iliamuru kwamba aliyeua lazima naye auawe ili nchi isiinue uovu na laana. Ingawa sheria hii Yesu alikuja kuiondoa na badala akaleta sheria mpya ya rehema, toba, na kusameheana kupitia Agano Jipya la Kuokolewa kwa neema kupitia kwa Damu ya Yesu. Sina ushahidi wa dhahiri kwamba Wajerumani walitubia uovu wao wa WW2. Ila nnachojua ni kwamba waliadhibiwa sana kwa kusababisha vita ile.

Kwahiyo, kwa sheria ya kiroho, ni vigumu mno kuamini kwamba Ujerumani alipaswa kupata laana zaidi ya hizo adhabu alizopewa na nchi zilizoshinda vita, kwani hata mateka wao wa vita wengi wao waliishia kuuawawa na kuzikwa ugenini bila hata ndugu kujua marehemu wao walipo.

Mchumi mashuhuri wa Uingereza, John Maynard Keynes, alivyo-review paper inayohusu financial reparation ambazo Germany alipaswa kulipa kama fidia, aliikataa kabisa hiyo paper kwani ilikuwa haiwezekani katika parameter za kiuchumi hizo fidia kulipika kwa kiasi na muundo ulioamuliwa. Hata hivyo, bado Ujerumani alilazimishwa kulipa.

Clearly, unaweza kuona kwamba , Germany alilipia kabisa uovu wake hata katika muktadha wa kiroho.

Pamoja na kunyang'anywa kila kitu, Ujerumani walianza upya manufacturing technology yao from scratch, na hadi mwanzoni mwa miaka ya 70, West Germany ilikuwa tena on top in engineering technology, hali iliyosababisha hata watesi wao waanze tena kuiba Germany technology.
 
Tatu, Hitler na genge lake waliwaaminisha wajerumani kwamba wao ni super race duniani, kwahiyo, wao wanapaswa kutawala na sio kutawaliwa na yeyote yule duniani.
I think this guy was trying to instill patriotic mindset kwa wananchi wake. Huu ni uzalendo sana kwa kiongozi...
 
Madini mazito sana haya kaka mkubwa.
 
Ulimwengu wa roho una kitu kinaitwa madai ambayo lazima yalipwe ili hali fulani mbaya inayokabili mtu/ ukoo/ kabila/ nchi itulie. Sio kila uovu unatoka kwa kukemewa kwa jina au damu ya Yesu.
asante mkuu...
 
Mdogoangu aliyehesabu hizo maiti milioni6, specifically za Jews ni nani??

Wewe tuuzie tu vitabu vya kijerumani, propaganda zao za kibeberu achana nazo...

Kuanzia IBM, mpaka experiments za pharmaceuticals za uzazi wa mpango zilifaidika sana na hii vita..
A lot of scientific discovery na research zilifaidika kwa hili..

Ni sawa tu na twende DRC.

Everyday is Saturday............................ 😎
 
Mao The Don uyu ndo anaongoza 70+ million waliteketea

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Roma ilianguka kwa sababu ilikwisha andikwa. Na siyo kwa sababu ya kumwua Yesu.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Kwa hapa sina comment kwa maana kila shetani ana mbuyu wake. Unayemuona hana maana kwako anaweza akawa ni mtu wa muhimu kwa mwingine...
Bwana mkubwa Mbowe kama unapita hapa nakuomba ikiwezekana tembea kwa magoti hadi chamwino ukaombe radhi kwa Rais Magufuli la sivyo mtakufa tu mtakuwa mmekaidi sauti ya Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…