DOKEZO Angalizo: Utapeli na wizi kwenye maduka ya Pharmacy/ biashara ya dawa za binadamu

DOKEZO Angalizo: Utapeli na wizi kwenye maduka ya Pharmacy/ biashara ya dawa za binadamu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
H
Usiwasahau na hawa wenye butcheries, hizi mizani digital wanaibia sana wateja. Mfano nyama kilo ni 10,000 yeye kwenye mzani anaandika 12,000 so utaambulia nyama pungufu maana mzani ukifika kwa 10,000 anakupa nyama yako. Muweni makini.
Huo mzani hauonyesh Kg Gm?
 
Hio ipo kwenye biashara zote. Hawa wauzaji hawafikirii mbali. Angesema 8,000 wala usingejali ungeona 2,000 yake ya usumbufu ila wana tamaa sana. Matokeo yake anapoteza mteja.
Biashara ya Dawa iko hivyo.
Dawa ya jumla na rejareja ni tofauti kubwa kabisa.

Mf. ukinunua vile vipima mimba kwa jumla unauziwa Tsh. 150/= ukinunua rejareja ni Tsh. 1,000/=
 
Haya mambo yapo dunia nzima kiongozi ndio biashara ilivyo hapa kununua ozempic ni $2000 lkn UK na Germany same drug ni $200 hadi $300
Huwezi kueleweka mpaka pale utakapo eleza hiyo dawa ya izempic inao uzwa 5m za kitamzania UK dawa ile ile iuzwe 500k nchi jirani.......thats over exagulation mkuu.
 
Haya mambo yapo dunia nzima kiongozi ndio biashara ilivyo hapa kununua ozempic ni $2000 lkn UK na Germany same drug ni $200 hadi $300
Hawa wanaoshangaa hapa wajichanganye waende Dubai sijui kutembea umeandaa bajeti ya nauli go & return 1.5M na malazi kule lets say 1M vichochoroni umepanga ukae siku 6. Fika uko uumwe malaria tu uone moto wake.

Au jichanganye pewa mwaliko Marekani si unakuwa mtumishi kanisani kwenu, fika uko usikate Visitor Health Insurance alafu umwa ndio utajua dunia duara.

Watu wanaenda nje na mlundikano wa madawa just in case. Malaria, painkillers, minyoo, mafua na kikohozi. Ukijifanya kwenda uko utalipia dawa zao bill inakuja kuja kuliko bajeti nzima ya kukaa uko.
 
Usiwasahau na hawa wenye butcheries, hizi mizani digital wanaibia sana wateja. Mfano nyama kilo ni 10,000 yeye kwenye mzani anaandika 12,000 so utaambulia nyama pungufu maana mzani ukifika kwa 10,000 anakupa nyama yako. Muweni makini.
Mizani niliyoiona ina display 3, bei kwa kilo, kilo zilizopo na gharama yake. Hapa unapigwaje?
 
Kwa hiyo hizo ndio bei elekezi kutoka Baraza la wafamasia....???
Mzee hili ni somo Pana Sana la dawa za binadamu Kuna brand nyingi sanaa.

Mfano.
Amoxclave 625mg tabs hili ni generic name
Ukiingia kwenye brand Sasa Kuna AUGMENTIN 625 TABS hii ni product ya GSK nenda kaulizie Bei Sasa whole sale @ 42,500
Wakati dawa hiyo hiyo brand za India Kama alphaclave 625,indiclave 625,spotclave 625, gamok 625, cledomox 625, clavam 625, curam 625 hizi zote Zina wastani wa wholesale @4500 nenda huko retail utanunua si Chini ya 10,000

Inawezekana dawa hiyo hiyo umenunua @ cheap brand @6000 na hiyo hiyo dawa ukanunua kwa Bei @ 20,000 juu mfano dawa za brand ya cyplus,gsk,astrazeneca, n.k

The same kama kwenye maji ya kunywa uhai,Dasani, Kilimanjaro n.k
 
Huwezi kueleweka mpaka pale utakapo eleza hiyo dawa ya izempic inao uzwa 5m za kitamzania UK dawa ile ile iuzwe 500k nchi jirani.......thats over exagulation mkuu.

Japo sijaelewa exagualation ni kitu gani ila dunia ya sasa ipo kwenye fingertips kama una akili sawasawa ingia tu Google bila kudhalilisha mtu ujiridhishe, that simple! Nimeongelea biashara in general, ni sawa na kununua jezi ya simba kwa vunja bei kwa laki wkt China haizidi sh 3000 ni maamuzi tu, dunia ina kila aina ya choice kiongozi
 
Habari za wakati huu ndugu zanguni.

Kama ilivyo ada na kawaida kuhabarishana habari mbali mbali zenye manufaa kwa ajili ya kuepushana na mambo yanayoonekana kutuathiri kwenye jamii na familia hii kwa ujumla wake.

Nimepata bahati mbaya ya kumuuguza mgonjwa hapa nyumbani kwangu mwenye ugonjwa wa muda mrefu anayelazimika kutumia dawa fulani kwa kila wiki.

Hali hiyo ilipelekea kuwa na bajeti ya kiasi cha Elfu 20 kila wiki ili kukidhi mahitaji ya mgonjwa wangu kimatibabu kwa maelekezo ya Daktari wake.

Nilikuwa navichukua kwenye pharmacy za mitaani wakinihakikishia kuwa dawa za namna hiyo ni adimu sana na hivyo ni ghali.

Walikuwa wananiuzia kila kidonge kiasi cha Elfu mbili.

Kuna siku ikatokezea pale wakawa hawana zile dawa....nikaona anamuita kijana wa boda boda ingawa walitaka kufanya siri lakini niliibahatika kunasa maongezi yao na kujua anapomuelekeza kwenda kuchukua.

Nikasikia jina la duka kubwa la pharmacy kubwa hapa Dar es salaam ambapo mimi mwenyewe nalijua lilipo.

Nikafanya maamuzi ya kwenda kununua huko nikamwambia basi siku nyingine nikamuona akawa mbishi kidogo lakini nikakomaa.

Kufika kule( huko kwenye hilo duka kubwa maarufu) nikakuta kule vile vidonge vinauzwa 6,000/= vyote kumi nilishtuka sana kutoka 20,000/= mpaka 6,000/= lakinj ndio basi tena ikawa nimeshapigwa, yule binti mpaka leo ananionea haya.

NB;
Nawasihi ndugu zanguni kama una uhitaji au matumizi ya dawa fulani wa muda mrefu jitahidi walau uzungukie maduka matano makubwa kujiridhisha maana hawa ndugu zetu wanaouza madawa wamepanga kuwa matajiri kupitia afya zetu na wapendwa wetu tunao wauguza.

Bado mgeni mjini wewe, chochote kile ukitaka kununua ambacho hujui bei yake, fanya utafiti mdogo sana wa kuulizia bei ujue bei yake halisi, iwe spares za magari, vifaa vya ujenzi, viwanja, kodi za nyumba, bei za hoteli, ukumbi, bei za nguo, gharama za mafundi ujenzi etc..

Sasa dawa tu ww umenunua hata kujua bei yake hujui, ndio maana umepigwa , sasa jifunze kujua thamani halisi ya kitu chochote kabla ya kununua
 
Japo sijaelewa exagualation ni kitu gani ila dunia ya sasa ipo kwenye fingertips kama una akili sawasawa ingia tu Google bila kudhalilisha mtu ujiridhishe, that simple! Nimeongelea biashara in general, ni sawa na kununua jezi ya simba kwa vunja bei kwa laki wkt China haizidi sh 3000 ni maamuzi tu, dunia ina kila aina ya choice kiongozi
Mkuu umeanza kuchanganya mambo jikite kwenye mada ya famasi na bei za dawa sio biashara zingine.
 
Bado mgeni mjini wewe, chochote kile ukitaka kununua ambacho hujui bei yake, fanya utafiti mdogo sana wa kuulizia bei ujue bei yake halisi, iwe spares za magari, vifaa vya ujenzi, viwanja, kodi za nyumba, bei za hoteli, ukumbi, bei za nguo, gharama za mafundi ujenzi etc..

Sasa dawa tu ww umenunua hata kujua bei yake hujui, ndio maana umepigwa , sasa jifunze kujua thamani halisi ya kitu chochote kabla ya kununua
Hii haihusiani na ugeni wa jiji.......
 
Ni kweli last two week nilikuwa zahanati X Kuna kazi nilienda kufanya wakati naongea na nurse wa pale akapigiwa simu kwamba Kuna msiba hivyo wanataka dawa ya sindano ya kumuhifadhi marehemu akawaambia pale dispensary hamna lakin atawaulizia kwenye kituo Cha afya Cha jirani, aliambia dawa IPO gharama ni sh 70,000 yeye alichofanya akamwita yule mfiwa akamwambia dawa IPO lakini bei ni 120,000 na hapo nimekuombea jamaa akajiliza wakafikia 100,000
Lakin baadae kwny maongezi yule nurse alijiskia vibaya baada ya kugundua hao watu walitoka kufiwa wiki ya NYUMA yake lakin akasema hana jinsia😁
Kwhy upigaji upo sana hata misibani
Sometimes kuchukua 30% profit sio upigaji.
Mtu kama umefiwa sio ndio utafute huruma za bidhaa za kufiwa wakati ile ni biashara.

Na biashara yoyote inaendeshwa na risk, jana kuna jamaa kaja nimpe bidhaa ndogo at a very good discount ya 5,000 nikaiharibu bahati mbaya mara mbili na nikaishiwa. Kwa majirani wanauza 10,000 ile bidhaa na mimi nilichukua China. Kufika hatua ile nikamwambia nimeziharibu nenda nitakuwa nazo kesho, kaenda nikajaribu kutafuta bei ya jumla ni 5,000 ileile nayouza rejareja.

Sasa nimeharibu twice, then nichukue kwa jumla nimuuzie bei ileile ya jumla nisipate faida ila bado niingie risk ya kuiharibu tena. Yanini yote hayo nikamwambia nimeshindwa ofa yake.

Sasa mteja kama hutaki muuzaji aingize faida basi usimuingize kwenye risk.
 
Ni kweli last two week nilikuwa zahanati X Kuna kazi nilienda kufanya wakati naongea na nurse wa pale akapigiwa simu kwamba Kuna msiba hivyo wanataka dawa ya sindano ya kumuhifadhi marehemu akawaambia pale dispensary hamna lakin atawaulizia kwenye kituo Cha afya Cha jirani, aliambia dawa IPO gharama ni sh 70,000 yeye alichofanya akamwita yule mfiwa akamwambia dawa IPO lakini bei ni 120,000 na hapo nimekuombea jamaa akajiliza wakafikia 100,000
Lakin baadae kwny maongezi yule nurse alijiskia vibaya baada ya kugundua hao watu walitoka kufiwa wiki ya NYUMA yake lakin akasema hana jinsia😁
Kwhy upigaji upo sana hata misibani

Tusisahau msiba wako ni biashara kwa wengine ndio maisha
 
JUzi tuu nimetoka kuuziwa dawa ya minyoo kwa bei mara 3 ya bei ya kawaida. Mimi nilitaka kununua dozi 3 nashangaa napewa moja na chenji kidogo kuuliza ananiambia ndio bei yake. Basi nikaondoka kwakuwa ni mama mtu mzima nikavunga kwa heshima.
Kwenda Pharmacy nikanunua dozi 2 zilizobaki kwa bei ya kawaida so maduka ya mtaani haya wanaongeza mno bei.
 
Sio sawa tu. Huwezi enda Duka moja ukaafiki bei ya chochote, Hata condom, lazima upiganishe bei!
Kuhusu kondom Kuna cheap brands na expensive brand.

Contempo ni gharama mfn. Rough rider,Wet &wild, kingsize, erotica n.k

Kondom za bei chee kiss kiss, bull, dume, fiesta, life guard n.k
 
Back
Top Bottom