KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 19,185
- 37,239
Habari za wakati huu ndugu zanguni.
Kama ilivyo ada na kawaida kuhabarishana habari mbali mbali zenye manufaa kwa ajili ya kuepushana na mambo yanayoonekana kutuathiri kwenye jamii na familia hii kwa ujumla wake.
Nimepata bahati mbaya ya kumuuguza mgonjwa hapa nyumbani kwangu mwenye ugonjwa wa muda mrefu anayelazimika kutumia dawa fulani kwa kila wiki.
Hali hiyo ilipelekea kuwa na bajeti ya kiasi cha Elfu 20 kila wiki ili kukidhi mahitaji ya mgonjwa wangu kimatibabu kwa maelekezo ya Daktari wake.
Nilikuwa navichukua kwenye pharmacy za mitaani wakinihakikishia kuwa dawa za namna hiyo ni adimu sana na hivyo ni ghali.
Walikuwa wananiuzia kila kidonge kiasi cha Elfu mbili.
Kuna siku ikatokezea pale wakawa hawana zile dawa, nikaona anamuita kijana wa boda boda ingawa walitaka kufanya siri lakini niliibahatika kunasa maongezi yao na kujua anapomuelekeza kwenda kuchukua.
Nikasikia jina la duka kubwa la pharmacy kubwa hapa Dar es salaam ambapo mimi mwenyewe nalijua lilipo.
Nikafanya maamuzi ya kwenda kununua huko nikamwambia basi siku nyingine nikamuona akawa mbishi kidogo lakini nikakomaa.
Kufika kule( huko kwenye hilo duka kubwa maarufu) nikakuta kule vile vidonge vinauzwa 6,000/= vyote kumi nilishtuka sana kutoka 20,000/= mpaka 6,000/= lakini ndio basi tena ikawa nimeshapigwa, yule binti mpaka leo ananionea haya.
NB: Nawasihi ndugu zanguni kama una uhitaji au matumizi ya dawa fulani wa muda mrefu jitahidi walau uzungukie maduka matano makubwa kujiridhisha maana hawa ndugu zetu wanaouza madawa wamepanga kuwa matajiri kupitia afya zetu na wapendwa wetu tunao wauguza.