mbuyake
JF-Expert Member
- Feb 20, 2013
- 293
- 510
Mimi nina mfano halisi sababu chaka langu la tonge la kila siku napatia kwenye afya za watu,kuna hizi dawa kama antibiotics ambazo sio common mtaani bei ya hasa amoxclav huwa tuchukua 4000 ila tunaipiga 12 maeneo yetu japo na mimi kuna sehem nilibamizwa kuna changamoto ya afya ilinikumba ni dawa ya kutuma muda mrefu kidogo nilitumia kidonge kimoja kila siku karibia miaka mitatu sasa nilikuwa mkoa wa katavi kidonge ilikuwa 150 sasa nikasafiri kwenda musoma huko nikiamini bei ni moja nitachukuwa huko basi kufika musoma mjini kabla ya kwenda kijijini nakuoelekea basi kupitia famacy moja nauliza wanauza mia sita kidonge kimoja na wanatoa kwa kibali cha dakitar na wanaangalia kaandika za miezi mingapi nikiangalia nimeambiwa nimeze kwa miezi mitatu kabla ya kurudi kwa tabibu kupiga hesabu ni 54000 du nilikacha na nikasema japo dawa ina withdral side effects nyingi nitakaza hadi nirudi mpanda kule pa 150 na vidonge kumi wanakupa kwa hiyo huku nako ni jipu,tangu kikwete airuhusu afya kuwa biashara huria basi ni kujipigia tu,ila wakuu sijui hii hela ni ya laaana maana ningumu kumwona jamaa kwenye afya kuwa na ukwasi wa kutisha labda wale wenye hospital zenye majina