Angalizo kwa haters mkiona faya inamwagia maji ndege haijaungua ile ni salute msije humu kukurupuka inawaka moto

Sasa mbona akiwasema mnawatetea tena hao hao waliofanya tufike hapa mkuu?
Look here,buddy!Nilicholenga ni kwamba anajidai ni yeye pekee aliyefanya maendeleo kuliko mtu yoyote wakati si kweli.Maisha ya Watanzania yapo hoi bin taaban halafu yeye ananunua midege.Ujinga.Vitu hufanywa kwa hatua siyo kurukaruka kama ngedere.
 
Jibu ni hili, pesa ambayo ingetaliwa kuwapandishia mshahara wafanyakazi na kuwalipa vyema stahiki zao zimepelekwa kununua midege, marais waliopita walijali zaid watu kuliko vitu
 
Ni bora pesa nyingi zipelekwe kwenye sekta zinazogusa maisha ya watu wengi, mfano maji, barabara, afya, kilimo, mifugo, uvuvi nk. Sasa nilipita ile barabara inayoingia kituo cha mawasiliano na ile inayoenda makongo juu, utafikiri ni mahandaki yako mle mabarabarani. Mnawaingiza wenye magari gharama kubwa za kuendesha magari yao, wakiomba kupandisha nauli kidogo inakuwa shida. sijui kama kuna watu wananielewa hapa???
 
Nimeogopa kusikia kuna katimu ka Mpira ka huko Misri (Pyramids FC) kameingia na ndege yao binafsi huko Mwanza nahisi itakuwa ni ndege ya Serikali ya Misri
Kama ni kweli ushangiliaji wetu ni wa kujichunguza
Kwani ATCL bado haina Ndege wameambiwa hizi ni za Serikali wamekopeshwa tu
wamefanikiwa kukusanya milioni 16 mpaka sasa kati ya ndege 7 na hii ya 8 sijui imenunuliwa cash 600m au 600 Bilioni
jamani ATCL tunzeni Shirika hili maana tumeambiwa hata ikifika miaka 100 ijayo muuwe mbali
 
Naona mitaani CCM na Wanyonge wanatembea kifua mbele wamenunuliwa mandege na JPM!
Vifua mbele vya wapi mkuu?Watu hawana furaha hela hakuna.Maisha magumu.Wakilalamika wanaambiwa walikuwa wapiga dili au wavivu.Na zaidi wanaambiwa wahame nchi utadhani wakati wanaomba uongozi ahadi ilikuwa ni kuwatengenezea Watanzania mazingira magumu ya kuishi kishetani/living hell!
 
Tukifikisha idadi ya ndege sawa na Ethiopia, watu wataota magaga ya kwenda Airport kupokea ndege.

Wakati wa Kambarage, ATC ikifikisha ndege 14. Mwenye picha "toka maktaba" Mwl akipokea ndege japo moja tu, atusaidie.
Acha magaga yatoke tu.IPI bora hela kuwa kwa watu wachache wengi hoi na hakuna vitu au bora hela kuwa chache kwa watu ingawa uhoi bado upo kiasi chake na tunaona maendeleo ya vitu au?

Maendeleo yamegawanyika sehemu 2,watu na vitu.

Maendeleo ya vitu husababisha maendeleo ya watu kwa sababu vitu ni nyenzo wezeshi katika maendeleo ya watu.

Zamani tunalalamika kulikuwa na hela,mbona hapakuwa na maendeleo ya watu na vitu? Hela zilikuwa zinafanya nini?

Inafurahisha ukiwa Indra Gandi Intl.Airport unaona kitu Air Tanzania nalo limetua na kutuna katika Uwanja huo uliopo kwenye top ten ya viwanja busy/vikubwa duniani.

Inafurahisha walahi,mnyonge mnyongeni lakini haki yake apewe.

Nipo hapa Kalabash Mwenge wanywaji Wa henken na Windhoek ni wachache,halafu sisikii lete kama tulivyo.

Heshima sasa hivi kudadadeki inaonyesha taswira yake sio kama zamani.

Halafu kuna kamsururu ka mademu classic wanahama toka mitaa pendwa ya kishua kwenda huko Temeke,Mbagala na uswazi mwingine kwa sababu ile mijamaa ya kuwapangishia, kuhonga vi-ist nk nao wamebwana.

Hakuna mishe town za kiboya kama zile enzi.

Povu ruksa,karibuni na tusipotoshane.

Hahahahaha!!!!

Tusipotoshane,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujio wa Ndege nyingine leo umezidi kumpa kete Rais Magufuli kwenye uchaguzi ujao na zaidi Wananchi kujenga matumaini makubwa kwenye ngwe yake ya pili



Kila kona ya Nchi sasa hivi imekuwa gumzo kwa jinsi Rais Magufuli kwa jinsi anavyorudisha Taifa kwenye mstari


Kama Rais Donald Trump wa Marekani anamkubali Rais Magufuli kwa jinsi anavyofanya mambo makubwa Nchini sie ni nani mpaka tumpinge?


Week ya jana nilikuwa Mtwara,Lindi,Arusha,Kilimanjaro,Dodoma,Morogoro na Tanga huko kote wananchi wanasema Rais Magufuli apewa muda zaidi wa kuendesha Nchi


#JPM KIOO TUELEKEACHO

Alex Fredrick
 
Mbona umeruka aliposema anajua kuna malalamiko ya ndege kuchelewa kuondoka na pia kuondoka zikiwa tupu, huku abiria wanaambiwa zimejaa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…