Andrew Chenge afika kwenye Kamati ya Katiba, awataka Wajumbe warudi kwenye Rasimu ya Warioba

Andrew Chenge afika kwenye Kamati ya Katiba, awataka Wajumbe warudi kwenye Rasimu ya Warioba

Wapo...ndiyo maana Dola yapasa kuamua Nani ashike hatamu,ukiacha demikrasia ufanye kazi kwa jamii isiyoelimika na kuitisa nchi kwenye bahari ya zahama
Kwenye hili naipenda sana CCM.wajinga wakiwa wengi na wakaunda chama alafu kikashikaa madaraka basi jua hiyo nchi inageuka kuwa jehanamu
 
Mzee Chenge , mtu anayeaminika kuwa miongoni mwa wanaccm wachache wenye busara , leo amefika kwenye Kamati ya Rais ya kuratibu maoni ya Katiba mpya na kueleza yaliyo moyoni mwake .

Chenge ambaye pia ni Mwanasheria wa Zamani wa Serikali ya Tanzania hakumung'unya maneno , amewataka wajumbe wa Kamati hiyo kurejea kwenye Rasimu iliyopendekezwa na Wananchi , Amedai ni kweli si rahisi kumzuia Rais wa Nchi kuteua Maofisa wa Serikali , lakini anawateua kwa utaratibu gani ? ni lazima Wateuliwa Waombe nafasi na Wasailiwe , amesema utaratibu huu ndio utakoiletea heshima nchi .

Chanzo : Mwananchi

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
Joka la Makengeza,msaka fedha, Mheshimiwa sana,Mtakatifu na Mpakwa mafuta,kiungo mchezeshaji wa Ufisadi FC,Mzee wa vijisenti na🤣🤣🤣Mwenyeheri Mtemi Andrew Chenge🤣🤣🤣
 
Tulimtukanaje na hilo linahusiana nini na maoni yake

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
Linahusiana kwa sababu bado chadema haijawahi kutoka hadharani kumsafisha Andrew Chenge dhidi ya tuhuma mlizowahi kumtuhumu kupitia "List of Shame" ya Mwembeyanga.

Mnapoongea muwe pia mnatunza kumbukumbu.
Kwa sababu wengi wa wafuasi wa Chadema,huwa hamjui kwamba kwenye Siasa hakuna "adui wa kudumu".
 
Mzee Chenge , mtu anayeaminika kuwa miongoni mwa wanaccm wachache wenye busara , leo amefika kwenye Kamati ya Rais ya kuratibu maoni ya Katiba mpya na kueleza yaliyo moyoni mwake .

Chenge ambaye pia ni Mwanasheria wa Zamani wa Serikali ya Tanzania hakumung'unya maneno , amewataka wajumbe wa Kamati hiyo kurejea kwenye Rasimu iliyopendekezwa na Wananchi , Amedai ni kweli si rahisi kumzuia Rais wa Nchi kuteua Maofisa wa Serikali , lakini anawateua kwa utaratibu gani ? ni lazima Wateuliwa Waombe nafasi na Wasailiwe , amesema utaratibu huu ndio utakoiletea heshima nchi .

Chanzo : Mwananchi

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
Angekuwa yupo ndani ya mfumo, kamwe asiongea hivi eti! Na hili ndilo tatizo la wana ccm walio wengi.

Wakiwa ndani ya mfumo akili zao zote zinahama kutoka kichwani na kwenda tumboni! Na wakitoka/wakitolewa na kuja huku nje tuliko sisi, akili zile zile zinahama kutoka tumboni na kurudi kichwani.
 
Back
Top Bottom