Angalia tofauti ya Rwanda na Tanzania kwenye masuala ya utalii. Tanzania tuna cha kujifunza kutoka Rwanda

Rwanda haina mbuga ya wanyama wala vivutio vyovyote vya kitalii kama ilivyonavyo Tanzania lakini mwaka 2022 Rwanda ilipokea watalii milioni 1.1 huku Tanzania ikipata watalii milioni 1.6 pamoja na kua na vivutio vya utalii visivyo na Idadi.
Wakiwa majukwaani wanasifia sana mafanikio ya utalii lakini tukija kutazama tulichovuna unasomewa changamoto tangu introduction mpaka hitimisho
 
Bahati mbaya sana Tanzania akili ndogo inatawala akili kubwa
Ndio chanzo cha kufeli kwenye mambo mengi.
Bodi ya utalii yenyewe walio jazana huko wengi unakuta ni wazee, wasio na ubunifu Makada wa chama walio pewa nafasi kwa kulipana fadhila

Wanachozingatia ni vikao na posho na hawawezi kumshauri mama hayo mabango yake huko barabarani ya kuuza sura yabadilishwe yawe ya vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini
 
Mabango ya Samia yanakera basi tu aisee.

Hapo kabla yalikua ni mabango ya biashara, haya ya raisi sidhani kama hata yanalipiwa.
 
Kwanza tuanze na takwimu za kijiografia.

Rwanda ni ndogo kuliko mko wa Tabora. Rwanda ina ukubwa wa Kilomita za mraba elfu 26, Tabora ina ukubwa wa mraba kilomita elfu 29.

Rwanda ina watu wasiozidi milioni 12. Tanzania ina watu zaidi ya milioni 61.

Rwanda haina mbuga ya wanyama wala vivutio vyovyote vya kitalii kama ilivyonavyo Tanzania lakini mwaka 2022 Rwanda ilipokea watalii milioni 1.1 huku Tanzania ikipata watalii milioni 1.6 pamoja na kua na vivutio vya utalii visivyo na Idadi.

Jana, tarehe 2.11.2023 Rwanda imetangaza kufuta visa ama kibali cha mtu yoyote kutoka Afrika kuitembelea Rwanda, kwenda Rwanda ni kama unaenda nyumbani kwako, hakuna wa kukuuliza masuala ya visa wala nini.

Rwanda inafanya matangazo ya vivutio vyao vidogo walivyonavyo kwenye klabu kubwa za mpira Duniani. Ukifika Rwanda mabango yote yanatangaza vivutio vya utalii. Tanzania kila barabara matangazo ni ya Rais Samia kuupiga mwingi.

Rwanda imekua nchi ya nne Afrika kufuta Visa kwa Waafrika wenzao ikitanguliwa na nchi nyingine kama Benin.

Je, Tanzania tuna cha kujifunza kutoka Rwanda?
Murakoze
 
Utalii wa Rwanda ni limited Sana, utalii wa msituni kuangalia sokwe, ni vigumu mtalii kurudi kutalii labda kama anafuatilia mbususu.

Kumbuka Rwanda Wana utalii wa kupromote mbususu zao
 
Basi Rwanda wamefeli walitakiwa wawe na watalii hata 7M au 10M, investment ambayo Rwanda ameifanya ni kubwa sana kuliko Tanzania.

Visit Rwanda Arsenal na PSG, watu wanaofuatilia mpira ni wengi sana na pesa waliyolipa ni kubwa mno kutangaza sekta yao ya utalii nafikiri siku Tanzania ikitumia same approach itafanya maajabu, ingawa hofu yangu sisi Watanzania ni walalamishi hapo zingekuja hoja watu wanakula mlo mmoja nyie mnaenda kuwapa pesa Arsenal?

Tunapenda matokeo ila hatupendi njia zinazoleta mafanikio.
Rwanda hawana mbuga za wanyama kama za Tanzania,haina vivutio vingi na vyenye hadhi kama vya tanzania, bado tunakaribiana kwa idadi ya watalii,wangekuwa na mbuga moja tu kama ngorongoro wangefikia hiyo idadi ya 7m au zaidi.
 
Kwanza tuanze na takwimu za kijiografia.

Rwanda ni ndogo kuliko mko wa Tabora. Rwanda ina ukubwa wa Kilomita za mraba elfu 26, Tabora ina ukubwa wa mraba kilomita elfu 29.

Rwanda ina watu wasiozidi milioni 12. Tanzania ina watu zaidi ya milioni 61.

Rwanda haina mbuga ya wanyama wala vivutio vyovyote vya kitalii kama ilivyonavyo Tanzania lakini mwaka 2022 Rwanda ilipokea watalii milioni 1.1 huku Tanzania ikipata watalii milioni 1.6 pamoja na kua na vivutio vya utalii visivyo na Idadi.

Jana, tarehe 2.11.2023 Rwanda imetangaza kufuta visa ama kibali cha mtu yoyote kutoka Afrika kuitembelea Rwanda, kwenda Rwanda ni kama unaenda nyumbani kwako, hakuna wa kukuuliza masuala ya visa wala nini.

Rwanda inafanya matangazo ya vivutio vyao vidogo walivyonavyo kwenye klabu kubwa za mpira Duniani. Ukifika Rwanda mabango yote yanatangaza vivutio vya utalii. Tanzania kila barabara matangazo ni ya Rais Samia kuupiga mwingi.

Rwanda imekua nchi ya nne Afrika kufuta Visa kwa Waafrika wenzao ikitanguliwa na nchi nyingine kama Benin.

Je, Tanzania tuna cha kujifunza kutoka Rwanda?
Hakuna cha kujifunza.
Rwanda ni sawa na mtu anaewekeza mtaji mkubwa akivuna faida ndogo.
Pesa anazotumia kujitangaza nje ni nyingi hazilingani na faida anayoingiza katika utalii.
 
Kwanza tuanze na takwimu za kijiografia.

Rwanda ni ndogo kuliko mko wa Tabora. Rwanda ina ukubwa wa Kilomita za mraba elfu 26, Tabora ina ukubwa wa mraba kilomita elfu 29.

Rwanda ina watu wasiozidi milioni 12. Tanzania ina watu zaidi ya milioni 61.

Rwanda haina mbuga ya wanyama wala vivutio vyovyote vya kitalii kama ilivyonavyo Tanzania lakini mwaka 2022 Rwanda ilipokea watalii milioni 1.1 huku Tanzania ikipata watalii milioni 1.6 pamoja na kua na vivutio vya utalii visivyo na Idadi.

Jana, tarehe 2.11.2023 Rwanda imetangaza kufuta visa ama kibali cha mtu yoyote kutoka Afrika kuitembelea Rwanda, kwenda Rwanda ni kama unaenda nyumbani kwako, hakuna wa kukuuliza masuala ya visa wala nini.

Rwanda inafanya matangazo ya vivutio vyao vidogo walivyonavyo kwenye klabu kubwa za mpira Duniani. Ukifika Rwanda mabango yote yanatangaza vivutio vya utalii. Tanzania kila barabara matangazo ni ya Rais Samia kuupiga mwingi.

Rwanda imekua nchi ya nne Afrika kufuta Visa kwa Waafrika wenzao ikitanguliwa na nchi nyingine kama Benin.

Je, Tanzania tuna cha kujifunza kutoka Rwanda?
Kinacho tafutwa ni soko , fikiria Una nyumba ya kulala wageni yenye vyumba 10, na idadi ya wateja ni wawili yaani hiyo ni Rwanda, inabidi uongeze wateja ili vyumba vijae, vivyo hivyo kwenye huduma zingine.
Tz unavyumba 100 na wateja 200. Sasa hapo utataka kuleta wateja wengine tena.

Kimsingi tatizo Letu bado lipo kwenye miundo mbinu , Kwa mfano wa TRA, kupata tozo la Kodi Kwa kila mauzo ya reja reja na hata ya jumla iwe kwenye huduma na pia katika biashara za kawaida. Ndio maana mwendo wetu ni wa kusua sua.
Taratibu zetu nyingi bado no goi goi. Sababu ya kupendekeza upigaji Kwanza Mama Tz baadae.
 
1. Kufuta visa kwa Waafrika sidhani kama kuna faida.
Hapa kuna kucheza na 'psychology'. Kenya wanatoza USD 30 kwa e-registering,hiyo ni Visa

Kuna 'fees' zimefichwa. Kwa mfano, ukiongeza cent 50 USD kwa kila abiria local or international kiasi ni kikubwa kuliko fedha za Visa, unacheza na saikolji.

Pili, lazima tuangalie 'usalama' mifumo yetu ya kutambua raia na usalama, iliyopo si ile ya 1961-90.
Kinachotokea DRC ni matokeo ya uhamiaji haramu, kama yanayotokea Dadabu, Kigoma n.k.
2. Kuboresha namna tunavyojitangaza ni wazo zuri.
Tuna tatizo kubwa . Kwanza, siamini katika bureaucracy za serikali iliyoshindwa kuendesha UDART licha ya soko lisilo na mpaka, siamini kuipa tena kazi hiyo. Serikali haiwezi kuendesha chochote!

Sekta binafsi ipewE kazi itafanikiwa. Kazi ya Serikali ni ku-monitor, kudhibiti na kutathmini utendaji wa kampuni.

Pili, tunaangalia matangazo kama sehemu ya Utalii, ni kweli lakini siyo hiyo tu.
Kama Balozi wa US anakwenda Arusha kula nyama choma, kwanini tusifanye Arusha kuwa 'capital' ya nyama choma EA? Je hilo si kujitangaza.

Utalii usiangaliwe kwa jicho la mabango, uangaliwe pia kwa huduma bora , ubunifu n.k.
Hivi kweli tumeshindwa kuandaa Tamasha la nyama pori mara moja kwa mwezi katika majiji yetu!

Tatizo letu 'tumepiga' marufuku ubunifu, ukijenga Bilicana inabomolewa kwa ushenzi tu na upumbavu
3. Tz tuna kasumba ya kumtangaza Raisi wetu kuliko tunavyoitangaza nchi na vivutio vya utalii tulivyonavyo.
Hakuna ubunifu! tuna chawa wengi kuliko 'watu' wenye akili. Bila kumtangaza utaonekanaje?

Mtu hawezi kutunga wimbo unaozungumzia nchi bila '' ni jembe, anaupigia, Babu, baba, mama' n.k

Nchi inatangazwa kwa alama zake si mtu, aghalabu ikitokea mtu kama Nyerere au Salim hiyo haijambo! lakini hao hawatokei kila siku.
 
Tatizo namba moja kwamba tumekariri kutangaza mbuga za wanyama ndio kivutio Cha utalii wakati wanyama Kila nchi inao kwake,wazungu wana hadi ranchi wamewafuga wanashinda nao huko wakicheza nao na hadi Kuna spicies zingine sisi hatuna asa unategemea Mimi nikisha muona simba ntarudi Tena kumwangalia ili iweje?
 
Back
Top Bottom