Angelina Jolie aliadopt mtoto wa kwanza wa kiume nchini Cambodia, akaja kuadopt mwengine wa kiume nchini Vietnam, akaja kuadopt mtoto mwengine wa kike nchini Ethiopia, hakua peke yake kwenye safari hiyo alikua na aliyekua mumewe Brad Pitt waliadopt wote,
Kwa mtoto wa Ethiopia jina lake Zahara, Angelina alimkuta kituo cha kulea watoto yatima akiwa ana miezi 7 tu, wahusika wa kituo wakamwambia mtoto yule ni yatima wazazi wake walifariki kwa virusi vya Ukimwi, huruma ilimjaa Jolie na kuamua kumchukua kwa taratibu zote stahiki,
Ukweli ukaja kujulikana miaka mitatu baadae, mama mzazi wa Zahara alikua hai, ni binti aliyepata ujauzito kwa kubakwa, huku akiishi na bibi yake na mjomba wake wakiwa katika maisha ya ufukara, baada ya kumzaa Zahara hali ilizidi kua mbaya, Mama Zahara akatoroka nyumbani na kumuachia mtoto bibi yake, bibi nae kwa hofu ya kumkosa mtoto kutokana na lishe duni akampeleka kituo cha kulea watoto yatima na kuomba msaada wampokee mtoto, atakufa kwa njaa,
Mama mtoto alichokiomba ni kuongea na mwanae hata kwa njia ya simu, kumjulisha kua ana familia Ethiopia na mama yake hajafa pia anampenda sana.
Wala hakutaka kumchukua ampeleke wapi na umaskini bado umemtawala.