T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 12,362
- 41,886
Wanafikiria mbali vizuri tu, na hawapotezi wateja wala. Nina rafiki yangu graduate wa pharmacy kanitangulia kuhitimu kama miaka miwili. Ana pharamacy na net income yake kwa mwaka ni zaidi ya 50 million na wala sina dalili za kuambulia kumkaribia kwenye biashara yangu ninayofanya kwa kuongeza hizo 2,000 kwenye 6,000. Wakati kahitimu akimiliki bodaboda tu sasahivi anajenga na ana maduka ya madawa mawili na biashara nyingine ndogo aliyoanza nayo.Hio ipo kwenye biashara zote. Hawa wauzaji hawafikirii mbali. Angesema 8,000 wala usingejali ungeona 2,000 yake ya usumbufu ila wana tamaa sana. Matokeo yake anapoteza mteja.
Kupoteza mteja mmoja aliyegundua duka la jumla haimaanishi ndio biashara imekufa. Kwanza hata huyo OP aliyenunua dawa kwa 6,000 sio sawa na anayenunua dawa nyingi au dawa aina tofauti mara nyingi. Hiyo 6,000 bado sio bei yake halisi. Huwa nanunua vipimo vya HIV kwa msambazaji wa vifaa tiba 15,000 vipo 20 wakati vile ukienda polyclinic kupima ni 5,000 hivyo vipimo 20 wanapata 50,000.
Jambo la kuepuka ni kununua dawa ya bei nafuu kwa bei ghali, unaenda hospitali private unapima unaambiwa utachomwa sindano 5 na kila sindano 20,000. Wanakuandikia jina la sindano ya bei ghali ile, ila wanakuchoma sindano nyingine sawa na ile ila ya bei nafuu kama 8,000 hivi.