DOKEZO Angalizo: Utapeli na wizi kwenye maduka ya Pharmacy/ biashara ya dawa za binadamu

DOKEZO Angalizo: Utapeli na wizi kwenye maduka ya Pharmacy/ biashara ya dawa za binadamu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Uchinga haupo kwenye mitumba tu ndugu zangu hata kwenye dawa,mfano ukiwa kinondoni studio nguo zilizotundikwa kwenye boutique za mtumba unaambiwa 30 ila nguo hiyohiyo ukiikuta karume 2500 unabeba hata famacy nazo kuna sehemu huwa wanachukulia kwa jumla lakini wanakuja kuuza kama duka la dawa,tofauti yao na duka la dawa wao wanaleseni ya kuuza dawa zaidi ya zile mhimu
Mfano wako hauna Uhalisia....kutoka2500 hadi 30000?
 
Kabisa Sasa hivi Kuna upandaji holela wa Dawa
Mfano Kuna Dawa moja Wanaita Erythromycin Nilikuwa nikinunua 10 kwa Tsh 1000
Ajabu Ndani ya muda mfupi Imekuwa 2000
Sasa Inapandaje Ghafla kwa ×2
Sijui nchi hii tunakwemda wapi
Ndugu.....

Jitahidi sana kama una uhitaji wa dawa kwa muda ( Mungu aepushie mbali) utembelee maduka makubwa makubwa tofauti na haya ya mtaani......kidogo Yana unafuu....
 
Ndugu
Tumeshaangamia kwani wapo wengi wanaojifia kwa kukatishwa tamaa na bei za kubumba Hali ya kuwa ni bei za kitapeli
Mimi kaka yangu alikufa 2001 kwa kukosekana buku 5 ya sindano ya pumu. Zahanati ya mtaani kabisa ambapo tunajulikana ila mtu na roho yake mbaya alishindwa kufanya tendo la kibinadamu na kupelekea mapafu kubana hatimaye kukata moto. Ni story ambayo haiwez futika akilini mwangu.
 
Mimi pia niliwahi kuuziwa kidonge kimoja elfu 2, ilikuwa dose ya mwezi mmoja. Nikasema ngoja nowe nachukua vya wiki wiki. Baade nikapata wazo la kuwasiliana na mdogo wangu yuko kwenye field hii ya afya. Akanielekeza sehem ambapo nilipata vile vidonge kwa 350 kwa kila kimoja.
Ni kawaida hiyo mkuu mbona. Wale ni machinga hivyo bei watakupga mara kadhaa. Hii ni kwa biashara zote si duka la dawa tu.
Hata bia kuna sehemu inauzwa buku 2 sehemu nyingine utanunua buku 7
 
Habari za wakati huu ndugu zanguni.........

Kama ilivyo ada na kawaida kuhabarishana habari mbali mbali zenye manufaa kwa ajili ya kuepushana na mambo yanayoonekana kutuathiri kwenye jamii na familia hii kwa ujumla wake.......

Nimepata bahati mbaya ya kumuuguza mgonjwa hapa nyumbani kwangu mwenye ugonjwa wa muda mrefu anayelazimika kutumia dawa fulani kwa kila wiki......

Hali hiyo ilipelekea kuwa na bajeti ya kiasi cha Elfu 20 kila wiki ili kukidhi mahitaji ya mgonjwa wangu kimatibabu kwa maelekezo ya Daktari wake.........

Nilikuwa navichukua kwenye pharmacy za mitaani wakinihakikishia kuwa dawa za namna hiyo ni adimu sana na hivyo ni ghali......

Walikuwa wananiuzia kila kidonge kiasi cha Elfu mbili.......

Kuna siku ikatokezea pale wakawa hawana zile dawa....nikaona anamuita kijana wa boda boda ingawa walitaka kufanya siri lakini niliibahatika kunasa maongezi yao na kujua anapomuelekeza kwenda kuchukua........

Nikasikia jina la duka kubwa la pharmacy kubwa hapa Dar es salaam.....ambapo mimi mwenyewe nalijua lilipo......

Nikafanya maamuzi ya kwenda kununua huko nikamwambia basi siku nyingine.....nikamuona akawa mbishi kidogo lakini nikakomaa......

Kufika kule( huko kwenye hilo duka kubwa maarufu)....nikakuta kule vile vidonge vinauzwa 6,000/= vyote kumi....nilishtuka sana....kutoka 20,000/= mpaka 6,000/= lakinj ndio basi tena ikawa nimeshapigwa.....yule binti mpaka leo ananionea haya......

NB;
Nawasihi ndugu zanguni kama una uhitaji au matumizi ya dawa fulani wa muda mrefu jitahidi walau uzungukie maduka matano makubwa kujiridhisha maana hawa ndugu zetu wanaouza madawa wamepanga kuwa matajiri kupitia afya zetu na wapendwa wetu tunao wauguza.......
Ni kweli kabisa, inashangaza sana sikuhizi Wauza madawa mpaka wanajitangaza sana kupitia WhatsApp, Tiktok, Instagram na kwingineko kama wauza nguo na bidhaa zingine
 
Mimi kaka yangu alikufa 2001 kwa kukosekana buku 5 ya sindano ya pumu. Zahanati ya mtaani kabisa ambapo tunajulikana ila mtu na roho yake mbaya alishindwa kufanya tendo la kibinadamu na kupelekea mapafu kubana hatimaye kukata moto. Ni story ambayo haiwez futika akilini mwangu.
Pole sana ndugu yangu......

Kaka yako ni miongoni mwa wahanga wanaoangukia kwenye mikono ya hawa mashetani walioweka fedha mbele na kuwacha ubinadamu nyuma.....
 
Back
Top Bottom