Ancestral Curse: Ujerumani iliwaua Wayahudi zaidi ya Milioni 6, lakini ndio nchi yenye nguvu zaidi Ulaya. Je, hii dhana ya laana ya asili ipo sahihi?

Ancestral Curse: Ujerumani iliwaua Wayahudi zaidi ya Milioni 6, lakini ndio nchi yenye nguvu zaidi Ulaya. Je, hii dhana ya laana ya asili ipo sahihi?

Wale waliouawa ni binadamu pasipo kujali walikuwa ni Wayahudi wa imani au damu ya Yakobo.

Wajerumani waliangamiza roho Milioni 6 ila hawana laana bali wananeemeka...
Unajua ni kwanini Dkt. Magufuli anamshinda Tundu Lissu?
 
Kuna coment hapo juu nimemuuliza mtoa mada atoe tafsiri sahihi ya hao waliouawa walikuwa ni wayahudi wenye asili ya Israeli au walikuwa ni wafuasi wa madhehebu tu, lakini kamute!
Mkuu, siku-mute bali nilikujibu kwamba, Hitler aliua BINADAMU pasipo kujali ethnicity yao. Hata kama wangekuwa ni wajaluo ama wamakonde roho ya mtu haifanyiwi siasa mzee baba...
 
Mkuu, siku-mute bali nilikujibu kwamba, Hitler aliua BINADAMU pasipo kujali ethnicity yao. Hata kama wangekuwa ni wajaluo ama wamakonde roho ya mtu haifanyiwi siasa mzee baba...
Sawa, hilo linafahamika na idadi hiyo ya watu kuangamizwa.

Sasa niliona kwa kuwa unauelewa mkubwa kuhusu hayo mambo, si vibaya ukanifafanulia na hilo.

Ujue mimi ninaelewa kuwa uyahudi ni madhehebu na wengine hudai kuwa wayahudi waliouawa ni wa asili ya Israeli.

Huo ndiyo utata.

Na wanahistoria wanaandika kuwa waliouawa ni wayahudi wa nchi zilizokuwa zimevamiwa na kuwekwa chini ya himaya ya ujerumani enzi hizo za vita.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa niliona kwa kuwa unauelewa mkubwa kuhusu hayo mambo, si vibaya ukanifafanulia na hilo.
Mkuu, uelewa wangu ni wa kawaida sana kaka mkubwa.

I am a very ordinary person bro. and I look very normal. Siku ukibahatika kuonana ana kwa ana na mimi hotoamini appearance yangu...
 
Huchukua muda kidogo kwa mfano dola ya kirumi ilikuwa ndio yenye nguvu ikitawala dunia lakini baada ya askari wake wa kirumi kumuua Yesu dola ya kirumi ilisambaratika na sasa Italia ni kiinchi kidogi tu cha hovyo

Pili kuna mjerumani mtu wa Mungu Martini Luther aliyeanzisha imani ya kiprotestanti duniani kazi yake yaweza kuwa sababu ya ujerumani kutopigwa na laana hadi sasa
Ulutheri imo pote duniani
Italy ni kinchi kidogo tu cha hovyo! Kwa kipimo kipi?
 
Mkuu, uelewa wangu ni wa kawaida sana kaka mkubwa.

I am a very ordinary person bro. and I look very normal. Siku ukibahatika kuonana ana kwa ana na mimi hotoamini appearance yangu...
Chadema ni genge la wakora ,wakuogopwa kama ugonjwa wa ukoma,hawafai.
 
I think this guy was trying to instill patriotic mindset kwa wananchi wake. Huu ni uzalendo sana kwa kiongozi...
Mi mwenyewe naweza waamini.Watu walipigwa vita wakashindwa vibaya.Wametumia akili, wamejenga uchumi, wamekuza teknolojia na Sasa ni taifa no.1 ualaya huoni kuwa hao ndio wazungu wenye akili zaidi kuwhi kutokea.Kuna wagunduzi wengi sana ujermani kuliko taifa lolote la ulaya.Marekani inatumia race zote kufanya maendeleo yake ujermani wapo kivyao.Uchina inaiba teknolojia Herman ina innivate!
 
Kabila la wameru Arusha walimtairi mmsionari mzungu kwa lazima na kumpiga sasa utaniambia wameru wapoje? Kina Nassari?
 
Ata kama hiyo laana ipo sio lazima itokee kwenye kizazi ambacho wewe upo.inawezekana ikaja kuwatafuna kizazi cha miaka mingi ijayo.Kwahiyo sio rahisi kupata majibu ya moja kwa moja sasa angali dunia na ujerumani bado ipo na itaendelea kuwepo ata baada ya sisi kupita.kwahiyo tuupe wakati muda wakuamua.
Hitler aliteketeza roho za watu achana na suala la Uyahudi kwanza. Kwanini hawa jamaa hawatafunwi na laana ya babu zao na badala yake wanazidi kuneemeka kiuchumi?...
 
Saddam Hussein alichoma visima vya mafuta vya nchini Kuwait katika vita ya ghuba miaka ile ya 1990s lakini fidia bado inalipwa na serikali ya Iraq mpaka leo hii.

Ujerumani ni Ujerumani tu hata kama ilikuwa chini ya utawala wa Adolf Hitler na Wanazi wenzake.
Chadema ingechaguliwa 2015 haya maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ikiwemo SGR, Bwawa la umeme Fly overs, ununuzi wa ndege nk...nk ingekuwa bado ni ndoto kwa watanzania.
 
We unadhani kwanini halaumiwi yeye tibbets na badala yake lawama zinaenda kwa marekani?
Upo sahihi mkuu. Ndio maana nimehoji juu ya dhambi ya mababu kwa Ujerumani na sio Hitler pekee.

Huyo jamaa hapo juu alikuwa anachanganya watu tu humu for no good reasons.
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Ndugu zangu watanzania;

Ujerumani iliwaua Wayahudi zaidi ya Milioni 6, lakini ndio nchi yenye uchumi mkubwa zaidi barani Ulaya (European Powerhouse).

Kwanini wao hawajatafunwa na laana hii ya asili kutoka kwa babu zao? Je, hii dhana ya laana ya asili (Ancestral/Generational Curse) ipo sahihi kweli?

Kama ipo sahihi, kwanini iwepo Afrika tu na sio Ulaya?


Laana ya Asili kama inavyofafanulia na Mtumishi Joel Osteen (American Preacher & Televangelist)
=============
Laana ya vizazi inaaminika kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa sababu ya uasi dhidi ya Mungu. Ikiwa ukoo wako umepewa laana ya talaka, uchumba, umaskini, hasira au mifumo mingine isiyo ya kimungu, unaweza kuwa chini ya laana ya ukoo.

Familia zetu zina ushawishi mkubwa juu ya maendeleo yetu, pamoja na ukuzaji wa mifumo yetu ya dhambi. Watu wengine wanadai kwamba laana za kifamilia au kizazi hupitishwa kwa njia ya kizazi.

Imani hii inatokana na vifungu vya Agano la Kale ambavyo vinasema kwamba Mungu "huwaadhibu watoto na watoto wao kwa dhambi za baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne" (Kutoka 34: 7).

Ikiwa familia zinarithi laana za kiroho au la, ni dhahiri kwamba mifumo ya dhambi hupitishwa kupitia familia. Kila mtu hutenda dhambi; lakini kama vile utamaduni, kabila, na jinsia zinavyoongoza mwelekeo wetu wa dhambi katika mwelekeo fulani, ndivyo pia familia zetu.

Tunarithi tabia nyingi na mapenzi ya kitu fulani kutoka kwa wazazi wetu ambao sio ushawishi mzuri kwetu au kwa wengine. Tunapopata tabia ya imani au imani ambayo inaathiri vibaya maisha yetu au wale wanaotuzunguka, hii inajulikana kama laana ya kizazi. Ni upande uliojificha wa tabia uliopitishwa kupitia vizazi.

KIINGEREZA KIDOGO: Many Africans, Christian or not, live in fear of generational curses. When misfortunes hit, they want to know who might have bewitched them.

Non-Christians may turn to the witchdoctor while believers seek a deliverance minister to diagnose their problem and prescribe necessary spiritual steps forward. But why is this so?

HISTORIA NDOGO YA MAUAJI YA WAYAHUDI BARANI ULAYA (HOLOCAUST)
==========
Holocaust, yalikuwa ni mauaji ya halaiki ya Vita vya pili vya dunia kwa Wayahudi wa Ulaya. Kati ya mwaka 1941 na mwaka 1945, Ulaya nzima ambayo ilikuwa inakaliwa na Wajerumani, Ujerumani ya wa Nazi na washirika wake waliwaua Wayahudi wapatao milioni sita, karibu theluthi mbili ya idadi ya Wayahudi wote wa ulaya kwa wakati ule.

Mauaji hayo yalifanywa kwa watu wengi kwa njia za upigaji wa risasi kwa halaiki ya watu;sera ya mauaji ya kutokomeza watu kupitia kazi katika kambi za mateso; na katika vyumba vya gesi na gari za gesi katika kambi za kuangamiza za Wajerumani, haswa Auschwitz, Belzec, Chelmno, Majdanek, Sobibór, na Treblinka katika Poland iliyokaliwa na Wajerumani.

UCHUMI WA UJERUMANI KWA UFUPI
=============
Pamoja na Pato la Taifa la zaidi ya Euro trilioni 3.4, uchumi wa Ujerumani ulikuwa mkubwa zaidi barani Ulaya mnamo mwaka 2019. Chumi zenye ukubwa sawa za Uingereza na Ufaransa zilikuwa chumi za pili na wa tatu kwa ukubwa barani Ulaya wakati wa mwaka jana, ikifuatiwa na Italia na Uhispania.

Uchumi mdogo kabisa katika takwimu hii ni ule wa taifa dogo la Balkan la Montenegro, ambalo lilikuwa na Pato la Taifa la Euro bilioni 4.66 tu, karibu mara 74 ndogo kuliko uchumi wa Ujerumani.

Uchumi wa Ujerumani umekuwa ndio uchumi mkubwa zaidi barani Ulaya tangu mmwaka 1980, hata kabla ya kuungana tena kwa Ujerumani Magharibi na Mashariki. Uingereza, kwa kulinganisha, imekuwa na bahati wakati huo huo na ilikuwa na uchumi mdogo kuliko Italia mwishoni mwa miaka ya 1980.

Uingereza pia ilipata mapigo makubwa zaidi ya chumi zingine kubwa wakati wa anguko la uchumi wa mwishoni mwa miaka ya 2000, ikimaanisha uchumi wa Ufaransa ulikuwa wa pili kwa ukubwa barani kwa muda baadaye. Uchumi wa Uhispania ulikuwa wa tano kwa ukubwa Ulaya katika kipindi hiki cha miaka 38, na kutoka 2004 kuendelea umekuwa na thamani ya zaidi ya Euro trilioni moja.

Tazama takwimu kutoka chanzo sahihi hapo chini.

View attachment 1559175

Kwanini Ujerumani haijawahi kutafunwa na laana hii ya asili ya babu zao licha ya kuwaua Wayahudi zaidi ya Milioni 6 badala yake inazidi kuneemeka kiuchumi?

Mpaka Engineers bora wapo kwao>>> Kwanini wahandisi wazuri sana duniani (Magari, Mitambo) wanapatikana nchini Ujerumani? Siri yao ni ipi hasa?

Je, dhana hii ya laana ya asili ipo sahihi kweli?

ANGALIZO: Hii mada haizungumzii Wayahudi kama taifa teule la Mungu bali inazungumzia roho za binadamu wa asili ya Uyahudi. It's all about humanity and not ethnicity.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Ilikwisha tabiriwa na nikuabarishe Tu mababu wa Israel walijitabiria dam yaMasia iwe juu Yao na uzao wao ndicho kikatokea baada ya miaka mingi kupita.
 
Back
Top Bottom