Angelina Jolie aanza kusumbuliwa na Mama wa mtoto aliyemuasili

Angelina Jolie aanza kusumbuliwa na Mama wa mtoto aliyemuasili

Naona nyote mnafunga akili zenu. Twende taratibu. Huoni kitendo cha kumtoa mtoto wake akaasiliwe kilikuwa cha kumtakia mema mtoto wake? Si ajabu kama angalimg'ang'ania angelikufa kutokana na umaskini? Nyie vipi!
Huyo alitelekeza mtoto kwa bibi sio kumtoa.Na tatizo ni uvivu.Maskini wanajulikana.na mtoto hana ugomvi na mzazi.watu wanajadili kitendo cha huyo mama kuibuka sasa baada ya mtoto kukua wakati taarifa zilizotolewa kwa jokie zilikua tofauti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwa wabongo tunafanya au tuliwahi fanya hiyo mambo lakini kwakweli wabongo ni tatizo.
Mimi niliwahi kuasili watoto 3 wawili walikuwa ndugu na mmoja ni wa familia nyingine
Tatizo lilikuja pale wale wawili walipo fika chuo kikuu wana boom akijitokeza mtu kuwa ni mzazi wao na mambo kibaaao!
Nilipata usumbufu wa kila aina ikabidi niache watoto waamue kwasababu tayari ni wakubwa.

Akabaki 1 ambae sasa yupo kidato 4 huyu nae mlezi wake akaanza longolongo kwakuwa sipendi vyesi nikamburuza Ustawi wa jamii kwasababu sikumchukua mtoto kienyeji. Akasalim amri amuache mtoto asome Mtoto ataamua pa kwenda akifikisha miaka 18.

Kuasili watoto wa watu wasiojielewa ni mtihani.
Ukitaka kuasili nenda kaasili kutoka vituo vya watoto yatima tofauti na hapo fanya shughuli nyingine za kusaidia wasiojiweza. Lakini usiali mtoto mwenye wazazi hatakama hajiwezi kupindukia.
Hao WA chuo wameamuaje?
Pole sana
 
Huyo alitelekeza mtoto kwa bibi sio kumtoa.Na tatizo ni uvivu.Maskini wanajulikana.na mtoto hana ugomvi na mzazi.watu wanajadili kitendo cha huyo mama kuibuka sasa baada ya mtoto kukua wakati taarifa zilizotolewa kwa jokie zilikua tofauti.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata ungekuwa wewe ungeibuka! Hivi hapa Tanzania hakuna akinamama wanaoafiki mabinti wakapigwe Miti huko ili mradi waje na mboga nyumbani?

Okay chukulia ukweli wa mambo kwa tuliobahatika kukaa maeneo yale! Binti alimleta kwa mama yake ili amsaidie kumlea (je hapa ni single maza wangapi wanasukumizia watoto wao kwa mama zao kijijini?). Na Bibi alipoona hali ni mbaya na pengine mtoto atakufa akampeleka kwa yatima. Uamuzi huo ni wa kishujaa. Aliangalia uhai wa kichanga.

Tusilaumu ila tuelewe mwanamke aliyepitisha mtoto katika k yake hamsahau. Kikubwa ni kumfahamisha kuwa yupo na pindi akipata Mtumba amkumbuke. Masuala ya vyeti au majina si hoja, hoja ni DAMU. Binti ni damu yake na itabaki kuwa hivyo.
 
Mtoto kama ana maokoto amsaidie tu mama yake japo kuna uongo ulifanywa na kituo kilichokuwa kinamlea kwa angelina, na sidhani kama angelina atamkataza mtoto kumsaidia biological mother wake au kuwasiliana naye, japo kiukweli mtoto kwa sasa ni wa angelina.

Angalizo, huyo mama asije tu akaanza zile tamaa za kiafrica kumtaka mtoto kisa kaona anaweza kuponeapo


Ila mtoto kawa pisi aisee
Kwan ukishakua mtoto wa Angelina,unakua na maokoto?..


Arudi Ethiopia achake...sema anabahati keshakua Pini, lazima apate Sponsa.
 
Back
Top Bottom