DOKEZO Angalizo: Utapeli na wizi kwenye maduka ya Pharmacy/ biashara ya dawa za binadamu

DOKEZO Angalizo: Utapeli na wizi kwenye maduka ya Pharmacy/ biashara ya dawa za binadamu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Zingatia ujumbe mkuu.....mengine niachie mwenyewe
baki nayo yote mwenyewe...

ki story hakina detail, haki make sense, tukibebe cha nini ?

Dawa ya 2,000/= umeuziwa 6,000/=

dawa gani ?
umeuziwa wapi ?
kwa nini hukirudi kwa 2000 ?
ulilazimishwa kuuziwa ya 6000 ?
 
baki nayo yote mwenyewe...

ki story hakina detail, haki make sense, tukibebe cha nini ?

Dawa ya 2,000/= umeuziwa 6,000/=

dawa gani ?
umeuziwa wapi ?
kwa nini hukirudi kwa 2000 ?
ulilazimishwa kuuziwa ya 6000 ?
Sawa ndugu mfamasia...... niwie radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwenye biashara yako......
 
Saf sana, kumbe mwamba yupo vzr nikajua anatamba Mbeya tu kumbe hadi Town huko,huku pia ukifika kwene pharmacy zake kuna sehemu maalum zakufanyia packagin yadawa zinazoenda sehemu mbali mbali kuna hadi boda special kwa ajili yakufanya delivery
Yuko vizuri sana.
 
😅😅 Ku exaggerate Jambo mfano wewe ni observer wa Jambo / tukio Fulani
Mfano umeenda chooni ukakutana na nzi wakubwa wakubwa
Akatokea mtu akakuuliza wewe ukasema umeona NZI WAKUBWA KAMA TEMBO CHOONI
Huko ndipo ku exaggerate Jambo 😅😀😂

Kumbe alimaanisha exaggeration kama ni hiyo naijua, nilihisi neno jipya kbs
 
Mbona watanzania wanapigwa tu left right up and down? Nenda makumbusho utapigwa kwenye simu, Kariakoo kila bidhaa, Bagamoyo ardhi, madalali nao wanapiga tu deile, ndio mfumo wa maisha ya nusu ubepari na nusu uchumi wa soko tatizo wa kwetu hauna standards na consumer protection tu kuhakikisha ukinunua basi hata kama umepigwa kisiwe feki tu! Kwetu unaopigwa na unakuta ni fekero pia halafu hauna wa kukutetea. Nchi za wenzetu wanazo hizo mechanisms
 
Sasa ukienda agha khan si uyakuja unalia hapa,kumuona daktari 50,000 wakati vichochoroni 15000 mpaka 20,000
Biashara zina codes nyingi usione watu wanatajirika
Aga Khan kumuona daktar mbona nlikua nalipa 61 mwaka 2022? Au wameshusha Bei?
 
Sioni utapeli wowote hapo,

Uyo dada Kaamua WINGA Kama ilivyo K'koo,karume n.k

Mbona k'koo mnanyooshwa Sana maduka ya USONI Ila hamlalamiki mnatapeliwa?
 
Kwani wewe hujui Daslade Kila kitu Kiko Exaggerated and total manipulated? Kama tu mfano gharama ya kitu kama Cake ambayo mikoani inauzwa 20K Dar wanauza 50k ukiuliza kwa nini wanadai Decor Pumbavu Kwani watu wanaenda kula hayo Marangi rangi ya Urembo na Ukiharisha infact Dar Kila kitu Kiko
Nilishangaa bei ya keki 15k mkoani kwa dar ni 60k,,
 
Mm Kuna kipindi tulikuwa tunauguza mgonjwa Kuna sindano ilikuwa inahitajika ili tumcome alale,Tumeenda tunapochukuaga kila siku wakasema zimeisha tunanunuga chini ya elfu 10,tukaenda pharmacy karibu na duka la hospitali ya mkoa wao wanauza laki sindano Ile Ile ..Yaani unabaki unaduwaaa yaani kutoka elfu 10 mpaka laki aah parefu mno
 
Habari za wakati huu ndugu zanguni.

Kama ilivyo ada na kawaida kuhabarishana habari mbali mbali zenye manufaa kwa ajili ya kuepushana na mambo yanayoonekana kutuathiri kwenye jamii na familia hii kwa ujumla wake.

Nimepata bahati mbaya ya kumuuguza mgonjwa hapa nyumbani kwangu mwenye ugonjwa wa muda mrefu anayelazimika kutumia dawa fulani kwa kila wiki.

Hali hiyo ilipelekea kuwa na bajeti ya kiasi cha Elfu 20 kila wiki ili kukidhi mahitaji ya mgonjwa wangu kimatibabu kwa maelekezo ya Daktari wake.

Nilikuwa navichukua kwenye pharmacy za mitaani wakinihakikishia kuwa dawa za namna hiyo ni adimu sana na hivyo ni ghali.

Walikuwa wananiuzia kila kidonge kiasi cha Elfu mbili.

Kuna siku ikatokezea pale wakawa hawana zile dawa, nikaona anamuita kijana wa boda boda ingawa walitaka kufanya siri lakini niliibahatika kunasa maongezi yao na kujua anapomuelekeza kwenda kuchukua.

Nikasikia jina la duka kubwa la pharmacy kubwa hapa Dar es salaam ambapo mimi mwenyewe nalijua lilipo.

Nikafanya maamuzi ya kwenda kununua huko nikamwambia basi siku nyingine nikamuona akawa mbishi kidogo lakini nikakomaa.

Kufika kule( huko kwenye hilo duka kubwa maarufu) nikakuta kule vile vidonge vinauzwa 6,000/= vyote kumi nilishtuka sana kutoka 20,000/= mpaka 6,000/= lakini ndio basi tena ikawa nimeshapigwa, yule binti mpaka leo ananionea haya.

NB: Nawasihi ndugu zanguni kama una uhitaji au matumizi ya dawa fulani wa muda mrefu jitahidi walau uzungukie maduka matano makubwa kujiridhisha maana hawa ndugu zetu wanaouza madawa wamepanga kuwa matajiri kupitia afya zetu na wapendwa wetu tunao wauguza.
Pole kwa kuchelewa kujua ila hiyo ni kawaida hata hospital ni hivyo hivyo watu wanapigwa kama kawaida
 
Back
Top Bottom