Angalia Jinsi Akili Bandia (AI) Inavyoanza kupumzisha Wachoraji wa katuni na Wengineo

Hii ni aina gani ya AI generator Mkuu hebu nipatie link
 
Bora ni focus kusoma vizuri hii Al
Maana hata kama inarahisisha mambo bado kuna watu hawajui matumizi yake ni wachache sana ndo wanaelewa haya mambo ...
Mkuu huo ndo ukweli AI kama hujui kuweka reasonable prompt always unaweza ukaona ina majibu yasiyojitosheleza inahitaj elimu ya ziada kujua viti vya muhimu
 
Mkuu huo ndo ukweli AI kama hujui kuweka reasonable prompt always unaweza ukaona ina majibu yasiyojitosheleza inahitaj elimu ya ziada kujua viti vya muhimu
Yaaah ni hivo mkuu..
Ina rahisisha mambo mengi mno lakini ishu ni je kila mtu anaweza kutumia....
Mfano mzuri hii ishu imefikia mpaka kwa music industry..
Sio kila producer anaelewa haya mambo.
 
Sidhani Kama itaweza kufikia uwezo wa binaadam halisi kwa asilimia 100. (Sio hawa wa maabara wa sasa)







Unachokunywa kinatosha. Nenda nyumbani.
unaifahamu croud computing, unaifahamu quantum computer.
Mpaka sasa wewe huna uwezo kama Bard au Chat gpt.
Yaani huo uwezo huna! huna! huna!
Labda uwezo wa kusikia njaa.
Labda hisia za ngono.
Ulimwengu tunaoenda ni mwingine kabisa msije mkasema hamkupewa tahadhari .
ISA wapo kuunda sera kudhibiti AI.
Hilo dude lisipodhibitiwa ni NOMA.
AI ni maakili ya geneus wengi unaowajua wewe wote.
Je wewe ujatajua mambo ya mageneus wote duniani?
Hilo dude si halisi.ni .Wewe kuwa halisi haimaanishi unauwezo mkubwa.
Wewe hapo ni halisi ila huna uwezo wa kubeba mizingo kama trekta ambayo sio halisi.
 



Nani katengeneza vyote hivyo na kuvipa uwezo huo?


Wewe hujui hata kucha yako imetengenezwa na nani.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ unavokuza mambo sasa....
 
Msomi mmoja aliwahi kusema...

"Asili ya ubongo wa mwana-Adam ni uliojikunja na kujinyongorota ndani ya fuvu la kichwa. Endapo utakunjuliwa unaweza kutoka bara la Amerika mpaka Afrika na kurudi na kwenda tena mara nne! (Yaani round nne)"

Hiyo ni Falsafa na ilikuwa na maana kubwa sana juu ya uwezo ambao anao mwanadamu. Tumejibweteka na hatutaki kushughulisha vichwa. Vyote hivyo unavyosifia vimeundwa na huyuhuyu mwana-Adam kwa karama na uwezo aliojaaliwa na mungu muumba, na ametuahidi tayari mpaka kwenye maandiko yake matakatifu kwamba bado kuna mengi makubwa tunaweza kuyafanya na kuyakamilisha endapo tutatumia ipasavyo bongo zetu.

ila cha kushangaza kuna wapuuzi wachache wa aina yako wanavisifia hivi vitu kwamba vinamzidi mwanadamu wa kawaida uwezo.

Unachekesha sana!
 
hii ni picha iliyochorwa kwa mkono zaidi ya karne kadhaa, artificial intelligence bado itakuwa na kibarua cha ziada kuweza kufuta karama ya uchoraji View attachment 2807021
Lakini tukubali kuwa mfano Da Vinci angekuwa hai, AI ina uwezo mkubwa sana wa kujifunza kutoka kwa Da Vinci na kuwa bora kama Da Vinci Au zaidi.
 
Acha kubishana na mtu asiyejua technolojia mkuu..

Kunakitu kwenye AI kinaitwa AoT (algorithms of Thought)

Pia kuna AI waliizuia OpenAI ilikuwa inauwezo wa kuweza kurun algorithm na kujua unafikiri nini ili ikupatie..
Sasa yeye anaweza kufanya hivyo kama anashindwa kujua hata mawazo ya paka wake nyumbni atajua mawazo ya binadamu?
Kuna wakati tukubali kwa sasa machine zitatushinda tu..

Na sasa hivi BIOENGENEERING IMEUNGANA NA AI company na wanacreate watu yaani wanafanya Genetic engeering kwa kufanya cloning ya copy ya binadamu walio hai na mtu kupata double cloned structure
 
Lakini tukubali kuwa mfano Da Vinci angekuwa hai, AI ina uwezo mkubwa sana wa kujifunza kutoka kwa Da Vinci na kuwa bora kama Da Vinci Au zaidi.
Uzuri ni kwamba unaweza kupromt AI ikafikiri au ikachora kam da vinci picha yoyote...
Kuna kipindi niliwahi kuuliza AI inipe mawazo ya magufuli kwenye.matter fulani hivi yaani kama angekuwepo angefanya nini na Angechukua jukumu gani na speech yake ingekuwaje...ikanipa
 
Dr ulianza vizuri tuu.
Ila hapo kwa machine zinatushinda
Nakushusha vyeo πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ
 
Mkuu hapo kwa ubongo nishushe kaka! Hii safari siwezi kuendelea 🀣🀣🀣
Kwamba ukunjue ubongo utoke Afrika mpaka Marekani na kurudi mara nne Aah mkuu nishushe sipandi mwndokasi 🀣🀣
 
Mkuu hapo kwa ubongo nishushe kaka! Hii safari siwezi kuendelea 🀣🀣🀣
Kwamba ukunjue ubongo utoke afrika mpaka marekani na kurudi mara nne Aah mkuu nishushe sipandi mwndokasi 🀣🀣
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ hii kateleza bahati mbaya bana msamehe
 
Dr ulianza vizuri tuu.
Ila hapo kwa machine zinatushinda
Nakushusha vyeo πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ
Mkuu kuna watu wanashindwa hao ambao hawajishughulishi...
Kwa mfano we unaona unaweza ukatengeneza kitu walau kwenye Computer ila kuna mtu computer kazi yake yeye ni kucheza game,Kuangalia mobi na suffing ...
Huyu mtu ntamuitaje ??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…