Salaam wakuu,
Ni baraka na Neema iliyoje kumpata Rais mwenye Uchungu na Mali za Umma? Hakika Mungu anatufundisha na kutuonesha Umakini wa Rais wetu Samia Suluhu. Mungu anatuonesha Uwezo wa kufuatilia mambo wa Rais samia na wakati wa kupiga kura hatutaumiza kichwa kujua ubora wake kwani tumeona Uwezo wake wa juu wa kupambana na Ufisadi. Huu ndo uwezo wake wa juu wa utendaji ambao Mungu kamjalia.
Hii imepelekea Wakazi wa Kata za Mbuchi na Mbwera Kibiti Mkoani Pwani wamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa daraja la Mbuchi lenye urefu wa mita 61 linalounganisha kata hizo ambao umegharimu shilingi bilioni 7.2.
Hongera sana Rais Samia Suluhu Hassan. Hakika wewe ni kielelezo cha Wanawake.
Kazi iendelee.
Asitokee mtu akamkosoa rais kwa utendaji huu. Tumpigie makofi tu kama anavyotaka. Kama Watawala wanaafiki hi kitu inatusaidia kujua akili zao na madhumuni ya kugombania vyeo.
Hadi sasa sijajua Watanzania wana uhusiano gani na Mungu. Hadi tunapata Viongozi/Watawala wa hivi
View attachment 2430635
View attachment 2430613View attachment 2430614