Anga la Tanzania lafungwa kwa safari zote za abiria za kimataifa

Anga la Tanzania lafungwa kwa safari zote za abiria za kimataifa

Bora dini ambayo inajulikana ni jambo la imani kuliko huu upuuzi wa siasa,ukiangalia comments za watu humu unaona ni jinsi gani watu akili zao zilivyoathiriwa na siasa na zimeharibiwa kabisa.
 
Ndio tuna anza kujitegemea na zile dola zinazo tutosha kujiendesha kiuchumi miezi zaidi ya sita
 
Nadhani Covid-19 amekuja kutupa fundisho! Kuna 'clip' moja ya Mkenya akisema ni fundisho ili tuimarishe mifumo yetu ya afya. Mimi naongeza, tujitathimini kama nchi nzima tunatakiwa tuendelee kuwa tunasubiri matamko ya mkuu wa 'inchi'. Nafikiria, kweli katika wakati kama huu tunasubiri mtu mmoja ajisikie yeye na kuamua tufanye nini!! Nyakati za kimaamuzi kama hizi ndizo hunifanya kuwaelewa sana wanaopigia kelele 'Katiba'.

Zaidi ya kufunga taasisi za elimu na kusimamisha michezo, tukiri hadi sasa hakuna tulichofanya. Hii kufunga anga ni kiini macho kabisa. Mashirika ya ndege (zaidi ya Ethiopia pekee nafikiri) yalisimamisha safari zote. Na zaidi tukiangalia takwimu za wwanaotangazwa kwa sasa, kesi zimehamia katika 'maambukizi ya ndani/wenyewe kwa wenyewe'.

Hii hatua ya kufunga anga ni sahihi lakini ilikuwa ya miezi kadhaa nyuma, kuifanya sasa ni kujikosha tu kwa Watanzania. Kwa hali ilivyo ya sasa Tanzania inahitaji njia ya kupunguza maambukizi ya ndani. Nchi nzima tunasubiri mtu mmoja ajisikie!!!
 
Taratibu wameanza kufuata ushauri wa Kamanda Mbowe
Serikali isipofanya wasemavyo upinzani, inalalamikiwa. Ikifanya, inadhihakiwa kwamba imefanya tulivyosema.

1. Upinzani hauna monopoly ya mawazo. Serikali ikifanya kitu kilichosemwa na upinzani isichukuliwe moja kwa moja kwamba imefanya hivyo kwa shinikizo lao. Inawezekana ilikuwa inasubiri tu muda muafaka wa kutekeleza hilo.

2. Kwa yale ambayo ni kwa uhakika kwamba serikali imefanya kutokana na ushauri wa upinzani, tushukuru kwamba serikali imepokea ushauri wa upinzani. Hiyo ndiyo demokrasia halisi. Siyo kuanza kuibeza. Usipinge kitu kwa kuwa tu kimesemwa na mpinzani hata kama unakiona ni sahihi.

Si busara kuleta siasa kila mahali. Tuunganishe juhudi zetu kupambana na tatizo lililopo. Serikali itimize ushauri wo wote mzuri bila kujali unatoka wapi. Na upinzani wasilete maneno maneno ya kisiasa kuibeza serikali ikifuata mapendekezo yao, hata kama ni kweli serikali imetimiza ushauri wa upinzani.

Hivi ndivyo tutasonga mbele na hiyo ndiyo faida ya demokrasia. Demokrasia siyo upinge tu kila kitu kitokacho kwa mpinzani wako. Hiyo ni demokrasia uchwara, na upinzani Tanzania hawana budi kulifahamu hilo.
 
Kwahiyo wale watalii wa kichina hatutaendelea kuwapokea tena?
 
Taratibu wameanza kufuata ushauri wa Kamanda Mbowe
Ndiyo tatizo la hawa watawala wakipewa ushauri mwanzoni wanaanza kudharau na kudhihaki kuwa wanaotoa ushauri ni nyumbu lakini mambo yakizidi wanafuata ushauri ule ule walioukataa.
 
Hata lockdown itakuja tu ni swala la muda, jpm hatumii akili, anawaambia watz chapeni kazi yeye kakimbia dar kaenda kujificha vijijini huko, anga lilitakiwa kufungwa mda sana, wameona tbc mzigo umeanza kutafuna watu ndio wameshtuka

Sent using Jamii Forums mobile app
Usilete mifano ambayo wala haihusiani. Kufunga mpaka wa nchi kunahusikana vipi na vifo vilivyotokea TBC? Serikali imesema tufanye kazi, lakini tuzingatie mawaidha yanayotolewa na wataalamu wa afya, kama vile kutosongamana.

Wafanyakazi wa TBC walionekana wakisherehekea kwenye hafla, wanapongezana kwa kushikana mikono na hata kulishana keki kwa mikono mitupu. Siku chache baada ya tukio hilo watatu kati ya hao walioonekana kwenye clip wakafariki.

Mola awalaze pema. Hatuna nia ya kuwasema vibaya marehemu lakini tukio hilo linabakia kuwa fundisho kwetu tuliosalia kwamba tuitikie maelekezo tunayopewa. Mbona hakujatokea yaliyotokea TBC mahali pengine pa kazi?

Au mpaka ungekuwa umefungwa na hapo TBC wakaendelea na waliyokuwa wakifanya wangesalimika kwa kuwa tu mpaka umefungwa? Tusilete porojo za kisiasa katika kila jambo. Tufanye yaliyomo kwenye uwezo wetu kadiri tunavyoelekezwa. Mengine tumuachie Mola.
 
Hivi ni Raisi pekee mwenye mamlaka ya kupiga lockdown au kuna wengine tofauti na rais wenye huo uwezo..???? kama mahakama nk. naomba kujua

kwako Pascal Mayalla
 
Ile kauli ya kuambiwa tufanye kazi usiku na mchana mbona imekiukwa,Bado mipaka sasa kufungwa
 
Tulijua tu, hakuna ujanja. Watu wenye akili wanajua hali ya maambukizi ni mbaya kuliko inavyoelezwa.
Unaweza ukagoma au ukachelewa kuchukua hatua mapema lakini mwisho wa siku hali halisi ikakulazimisha kuchukua hatua.

Tumeanza na hilo la safari, soon social gathering zitapigwa marufuku then partial lockdown itafuata.

Tutakuja hapa hapa JF kukiri hayo.
Lol..Nchi hii!?

Hizo unazozitaja si ndo hatua zenyewe za kuchukua? Au wewe ulitaka ianze hatua gani?
 
Mamlaka ya Usafiri wa Anga imefuta safari zote za ndege za abiria za kimataifa tangu jana.

Ndege za mizigo tu ndio zitaruhusiwa kuingia kwa masharti kuwa wafanyakazi wa ndege hizo watawekwa quarantine kwa gharama zao.

At last, wanasiasa wamesikiliza ushauri wetu juu ya Corona pandemic.

[emoji4][emoji4][emoji4]sisi kama kamati ya wachawi tutaenda kulijadili hili tuone kama inafaa kusitisha safari zetu pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom