Angalia daraja Mbuchi na Mbwera Kibiti la Bilioni 7.2 lililojengwa na Rais wetu Mpendwa Samia Suluhu. Tujipongeze

Angalia daraja Mbuchi na Mbwera Kibiti la Bilioni 7.2 lililojengwa na Rais wetu Mpendwa Samia Suluhu. Tujipongeze

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Salaam wakuu,

Ni baraka na Neema iliyoje kumpata Rais mwenye Uchungu na Mali za Umma? Hakika Mungu anatufundisha na kutuonesha Umakini wa Rais wetu Samia Suluhu. Mungu anatuonesha Uwezo wa kufuatilia mambo wa Rais samia na wakati wa kupiga kura hatutaumiza kichwa kujua ubora wake kwani tumeona Uwezo wake wa juu wa kupambana na Ufisadi. Huu ndo uwezo wake wa juu wa utendaji ambao Mungu kamjalia.

Hii imepelekea Wakazi wa Kata za Mbuchi na Mbwera Kibiti Mkoani Pwani wamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa daraja la Mbuchi lenye urefu wa mita 61 linalounganisha kata hizo ambao umegharimu shilingi bilioni 7.2.

Hongera sana Rais Samia Suluhu Hassan. Hakika wewe ni kielelezo cha Wanawake.

Kazi iendelee.

Asitokee mtu akamkosoa rais kwa utendaji huu. Tumpigie makofi tu kama anavyotaka. Kama Watawala wanaafiki hi kitu inatusaidia kujua akili zao na madhumuni ya kugombania vyeo.

Hadi sasa sijajua Watanzania wana uhusiano gani na Mungu. Hadi tunapata Viongozi/Watawala wa hivi.

Tumewaseti watu wapongeze, then tunawapa elfu 50 kila mmoja. Angalia Video. Majaliwa mjanja sana

FB_IMG_1669711313757.jpg
FB_IMG_1669711318217.jpg
 
Huku ni kwetu kwa 100%, hakuna watu wajinga na wanapigwa hela kama watu wa Rufiji wao wanajiona wanajua kila kitu. Ni watu wa hovyo sana hii jamii. Wana maisha duni sana na wana ardhi nzuri nenda ukaone maisha yao. Sasa hilo daraja wanaona kama vile wametengenezewa kitu cha maana. Baranbara zao zipo duni sana.

Nenda pale Temeke Sudan kaangalie mabasi yao ya kwenda Rufiji ni moja tu ndio roho yao basi la Akida, hawa watu wanatakiwa kupatiwa elimu ya mageuzi ya kifikra kubwa sana.

Unatoka Dar es Salaam pale Temeke mpaka kuingia Rufiji kule Mloka ni siku nzima. Huyu Mchengelwa yupo na Wabunge wa huko wapo kimya.

Hili daraja ni kituko cha mwaka. Wanasiasa hasa CCM wameshaona wakazi wa Rufiji hawafai kupewa maendeleo.
 
Salaam wakuu,

Ni baraka na Neema iliyoje kumpata Rais mwenye Uchungu na Mali za Umma? Hakika Mungu anatufundisha na kutuonesha Umakini wa Rais wetu Samia Suluhu....
Bilioni 7 zingeweza kujenga daraja la zege, la kudumu na chenchi kubaki kwa maendeleo mengine! Hilo ni daraja la muda ambalo life span yake haitazidi miaka 25 kabla kudai matengenezo!
 
Bilioni 7.2 kwa urefu wa mita 61 tena single lane bila kuwa na pedestrian. Ni wizi mkubwa hapo tayari, mleta mada umemuharibia mama badala ya kusifu.
Inaweza ikawa ni njia pia ya kuibua ubadhirifu kama upo! Sidhani kama Mhe amslifungua, ila anashukuriwa. Hivyo, mada husika inaweza toa nafasi ya ufuatiliwaji na hatua!
 
Huku ni kwetu kwa 100%, hakuna watu wajinga na wanapigwa hela kama watu wa Rufiji wao wanajiona wanajua kila kitu. Ni watu wa hovyo sana hii jamii...
Last wiki nilikua na zoezi moja wilaya ya rufiji..hali inatisha sana asee..barabara mbovu sana..jamii imechoka sana.

#MaendeleoHayanaChama
 
Na ni vyuma tupu!
Bilioni 7.2 kwa urefu wa mita 61 tena single lane bila kuwa na pedestrian. Ni wizi mkubwa hapo tayari, mleta mada umemuharibia mama badala ya kusifu.
 
Hii ina maana kila hatua moja imegharimu takribani milioni 118 na usheee.
Tujipigie makofi tafadhali[emoji122][emoji122][emoji122]
Hii ni hatari sana!! Kama hakuna approach road ya Kiwango Cha lami kila upande Kwa km 2, huu upigaji umevuka mipaka
 
Back
Top Bottom