Angalieni umbo la hiki kiwanja, maana huyu mtu analia

Ndio. Mita 510 sio nyingi, ghorofa itamuachia nafasi kubwa. Tuseme anataka kujenga nyumba yenye sqm 100, anaweza kujenga chini sqm 50 na juu 50. Aidha, itakuwa rahisi zaidi kuijenga kwa awamu.

Amandla...
Ni kweli kabisa
 
Je, Mfukoni/Uwezo unamruhusu? Asije akaishia katikati.
Ataweza tu, muda anao. Watu wanaogopa bure ghorofa. Anaweza kufanya hivi:
1. Nyumbe iwe ya ghorofa mbili.
2.Chini anakuwa na chumba kimoja, stoo, choo na sehemu ya kupaki gari na kuanika nguo.
3.Ghorofa ya kwanza anakuwa na sebule iliyoungana na dining, jiko, choo na chumba cha kulala mgeni.
4. Ghorofa ya pili anakuwa na Master pamoja na vyumba viwili vya watoto.
5 Kwenye paa anakuwa na sehemu ya Sim Tank, sola na bustani.

Anaanza kwa kujenga nguzo na sakafu zote zinazohitajika.
Baada ya hapo anagawa vyumba. Anaweza hata kuhamia ghorofa ya kwanza kabla hajamaliza nyumba yote. Anaweza kujipa hata miaka minne ya kukamilisha ujenzi wake.

Aidha, ghorofa ina usalama zaidi. Na kwa vile nyumba yake itakuwa na sehemu kubwa ya bustani na ya kuchezea watoto itakuwa na thamani zaidi ya hao waliojenga na kujaza uwanja wote.

Amandla...
 
Nani alikuambia (Tafakari) kwamba ulivyo kwa sasa utadumu hivyo-hivyo hadi umalize hizo unazoziita Awamu? Leo ni mzima, kesho afya imetetereka, leo una kidogo kesho umepinda n.k. Liwezekanalo leo lisingoje kesho. Kesho ni majaliwa.
Hapana. Tunasema haraka haraka haina baraka. Unaweza kujenga kitu kwa haraka haraka halafu ukakijutia maisha yako yote. Ajenge kwa spidi yake ile apate kitu ambacho atakipenda maisha yake yote. Kama Mungu atakuwa na mipango yake mingine, hilo halikwepeki.

Amandla...
 
Nani alikuambia (Tafakari) kwamba ulivyo kwa sasa utadumu hivyo-hivyo hadi umalize hizo unazoziita Awamu? Leo ni mzima, kesho afya imetetereka, leo una kidogo kesho umepinda n.k. Liwezekanalo leo lisingoje kesho. Kesho ni majaliwa.
Uko sahihi bora afanye anachoweza yeye alisema uwezo wake kujenga nyumba yenye room 3 master moja na self moja na single moja

Living room,Dining,kitchen & store + public toilet

Napo ni kwa awamu yaan mwaka wa kwanza aanze msingi,mwaka wa pili apandishe ukuta na mwaka wa 3 kupaua
 
Ahsante me naona naomba nikufate pm kwaajili ya wakati ujao
 
Uko sahihi, na Mungu huyo amempatia hicho alichonacho SASA ili akitumie kwa ufanisi wa kiwango cha juu. Mungu angelitaka ampe cha kuingia kwenye ulingo wa kushindana (Ujenzi wa maghorofa) angempa na mchongo wa kuupata uwezo huo. Lakini kama ni hizi za kuwindisha Biashara au Ofisi za Serikali cjui. Namtakia kila la kheri
 
Huo mtiririko wa Awamu Mmh! Mtiririko mzuri ungekuwa 1. Kusafisha kiwanja/eneo, kuweka msingi na kupandisha Ukuta. Mbona kupandisha ukuta ni rahisi na haichukui muda?(Mafundi watakwambia nyumba hapo bado inaongea kiswahili). 2. Kupaua, kuweka miundo-mbinu ya maji na umeme (Mafundi watakuambia hapo nyumba inaongea kingereza) 3. Finishing. (Awamu hii ndo inaitwa pasua kichwa-ni gharama kubwa na huwezi kuikwepa). Ila utamaliza tuu, usianze kuwa na wasiwasi. Bora ulinde Nidhamu ya mali -vitu na pesa ikiwezekana simamia mwenyewe mwanzo mwisho.
 
Kumbe mwanzo msingi ndo huwa mgumu ee ?
 
Kumbe mwanzo msingi ndo huwa mgumu ee ?
Sio. Msingi sio mgumu hadi kupandisha kuta. Ugumu unaanzia kwenye kupaua na kendelea kwani hadi mwisho wa kukamilisha kitu kitakachoitwa ni nyumba.
Ukiishia katikati hiyo itaitwa ni pagale kwani hawezi mtu kuishi. Lakini ukisha paua , mtu anaweza hata kujificha mvua hapo. Hiyo ni nyuma japo haijakamilika. Baada ya kuapaua kuna vikorokoro vingi na vinahitaji hela ndefu tena vinaambatana i.e. huwezi kuvitenganisha. eg. Ukifanya "blundering" lazimamtu wa umeme uwe tayari ushamwandaa. Ukipiga ripu lazima mtu wa skimming uwe ushamwandaa na mtu wa kufunga grills uwe meshamweka sawa. n.k.n.k. ndo mana awamu hiyo inaitwa pasua kichwa.
 
Shukran nimeelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…