Pre GE2025 Angalia CCM jinsi wamemtuma Kijakazi Yunus Kumhoji Tundu Lissu kwa Kivuli cha Clouds Media

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

View: https://www.youtube.com/live/h9cHr7NLIBA?si=L-nYOeceS1NrpmnVKasoro kubwa katika interview hii ya leo katika kipindi cha hiki cha 360° Clouds TV:

1. Ni mtangazaji huyu wa kike (Kijakazi Yunus) kutokuwa makini ktk kazi yake. Angalia alivyokaa, anachofanya, anauliza swali na haoneshi umakini wowote ktk kusikiliza na matokeo yake maswali nyongeza (follow up questions) kutoka kwake ktk interview hii kuwa "very vague" kuonesha kuwa hafuatilii majibu ya maswali aliyouliza mwenyewe...

2. Ni wazi kuwa hakujiandaa kwenda kufanya mahojiano na mtu wa aina ya Tundu Lissu ambaye naweza kusema hamjui vizuri au alidhani anajua zaidi kuliko yeye...

3. Hili #2 hapo juu inathibitishwa na kukosa kwake umakini kiasi cha maswali yake kuwa ya shaghala-baghala kwa sababu hasikilizi majibu yake toka kwa anayemuuliza maswali. Ikafika time anamtaka mfanyiwa mahojiano aanze kumhoji mtangazaji...!!

4. Ilifika wakati Tundu Lissu (mhojiwa) kumrejesha mtangazaji kwenye mstari na kumwambia "kuwa makini, Fuatilia logic ya maelezo yangu..."

5. Kwa maoni yangu huyu Mtangazaji (Dada Kija), hafai kuongoza kipindi cha kuhojiana na watu wenye akili na ufahamu mkubwa kama Tundu Lissu badala yake ahojiane na waimba taarabu na miziki ya mipasho huko...!!
CC: @CloudsTV
 
Kwani kusema ukweli ni kumtuhumu mtu? Kama Lisu kasema uongo dhidi ya mwenyekiti au mtu mwingine si ndio mahali kumkamata Lisu kwa kuweka ukweli hadharani? .Nimewaona baadhi ya wanahabari wakimwuliza makamu maswali ya mitego wakidhani atashindwa kujibu na kumpunguzia umaarufu kumbe ndo wanampiga teke chura na kumwongezea umaarufu zaidi.kuongea ukweli si kumtuhumu mtu
 
Dah, think tank ya lissu hiyo🤣🤣🤣🤣
 
EATV alikuwa mtangazaji wa muziki wa bolingo sasa hii ya siasa ni kumtupa baharini wakati hajui kuogelea.
Mkuu wana nanjaa asipojitupa hapa na pale anakuwa hana kazi.

Media zenyewe unakuta zina watangazaji wasiozidi 6. Hivyo wanalazimika kuendesha vipindi vyote hata kama hawana ujuzi huo.

Kuna Mdau alisema TV Imaani ina watangazaji watatu tu. Asubuhi hadi usiku wanabadilishana shifti tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…