Angalizo la Picha: Donda lisilopona kwa zaidi ya Miaka 10, Naomba msaada wa Dawa

Habari zenu wana JF.

Ninaomba mwenye kujua dawa ya hili donda. Saivi lina miaka zaidi ya kumi, linakauka na kurudia tena.

Hospitali za kawaida mpaka Muhimbili kwa kulazwa mwezi mzima. Limefika hili donda mpaka India. Limepakwa dawa za kunywa na kupaka, za mitishamba.

Likichomoka lina maumivu makali sana mpaka lipate sindano. Linasababisha kukosa usingizi, kutoka nje, na kutokuwa na hamu ya kula.

Sio mgonjwa wa sukari, wala sio kansa. Ni donda tuu lililokuwa haliponi kwa miaka mingi sana.

View attachment 3295772
Pole sana kwa kuuguza Mgonjwa wa namna hii. Ni changamoto kubwa.

Kama ulivyosema ametibiwa kwa Hospitali za kawaida, Muhimbili na hadi India ameenda.

Naamini Madaktar wamefanya kazi yao uchunguzi na Tiba zote muhimu.

Pia naamini Walishamweleza mgonjwa tatizo lake na changamoto zake.

Akubaliane na hali aendelee na tiba za kawaida kuweza kutunza hali yake ya afya na hali nzuri.

Asidhani kuna tiba zaidi ya hizo vinginevyo atapigwa pesa na matapeli waganga na manabii wa uongo.

Hicho kidonda kinaitwa Arterial Ulcer kinauma sana. Kinachelewa kupona.

Huathiri watu wenye tabia ya kuvuta sigara kwa muda mrefu, hitilafu za kurithi za kibaiolojia.

Wapo wachache wanaweza kuwa na Sukari au kiwango kikubwa cha cholesterol.

Yoote haya tunayaeleza kukuza ufahamu ili msipigwe na pia msikate tamaa.
 
Habari zenu wana JF.

Ninaomba mwenye kujua dawa ya hili donda. Saivi lina miaka zaidi ya kumi, linakauka na kurudia tena.

Hospitali za kawaida mpaka Muhimbili kwa kulazwa mwezi mzima. Limefika hili donda mpaka India. Limepakwa dawa za kunywa na kupaka, za mitishamba.

Likichomoka lina maumivu makali sana mpaka lipate sindano. Linasababisha kukosa usingizi, kutoka nje, na kutokuwa na hamu ya kula.

Sio mgonjwa wa sukari, wala sio kansa. Ni donda tuu lililokuwa haliponi kwa miaka mingi sana.

View attachment 3295772

Ni kidonda ambacho kinaweza kuhusisha mishipa ya damu(Venous vs Arterial Ulcer).

Pamoja na tiba ya kidonda, daktari bingwa wa mishipa ya damu ni muhimu ili kutathimini hali ya eneo zima kulishwa na kuondoa uchafu kwenye eneo husika(afya, ubora na uimara wa mishipa ya damu eneo husika). Pia ushauri wa jinsi ya kutunza eneo husika(ufanye na usifanye nini ili kuwe salama).
 
Habari zenu wana JF.

Ninaomba mwenye kujua dawa ya hili donda. Saivi lina miaka zaidi ya kumi, linakauka na kurudia tena.

Hospitali za kawaida mpaka Muhimbili kwa kulazwa mwezi mzima. Limefika hili donda mpaka India. Limepakwa dawa za kunywa na kupaka, za mitishamba.

Likichomoka lina maumivu makali sana mpaka lipate sindano. Linasababisha kukosa usingizi, kutoka nje, na kutokuwa na hamu ya kula.

Sio mgonjwa wa sukari, wala sio kansa. Ni donda tuu lililokuwa haliponi kwa miaka mingi sana.

View attachment 3295772
DR Mambo Jambo
 
Back
Top Bottom