DOKEZO Angalizo: Utapeli na wizi kwenye maduka ya Pharmacy/ biashara ya dawa za binadamu

DOKEZO Angalizo: Utapeli na wizi kwenye maduka ya Pharmacy/ biashara ya dawa za binadamu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Habari za wakati huu ndugu zanguni.

Kama ilivyo ada na kawaida kuhabarishana habari mbali mbali zenye manufaa kwa ajili ya kuepushana na mambo yanayoonekana kutuathiri kwenye jamii na familia hii kwa ujumla wake.

Nimepata bahati mbaya ya kumuuguza mgonjwa hapa nyumbani kwangu mwenye ugonjwa wa muda mrefu anayelazimika kutumia dawa fulani kwa kila wiki.

Hali hiyo ilipelekea kuwa na bajeti ya kiasi cha Elfu 20 kila wiki ili kukidhi mahitaji ya mgonjwa wangu kimatibabu kwa maelekezo ya Daktari wake.

Nilikuwa navichukua kwenye pharmacy za mitaani wakinihakikishia kuwa dawa za namna hiyo ni adimu sana na hivyo ni ghali.

Walikuwa wananiuzia kila kidonge kiasi cha Elfu mbili.

Kuna siku ikatokezea pale wakawa hawana zile dawa, nikaona anamuita kijana wa boda boda ingawa walitaka kufanya siri lakini niliibahatika kunasa maongezi yao na kujua anapomuelekeza kwenda kuchukua.

Nikasikia jina la duka kubwa la pharmacy kubwa hapa Dar es salaam ambapo mimi mwenyewe nalijua lilipo.

Nikafanya maamuzi ya kwenda kununua huko nikamwambia basi siku nyingine nikamuona akawa mbishi kidogo lakini nikakomaa.

Kufika kule( huko kwenye hilo duka kubwa maarufu) nikakuta kule vile vidonge vinauzwa 6,000/= vyote kumi nilishtuka sana kutoka 20,000/= mpaka 6,000/= lakini ndio basi tena ikawa nimeshapigwa, yule binti mpaka leo ananionea haya.

NB: Nawasihi ndugu zanguni kama una uhitaji au matumizi ya dawa fulani wa muda mrefu jitahidi walau uzungukie maduka matano makubwa kujiridhisha maana hawa ndugu zetu wanaouza madawa wamepanga kuwa matajiri kupitia afya zetu na wapendwa wetu tunao wauguza.
Asante sana kwa keshea nasi taarifa muhimu kama hii,

Juzi kati tu hapo nilimskia wifi yangu anamwambia mdogo wake 'zile dawa tunazomnunulia mama za miguu kwa shlng elfu 6 kuna mdada anawauzia watu kwa elfu 70 ati anawaambia zinatoka nje' Yaani mdada anafanya kuchkua pesa na kujifanya anaagizia nje kumbe anaenda kwenye pharmacy kununua kwa elfu 6 then yeye anauza elfu 70.
Yaelekea tushapigwa sana sana
 
Pole kwa hiyo kadhia mkuu, ila kwa upande wangu nina mtazamo tofauti na wewe/wengi.

Kwa upande wangu huo siwezi kuuita ni utapeli. Kwenye biashara ya mtu huwezi kumpangia apate faida kiasi gani maana hujui gharama za uendeshaji au mzunguko wa hiyo biashara yake. Miaka kadhaa iliyopita kuna mpiga debe alinikatishia tiketi ya kutoka Mbeya kwenda Mafinga kwa 15,000/=, ila nikiwa ndani ya bus akaja konda na kuanza kutoa tiketi rasmi, nilivyompa tiketi yangu, akaipokea na kunipa nyingine ambayo ilionesha nauli ni 10,000/=. Hayo yote wakati yanatokea, yule mpiga debe namuona yupo nje kwa dirishani. Sikumaindi sana as long as niliridhia wakati nampa ile hela, so nikaasssume nimemuungia hela ya kula.

Kipindi wewe unasema faida aliyokuwa anajitengenezea ni kubwa, kumbuka kuna dawa zingine mpaka zinaexpire hazijawahi kununuliwa. So take it easy and move on broh.
Acha mambo ya kuaassume sema ulipigwa kitendo tu cha kuchungulia na kuangalia aliyekukatia tiketi yuko wapi basi ni lazima ulijisikia vibaya
 
Habari za wakati huu ndugu zanguni.

Kama ilivyo ada na kawaida kuhabarishana habari mbali mbali zenye manufaa kwa ajili ya kuepushana na mambo yanayoonekana kutuathiri kwenye jamii na familia hii kwa ujumla wake.

Nimepata bahati mbaya ya kumuuguza mgonjwa hapa nyumbani kwangu mwenye ugonjwa wa muda mrefu anayelazimika kutumia dawa fulani kwa kila wiki.

Hali hiyo ilipelekea kuwa na bajeti ya kiasi cha Elfu 20 kila wiki ili kukidhi mahitaji ya mgonjwa wangu kimatibabu kwa maelekezo ya Daktari wake.

Nilikuwa navichukua kwenye pharmacy za mitaani wakinihakikishia kuwa dawa za namna hiyo ni adimu sana na hivyo ni ghali.

Walikuwa wananiuzia kila kidonge kiasi cha Elfu mbili.

Kuna siku ikatokezea pale wakawa hawana zile dawa, nikaona anamuita kijana wa boda boda ingawa walitaka kufanya siri lakini niliibahatika kunasa maongezi yao na kujua anapomuelekeza kwenda kuchukua.

Nikasikia jina la duka kubwa la pharmacy kubwa hapa Dar es salaam ambapo mimi mwenyewe nalijua lilipo.

Nikafanya maamuzi ya kwenda kununua huko nikamwambia basi siku nyingine nikamuona akawa mbishi kidogo lakini nikakomaa.

Kufika kule( huko kwenye hilo duka kubwa maarufu) nikakuta kule vile vidonge vinauzwa 6,000/= vyote kumi nilishtuka sana kutoka 20,000/= mpaka 6,000/= lakini ndio basi tena ikawa nimeshapigwa, yule binti mpaka leo ananionea haya.

NB: Nawasihi ndugu zanguni kama una uhitaji au matumizi ya dawa fulani wa muda mrefu jitahidi walau uzungukie maduka matano makubwa kujiridhisha maana hawa ndugu zetu wanaouza madawa wamepanga kuwa matajiri kupitia afya zetu na wapendwa wetu tunao wauguza.
Kaka wewe ni M-pare, dawa huwa hazina burgaining!
 
Ni kawaida hiyo mkuu mbona. Wale ni machinga hivyo bei watakupga mara kadhaa. Hii ni kwa biashara zote si duka la dawa tu.
Hata bia kuna sehemu inauzwa buku 2 sehemu nyingine utanunua buku 7
Alaf ipo viceversa ,upande wabia ukikuta sehemu kali sana ndo bei imechangamka tofauti navigrosari vyamtaani,lkn huku kwene dawa maduka makubwa ndo bei chini,njoo ukutane nasisi sasa tuliopanga box zetu mbili tatu kwene shelf
 
Huyu ana duka la jumla Kariakoo lazima awe na bei nzuri.
Saf sana, kumbe mwamba yupo vzr nikajua anatamba Mbeya tu kumbe hadi Town huko,huku pia ukifika kwene pharmacy zake kuna sehemu maalum zakufanyia packagin yadawa zinazoenda sehemu mbali mbali kuna hadi boda special kwa ajili yakufanya delivery
 
Asante sana kwa keshea nasi taarifa muhimu kama hii,

Juzi kati tu hapo nilimskia wifi yangu anamwambia mdogo wake 'zile dawa tunazomnunulia mama za miguu kwa shlng elfu 6 kuna mdada anawauzia watu kwa elfu 70 ati anawaambia zinatoka nje' Yaani mdada anafanya kuchkua pesa na kujifanya anaagizia nje kumbe anaenda kwenye pharmacy kununua kwa elfu 6 then yeye anauza elfu 70.
Yaelekea tushapigwa sana sana
Watu wamekuwa mashetani kabisa
 
Kuna pharmacy nilienda Sina hamu, nilinunulishwa dawa Aina 2 tofauti zote zinafanya kazi moja, nilivyotumia nikaanza kuzidiwa, nilipomuona doctor akaniambia nilipaswa kunywa Aina moja tu na sio zote kwa pamoja.
Pole sana........watu wapo radhi hata kukuudhia dawa zilizoisha muda wake ili kushibisha matumbo yao.....
 
Watanganyika tunazidiwa Sana na wazanzibar kwenye dhulma.
Mpemba sio rahisi kumdhulumu MTU.
Sasa njoo huku Nyamagana, Ushirombo, Rombo (huku hata pombe chafu utauziwa kwa Bei mbaya)
Mombo hapa hata nyama ya mbwa utachanganyiwa kwenye nyama choma ya mbuzi hasa usiku wakati wa kusafirisha maiti)
 
Na kuna baadhi ya vituo vya afya ukienda unabambikiwa magonjwa ili ununue dawa nyingi wapate faida. Nilishapewa dawa za vidonda vya tumbo wakati sina yaani watu wanawaza hela tu hayo mengine hayawahusu.
 
Back
Top Bottom