Angela Kairuki amuwakilisha Dkt. Mpango kwenye mkutano wa TAWIRI

Angela Kairuki amuwakilisha Dkt. Mpango kwenye mkutano wa TAWIRI

Ninavuta picha iwapo wanafamilia wanaperuzi mitandao na kuona mijadala hii kuhusu baba yao. Inauma!
Inauma kwa nini? Serikali ndiyo inasababisha haya ikiwemo hiyo familia yake na yeye. Kama anaumwa, kila binadamu anaumwa. Kuumwa siyo jambo la kuonea aibu au kufanya siri. Hebu some huu mfano hapa: ''Makamu wa rais, Philip Mpango, yuko nchini Uingereza akitibiwa na anaendelea vizuri. Inategemewa atakuwepo huko kwa mwezi mmoja''. Hivi serikali ingetoa sentensi fupi kabisa yenye maneno hayo kingeharibika nini?
 
Kuna sehemu Paskal alilizungumzia hili
asee yule bro ana macho kama eagle.
Hakuna cha eagle , kwani wewe yule humjui ni nani?

CCM imetengeneza mambo ya hovyo sana kuna watu wanaonekana wapo wapo ila wana kazi serikalini huku wakijidai ni wafanyabiashara sijui wajasirimali.

Fuatilia vizuri ujue huyo jamaa ni nani sio upande wa pili anaojificha humu.

Nakupa tip hii muulize aliwahi kuwa ...wa ubalozi gani then akikujibu utaanzia hapo.
 
Wanajamvi,

Makamu wa Rais, Dr Phillip Mpango alikuwa awe mgeni rasmi wa mkutano wa TAWIRI unaofanyika Dodoma, hata hivyo amewakilishwa na Angella Kairuki.
View attachment 2834679

Hii inatia mashaka zaidi kutokana na Speculations ambazo tayari zipo kuhusu mtu huyu.
Nafikiri Serikali kwa sasa inapaswa kuujulisha umma juu ya suala hili. Kiongozi mmoja mkubwa (lakini asiwe Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa) anapaswa kujitokeza hadharani na kutoa ufafanuzi juu ya jambo hili ili kuzima minong'ono isiyokuwa rasmi ambayo tayari imeanza kuenea kwa kasi ya ajabu.
 
Inauma kwa nini? Serikali ndiyo inasababisha haya ikiwemo hiyo familia yake na yeye. Kama anaumwa, kila binadamu anaumwa. Kuumwa siyo jambo la kuonea aibu au kufanya siri. Hebu some huu mfano hapa: ''Makamu wa rais, Philip Mpango, yuko nchini Uingereza akitibiwa na anaendelea vizuri. Inategemewa atakuwepo huko kwa mwezi mmoja''. Hivi serikali ingetoa sentensi fupi kabisa yenye maneno hayo kingeharibika nini?
Siyo lazima
 
Majaliwa alikosea sana kusema Makamu wa Rais yupo nje kimajukumu, angesema yupo likizo ingetosha. Majukumu gani nje ya nchi mwezi mzima?. Majaliwa awe ana nyamaza.
PM angesema tu Makamu ana mapumziko ya kiafya au ameenda nje ya nchi kucheki afya yake. ingetosha kabisa kauli ya kidiplomasia na kiutu mzima.
 
Back
Top Bottom