Andiko la Prof. Mwalyosi la 2009 kutumika kama tathmini ya mazingira Stiegler's gorge; watakaopinga kufungwa

Andiko la Prof. Mwalyosi la 2009 kutumika kama tathmini ya mazingira Stiegler's gorge; watakaopinga kufungwa

Zurie

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2014
Posts
2,012
Reaction score
5,571
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Bw. Kangi Lugola amesema Bungeni siku ya Jumanne Mei 22 kuwa 'pepa' iliyoandaliwa na Prof. Raphael Mwalyosi kutoka IRA UDSM ya mwaka 2009 itatumika kama tathmini ya athari za kimazingira za ujenzi wa bwawa la Stiegler's.

Amesema, " Kwa taarifa yenu, Serikali itaendelea na utekelezaji wa mradi mpende ama msipende. Wanaopinga mradi huu wataishia jela"

Haya yote yalisemwa baada ya Wabunge kuonesha wasiwasi wao kuwa mradi unaenda kutekelezwa bila tathmini yeyote ya mazingira. Waziri wa Nishati, Dkt. Kalemani alijibu kuwa taratibu zote za kimazingira zitafuatwa kabla ya utekelezaji wa mradi.

Mradi huu utakaozalisha zaidi ya Megawati 2000, unatarajiwa kusababisha ukataji wa miti zaidi ya milioni 3 katika hifadhi ya Selous.

======

The deputy minister in the Vice President's Office responsible for union and environment Mr Kangi Lugola said in Parliament on Tuesday that a paper prepared by Prof Raphael Mwalyosi from the University of Dar es Salaam's Institute of Resource Assessment in 2009 would be used as the environmental impact assessment for the Stiegler's Gorge hydropower project.

"For your information, the government will go on with implementation of the project whether you like it or not. Those who are resisting the project will be jailed," he said.

This came after the Minister for Energy Dr Medard Kalemani revealed in the evening Parliamentary session, that all environmental procedures will be followed before actual implementation of Stiegler's Gorge hydropower project implementation.

Dr Kalemani was responding to concerns by MPs raised earlier in the day, that the project was being implemented before the environmental impact assessment was done.

When the Parliament sat as a committee earlier, chairman Mr Job Ndugai asked the energy ministry to ensure that Tanzania Electricity Supply Company Ltd (Tanesco) puts in place mitigation plans as the implementation would involve felling of more than three million trees.

Source: Anyone against Stiegler's Gorge project will be jailed
 
Amesema, " Kwa taarifa yenu, Serikali itaendelea na utekelezaji wa mradi mpende ama msipende. Wanaopinga mradi huu wataishia jela"..
 
Miti milioni tatu? Hawa jamaa wanataka kuigeuza hii nchi jangwa.

Mbona hawasemi kwanini hawaelekezi nguvu kwenye umeme wa gesi?
 
Miti zaidi ya milion 3, halafu still wanasema hawata haribu mazingira!! like seriously!?
 
3,000,000 trees[emoji849]
Hebu watupe case study ya nchi nyingine iliyowahi ku implement project iliyoleta madhara makubwa ya kimazingira kama hii.

Na je hali ikoje kwa sasa kwenye nchi hiyo hata baada ya kufanikisha mradi huo?
 
3,000,000 trees[emoji849]
Hebu watupe case study ya nchi nyingine iliyowahi ku implement project iliyoleta madhara makubwa ya kimazingira kama hii.
Na je hali ikoje kwa sasa kwenye nchi hiyo hata baada ya kufanikisha mradi huo??

Wewe sio mzalendo..
 
Aisee, Miti milion tatu sio mchezo. Kwanini tusirudi tuu kwenye gesi ambako miundombinu yote ishafanyika. Tuweke gas plant kubwa tuu pale Lindi na uzalishaji uanzie pale. Chenji itayobakia tuwekeze kwenye kilimo ili ku boost Sera ya viwanda na kurahisisha upatikanaji wa malighafi.
 
Miti milioni tatu wakishamaliza kuikata bado watakuwa na hiyo ndoto ya kupata MGWT 2000? Yani unaharibu chanzo cha mvua ambapo hiyo mvua ndiyo unayoitegemea kwenye kuzalisha umeme?

Serikali inayoongozwa na jiwe haijawahi kuwa na ufanisi!
 
Nimemsikia J.Makamba leo PB ya clouds fm anasema wataangalia cha kufanya
 
Kuna jamaa alisema wananchi wale nyasi ndege ya rais lazima inunuliwe alikaa lupango muda wake ulipoisha waambien wapunguze ngebe muda utawaumbua
 
Kama wanakata miti milioni tatu basi wawe na program ya kupanda miti mingine walau milioni tano
 
Lazima kuna upigaji mkubwa hapa wa pesa. Uwezi kumpeleka mtu jela kisa kakukosoa. Halafu mkiitwa kale kajina ka Tundu Lisu mnakuja juu eti mmetukanwa. Siku hizi wamebadilisha lugha eti ukiambiwa ukweli mchungu unakuwa umetukanwa. TATAKI mko wapi mtengeneze kamusi toleo mpya.
 
Aisee, Miti milion tatu sio mchezo. Kwanini tusirudi tuu kwenye gesi ambako miundombinu yote ishafanyika. Tuweke gas plant kubwa tuu pale Lindi na uzalishaji uanzie pale. Chenji itayobakia tuwekeze kwenye kilimo ili ku boost Sera ya viwanda na kurahisisha upatikanaji wa malighafi.
Watapigaje?
lazima waje na kitu kipya
 
Aisee, Miti milion tatu sio mchezo. Kwanini tusirudi tuu kwenye gesi ambako miundombinu yote ishafanyika. Tuweke gas plant kubwa tuu pale Lindi na uzalishaji uanzie pale. Chenji itayobakia tuwekeze kwenye kilimo ili ku boost Sera ya viwanda na kurahisisha upatikanaji wa malighafi.
SIJAWAHI kumsikia yeyote anatoa majibu ya gesi katika kuondoa tatizo la umeme
 
Back
Top Bottom