Andrew Chenge afika kwenye Kamati ya Katiba, awataka Wajumbe warudi kwenye Rasimu ya Warioba

Andrew Chenge afika kwenye Kamati ya Katiba, awataka Wajumbe warudi kwenye Rasimu ya Warioba

Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na mbunge wa zamani wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge amesshauri muundo na utaratibu wa uteuzi wa viongozi wa Tume ya Uchaguzi utumike uliopo kwenye Katiba pendekezwa.

Chenge aliyekuwa mwanasheria mkuu wa Serikali kati ya mwaka 1993 hadi 200, amesema hayo leo Ijumaa Julai 15, 2022 baada ya kutoka kuwasilisha maoni yake kwenye Kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa katika ofisi ndogo za Bunge Dar es Salaam.

CHANZO: mwananchi_official
 
Baada ya kung'atwa, akili imerudi sehemu yake sahihi.

Angekuwa bado ni Mbunge wa Bariadi, usingemsikia akisema chochote kuhusu Katiba, kama ilivyo kwa wabunge wenzake aliowaacha kule Dodoma.
 
Mzee Chenge , mtu anayeaminika kuwa miongoni mwa wanaccm wachache wenye busara , leo amefika kwenye Kamati ya Rais ya kuratibu maoni ya Katiba mpya na kueleza yaliyo moyoni mwake .

Chenge ambaye pia ni Mwanasheria wa Zamani wa Serikali ya Tanzania hakumung'unya maneno , amewataka wajumbe wa Kamati hiyo kurejea kwenye Rasimu iliyopendekezwa na Wananchi , Amedai ni kweli si rahisi kumzuia Rais wa Nchi kuteua Maofisa wa Serikali , lakini anawateua kwa utaratibu gani ? ni lazima Wateuliwa Waombe nafasi na Wasailiwe , amesema utaratibu huu ndio utakoiletea heshima nchi .

Chanzo : Mwananchi

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
Tatizo viongozi wa Tanznia ni wanafiki sana ..... wakiwa madarakani hawasemi kitu cha maana zaidi ya kukifurahisha chama na serikali. Wakitoka ndiyo ile guilty conscious inawaingia ..... sijui huwa wanakumbuka kuwa siku zimekaribia ....!! Maana wakati Bunge la katiba linashiriki kuipindisha Rasimu ya Warioba huyu bwana alikuwepo na alishirikiana vizuri tu na wana CCM wenzake .... Hawa Wazee huwa sometimes wanatia hasira sana ....!!
 
Sio ajabu,.atakuwa ameonja shubiri ya mamlaka ya kifalme
..aliyeyumba ni Andrew Chenge, sio Chadema


..Chenge ndiye aliyechakachua rasimu ya Warioba na kutoa katiba pendekezwa.

..Ni ajabu Chenge kugeuka na kudai rasimu na mapendekezo ya Warioba yazingatiwe.
 
Chenge huyu ndio mlimtukana matusi yote? Leo kawa mzuri?
Ndiyo, ni mzuri;

✓Hakuna mtu mbaya ama mzuri kwa 100%, UKIWEMO WEWE...

✓Kila binadamu ana pande mbili. Yaani upande wa udhaifu na ule wa uimara/mazuri, UKIWEMO WEWE...

✓ Hakuna mtu ambaye ana maadui tu, UKIWEMO WEWE...

✓ Hakuna mtu ambaye anapendwa na watu wote, UKIWEMO WEWE..

✓ Hakuna mtu ambaye ana maadui wote, UKIWEMO WEWE..

## Wewe ndiye mwenye matatizo iwapo mchana kutwa umetazama madhaifu au mabaya ya mtu pekee yake..

## Ili usiumie, nakushauri tazama upande wa mazuri ya mtu hata mara moja tu kwa kutwa, utauona uponyaji wako...!!

CC: SINGLE WINDOW
 
Ccm watapinga kisa wao wanataka serikali 2 ambazo kimasingi Tanganyika kavalishwa koti la muungano..huku zenji akiafidi muungano kupitia jasho la watanganyika.

Viongozi waccm uchuwenu wa madaraka mnaumiza watanganyika.

Twende na serikali moja la ziwepo tatu..sisi watanganyika tumeimisi Tanganyika yetu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom