Andrew Chenge afika kwenye Kamati ya Katiba, awataka Wajumbe warudi kwenye Rasimu ya Warioba

Andrew Chenge afika kwenye Kamati ya Katiba, awataka Wajumbe warudi kwenye Rasimu ya Warioba

Hahaha....... Chadema mnayumba sana!
Chadema imekuwa ikisisitiza Tangu Bunge la Katiba kuheshimiwa Kwa rasmu ya Warioba ambayo ilibeba maoni ya Wananchi. Leo Chenge ambaye alishiriki Sana kwenye Katiba iliyopendekezwa ya kiCCM, ameona alipokosea na kutamka Wazi Rasmu sahihi ni ya Warioba na siyo iliyochakachuliwa na kuitwa Katiba inayopendekezwa. Hapo Chadema wamegeuka nini?
 
Mzee Chenge , mtu anayeaminika kuwa miongoni mwa wanaccm wachache wenye busara , leo amefika kwenye Kamati ya Rais ya kuratibu maoni ya Katiba mpya na kueleza yaliyo moyoni mwake .

Chenge ambaye pia ni Mwanasheria wa Zamani wa Serikali ya Tanzania hakumung'unya maneno , amewataka wajumbe wa Kamati hiyo kurejea kwenye Rasimu iliyopendekezwa na Wananchi , Amedai ni kweli si rahisi kumzuia Rais wa Nchi kuteua Maofisa wa Serikali , lakini anawateua kwa utaratibu gani ? ni lazima Wateuliwa Waombe nafasi na Wasailiwe , amesema utaratibu huu ndio utakoiletea heshima nchi .

Chanzo : Mwananchi

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
Huyu ni mshenzi Sana! Ndio aliharibu mchakato wote!

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
FISADI papa Andrew John Chenge. Uzuri ukitaka akili za mwafrika zimrudie mtoe nje ya duara la kula ubwabwa.
 
Linahusiana kwa sababu bado chadema haijawahi kutoka hadharani kumsafisha Andrew Chenge dhidi ya tuhuma mlizowahi kumtuhumu kupitia "List of Shame" ya Mwembeyanga.

Mnapoongea muwe pia mnatunza kumbukumbu.
Kwa sababu wengi wa wafuasi wa Chadema,huwa hamjui kwamba kwenye Siasa hakuna "adui wa kudumu".
Kwamba kwa vile Chenge ni fisadi basi habari zake kuhusu Katiba zifichwe ?

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Mzee Chenge , mtu anayeaminika kuwa miongoni mwa wanaccm wachache wenye busara , leo amefika kwenye Kamati ya Rais ya kuratibu maoni ya Katiba mpya na kueleza yaliyo moyoni mwake .

Chenge ambaye pia ni Mwanasheria wa Zamani wa Serikali ya Tanzania hakumung'unya maneno , amewataka wajumbe wa Kamati hiyo kurejea kwenye Rasimu iliyopendekezwa na Wananchi , Amedai ni kweli si rahisi kumzuia Rais wa Nchi kuteua Maofisa wa Serikali , lakini anawateua kwa utaratibu gani ? ni lazima Wateuliwa Waombe nafasi na Wasailiwe , amesema utaratibu huu ndio utakoiletea heshima nchi .

Chanzo : Mwananchi

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
Huyu Mh kwangu ni Genius. Hatakama alipiga. Hiki kichwa nihatari.
 
Back
Top Bottom