Angalizo la Picha: Donda lisilopona kwa zaidi ya Miaka 10, Naomba msaada wa Dawa

Angalizo la Picha: Donda lisilopona kwa zaidi ya Miaka 10, Naomba msaada wa Dawa

Habari zenu wana JF.

Ninaomba mwenye kujua dawa ya hili donda. Saivi lina miaka zaidi ya kumi, linakauka na kurudia tena.

Hospitali za kawaida mpaka Muhimbili kwa kulazwa mwezi mzima. Limefika hili donda mpaka India. Limepakwa dawa za kunywa na kupaka, za mitishamba.

Likichomoka lina maumivu makali sana mpaka lipate sindano. Linasababisha kukosa usingizi, kutoka nje, na kutokuwa na hamu ya kula.

Sio mgonjwa wa sukari, wala sio kansa. Ni donda tuu lililokuwa haliponi kwa miaka mingi sana.

View attachment 3295772
Dah,pole sana ndugu yangu,

M/mungu akuponye na iko kidonda aisee . Dah!
 
Shukrani sana!
Nimeona Picha na Maelezo Ya Hiyo Chronic ulcer..
mimi Nina maswali kwa Mgonjwa..

  • Vipi umewahui kufanya biopsy ya kidonda lini imewahi kufanyika? Maana Kabla hatujakupa Dawa ni muhimu kuthibitisha kama siyo Pyoderma gangrenosum, kwenye Hatua Za Mwanzoni au ni Vasculitis ulcer, au aina Nyingine ya Maambukizi Kama umewahi kupima Majibu Yalikuwaje
  • Pia Umewahi kupimwa mzunguko wa damu (arterial/venous Doppler scan)?
  • Kuna homa au usaha wowote unaotoka mara kwa mara?
  • Ulishawahi kupima magonjwa ya autoimmune kama lupus, scleroderma, au vasculitis?
HIyo sehemu ya Kidonda Inauma? Kama haiumi tunaweza kuintroduce magott RX
TUanze na Hayo maswali kwanza
Cc: Proved SeliSelina
NATAKA KUKUTUMIA PRIVATE VETI VYOTE ILA NASHINDWA


BIOPSY ALISHAFANYA SIO MARA MOJA, DOPPLER NAYO IMEFANYIKA PIA.

HAKUNA HOMA, WALA USAHA , NI MAJI TUU HUWA KINATOA

MGUU ULIANZA KUWA MWEUSI, AKAPEWA DAWA, PAKAFANYA KIJIPU, BAADA YA KUPIMWA NDIO AKAAMBIWA ENDE MUHIMBILI KWA MARA YA KWANZA, WAKATI ANAMSUBIRI DAKTARI, NDIO PAKATUMBUKA PAKATOKA MAJI MENGI SANA, AKALAZWA MIEZI MIWILI KWA MARA YA KWANZA, AKATIBIWA AKAPONA, BAADA YA MUDA UKAREJEA UPYA, AKARUDI TENA MUHIMBILI, AKALAZWA TENA, AKATIBIWA AKAPONA, BAADA YA MUDA UKARUDI TENA NDIO AKAENDA INDIA, AKAPATA MATIBABU, AKAPONA, UKAREJEA TENA, HALI NDIO HIYO HIYO YA KUJIREJEA REJEA NDIO ALOKUWA NAYO, NDIO MPAKA AKATUMIA MITI SHAMBA.

SASA HIVI MGUU MWENGINE NDIO UMEANZA ISHARA ZILE ALIZOKUWA NAZO MWANZO KWENYE MGUU WA KWANZA, NDIO NIKAONA NILETE HAPA KWA WATAALAM WA JAMIIFORUM TUPATE KUSAIDIANA. HIVI SASA PIA YUPO MAHANGAIKO, ILA ALISHAPITIA KWA MADAKTARI WENGI, WA KWETU, WA KICHINA NA DAWA ZAO, WA KIHINDI, WA MTISHAMBA, MGUU UNAKWENDA NA KURUDI.

AHSANTENI,

SHUKRANI WA WOTE WA JF
 
NATOA SHUKRAN KWA WANA JF WOTE KWA KUONYESHA USHIRIKIANO WA HALI YA JUU. Nakuombeeni KHERI na baraka.
Ama kwa wale walioonyesha istihzaai. Namuombq Mungu awasamehe na awaobdoshee mabalaaa.
Amiyn
 
NATOA SHUKRAN KWA WANA JF WOTE KWA KUONYESHA USHIRIKIANO WA HALI YA JUU. Nakuombeeni KHERI na baraka.
Ama kwa wale walioonyesha istihzaai. Namuombq Mungu awasamehe na awaobdoshee mabalaaa.
Amiyn
Kwakua umeenda hadi India imeshindikana(means sio kisukari Wala Kansa)...kama itakua Bado ebu njoo nikusaidie mtu wa upande wa pili tuone tunasolve vip
 
Kwa miaka yote hiyo,huenda wangekuwa wamesha kushauri kufanya Amputation! Ndiyo final solution.
 
Kama upo serious kweli njoo pm ipo dawa atapona mtasahau
Mkuu; Tunaomba, ikikupendeza, uweke hapa hadharani kwa manufaa ya wengi. Huko piemuni unakuwa ni uchoyo ilhali ww sio mchoyo kivile.
 
Kwa miaka yote hiyo,huenda wangekuwa wamesha kushauri kufanya Amputation! Ndiyo final solution.
Mkuu; Wataalam madaktari wapo makini sana. Hawaioni sababu yenye mashiko ili kuukata huo mguu. Bado wanapambana sambamba jinsi naye Seli.. anavyojipambania hali inayomsibu. Hakuna kukata tamaa au kutoa majibu rahisi kwa swali gumu. Mwisho ni uhakika watafanikiwa na Seli.. atakuwa vizuri tuu.
 
Na wewe waamini ktk ujinga huo?
Kwani huyo mgonjwa ni mtu mzima(Adult)? Mbona naona ni kama ni Mzazi anayempambania mwanaye ambaye mguu wake huyo mtoto umetatizika kwa kidonda kisichopona? ref. maelezo hapo Na.#86.
 
Kuna dawa ya kienyeji unaweza tumia. Muhimu kuizingatia. Hamna gharama zaidi ya muda wako. Nitumie ujumbe
 
Back
Top Bottom