Angelina Jolie aanza kusumbuliwa na Mama wa mtoto aliyemuasili

Angelina Jolie aanza kusumbuliwa na Mama wa mtoto aliyemuasili

Angelina Jolie aliadopt mtoto wa kwanza wa kiume nchini Cambodia, akaja kuadopt mwengine wa kiume nchini Vietnam, akaja kuadopt mtoto mwengine wa kike nchini Ethiopia, hakua peke yake kwenye safari hiyo alikua na aliyekua mumewe Brad Pitt waliadopt wote,

Kwa mtoto wa Ethiopia jina lake Zahara, Angelina alimkuta kituo cha kulea watoto yatima akiwa ana miezi 7 tu, wahusika wa kituo wakamwambia mtoto yule ni yatima wazazi wake walifariki kwa virusi vya Ukimwi, huruma ilimjaa Jolie na kuamua kumchukua kwa taratibu zote stahiki,

Ukweli ukaja kujulikana miaka mitatu baadae, mama mzazi wa Zahara alikua hai, ni binti aliyepata ujauzito kwa kubakwa, huku akiishi na bibi yake na mjomba wake wakiwa katika maisha ya ufukara, baada ya kumzaa Zahara hali ilizidi kua mbaya, Mama Zahara akatoroka nyumbani na kumuachia mtoto bibi yake, bibi nae kwa hofu ya kumkosa mtoto kutokana na lishe duni akampeleka kituo cha kulea watoto yatima na kuomba msaada wampokee mtoto, atakufa kwa njaa,

Mama mtoto alichokiomba ni kuongea na mwanae hata kwa njia ya simu, kumjulisha kua ana familia Ethiopia na mama yake hajafa pia anampenda sana.

Wala hakutaka kumchukua ampeleke wapi na umaskini bado umemtawala.
Hana lolote sema tu ashajua mtoto ana future ya uhakika target ya uyo mama wa kumzaa ni maokoto tu.
 
Kwan ukishakua mtoto wa Angelina,unakua na maokoto?..


Arudi Ethiopia achake...sema anabahati keshakua Pini, lazima apate Sponsa.
mkuu huyo binti ako na 18 tayari, ukute alishaanza modelling kitambo sema tu alikuwa hajatambulisha kwenye ulimwengu wa fashion rasmi, labda alikuwa anadeal na kampuni ndogo ndogo, usikute ana maokoto ya kutosha tayri, mkuu marekani sio bongo, watu hawatumiki ovyo ovyo/burebure. anaanzaje kurudi ethiopia wakati kwao ni marekani, huyo mama yake mzazi ni wa kumsaidia tu, ila huyo ni mtoto wa angelina na brad pitt
 
Mimi nina ndugu yangu ambae ni dada aliadopt mtoto, mtoto alipofikisha miaka 6 mama ake mzazi akajitokeza, sijawahi kufatilia ilo suala walimalizana vipi ila mtoto bado anakaa na sista mara moja moja hasa kipichi cha likizo anaendaga kwa mama ake mzazi na kukaa siku kadhaa then sista anaenda kumchukua. Anjelina amuinue kimaisha uyo mama mzazi suala la mtoto kuwa na upendo kwa mama ake mzazi libaki kuwa maamuzi ya zahara mwenyewe. Mama wa Zahara sio wa kulaumiwa umasikini ni mbaya sana, hopeful mtoto hajalishwa chuki kwa wazazi wake wa kibaiolojia.
 
Wapo kielimu zaidi lakini kibinaadamu nimewashuri kuwa wawapo na chochote wamsaidie ila wakimaliza chuo tufanye DNA kubaini uhalali wa kuwa ni mzazi wao.
Maana kwa maelezo tu hakuna uhusiano wa stori ya kupatikana watoto na yeye kuwa ni mzazi.
Bado wako na mapenzi na wewe?
 
Sawa we sio yatima kwakuwa umevuka umri wa miaka 18
Staki niadopt me yatima 🥹🥹
Kwani miaka 18 inabadili kuwa sip yatima?!
Hayo me sitaki kujua, kikubwa uniadopt nije kula bata, ukifa mwanao nipate ulisi 🤣🤣🤣
 
Hizo nazo ni mbinu za kulea. Kuliko angemuua. Mbona hii mbinu ni watu wengi wanafanya hivyo. Mfano India etc. Kuliko kubanana na mtoto ambaye hutakuwa na uhakika wa kumtunza, bora apelewe akalelewe huko. Hapo unaangalia uhai wa mtoto. Uhai wa mtoto unapewa kipaumbele.

Binti huyo naamini atamkana Biological mother sasa ila hapo mbeleni baada ya kunyaka mkwanja akajitegemea, atamrudia tu.
Ni mama yake mzazi lakini hana mamlaka naye.
 
Back
Top Bottom