1. Kufuta visa kwa Waafrika sidhani kama kuna faida.
Hapa kuna kucheza na 'psychology'. Kenya wanatoza USD 30 kwa e-registering,hiyo ni Visa
Kuna 'fees' zimefichwa. Kwa mfano, ukiongeza cent 50 USD kwa kila abiria local or international kiasi ni kikubwa kuliko fedha za Visa, unacheza na saikolji.
Pili, lazima tuangalie 'usalama' mifumo yetu ya kutambua raia na usalama, iliyopo si ile ya 1961-90.
Kinachotokea DRC ni matokeo ya uhamiaji haramu, kama yanayotokea Dadabu, Kigoma n.k.
2. Kuboresha namna tunavyojitangaza ni wazo zuri.
Tuna tatizo kubwa . Kwanza, siamini katika bureaucracy za serikali iliyoshindwa kuendesha UDART licha ya soko lisilo na mpaka, siamini kuipa tena kazi hiyo. Serikali haiwezi kuendesha chochote!
Sekta binafsi ipewE kazi itafanikiwa. Kazi ya Serikali ni ku-monitor, kudhibiti na kutathmini utendaji wa kampuni.
Pili, tunaangalia matangazo kama sehemu ya Utalii, ni kweli lakini siyo hiyo tu.
Kama Balozi wa US anakwenda Arusha kula nyama choma, kwanini tusifanye Arusha kuwa 'capital' ya nyama choma EA? Je hilo si kujitangaza.
Utalii usiangaliwe kwa jicho la mabango, uangaliwe pia kwa huduma bora , ubunifu n.k.
Hivi kweli tumeshindwa kuandaa Tamasha la nyama pori mara moja kwa mwezi katika majiji yetu!
Tatizo letu 'tumepiga' marufuku ubunifu, ukijenga Bilicana inabomolewa kwa ushenzi tu na upumbavu
3. Tz tuna kasumba ya kumtangaza Raisi wetu kuliko tunavyoitangaza nchi na vivutio vya utalii tulivyonavyo.
Hakuna ubunifu! tuna chawa wengi kuliko 'watu' wenye akili. Bila kumtangaza utaonekanaje?
Mtu hawezi kutunga wimbo unaozungumzia nchi bila '' ni jembe, anaupigia, Babu, baba, mama' n.k
Nchi inatangazwa kwa alama zake si mtu, aghalabu ikitokea mtu kama Nyerere au Salim hiyo haijambo! lakini hao hawatokei kila siku.