Anguko la Diamond Platinumz kimziki

Anguko la Diamond Platinumz kimziki

Achana na hiyo unayosema,hivi unajua Diamond ana video ambayo inasumbua sana kimataifa inaitwa Bum bum kamshirikisha Iyanya!!!? Kama unakodoleaga Channel 0,Trace na tv zingne za kimataifa utaona kule jamaa anavyosumbua mpaka hiyo Number 1 unayoisema watu washaisahau kule sema tu humu ndani haijaanza kupigwa kawapa kwanza hiyo Mdogomdogo.....haaaaa haaaaa huyu jamaa utamsubir sana kama unategemea atashuka yan ni sawa na kusubir meli ubungo
]
Nothing big than youtube,mengine ni bla bla
 
achana na kitorondo wewe, lazima utikise kichwa lile dude likipigwa redioni. bonge moja la hit na litasumbua sana kwenye soko la ndani

Tatizo watu wanaichukulia poa, ukitaka uifaidi ile kitu uisikilize kwenye mziki mnene, Dangote anajua bana, haters siku zote hawakosekani.

Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
Kama alivyoanza Feruzi kwenye michiriku akapotea kabisa.
Mwanzo lazima uwe na mwisho.
Diamond kitu gani bana
 
Kipindi hicho ukienda Uganda lazima uulizwe Mr. Nice hajambo?
Ukienda Dermarnk unaulizwa how is Mr NICE,kuna madem wa kizungu mpaka walijichora tatoo ya mr nice
 
tatizo la wa tanzania tina kasumba ya kuponda sana vitu loooo na kufikia zama hizi nadhan umeshakuwa utamaduni wetu
 
Binafsi Kitorondo Naupenda Vibaya sana kuliko hata hiyo Number one ,Yaani Umenibamba kinoma Kijana yupo Juu lazima Utafute soko kwa Watu wa Aina zote ,Wa Nje ya Mipaka , Wa Masaki , Na sisi Wa Mwananyamala + Mtogole hiyo ndio Biashara , Vannesa Mwenyewe Kashituka katoa wimbo wa Mipasho sasa hata sisi wa Mwananyamala Tunamsikiliza ...Diamond Mungu akuzidishie Uzidi Kusimama Imara Mtoto wa Bi Sandraaa

Mi simo! Kwa kuwa ni mara chache kushabikia Bongo fleva( Boxer, Viduku), Diamond nyota yake iko juu, hilo halina ubishi, lakini hiyo haithibitishi kuwa yeye ni mahiri zaid ya Wenzake. Ukiusikiliza huo my number one ( assume haujatoka video, for sure ni makapi), huo unazidiwa na Nitarejea wa kwake Diamond mwenyewe! Kwa hiyo video nzuri ya wimbo my number( uzur wa location za kiulaya ulaya/ south africa ambazo si realistic Tanzania) ndiyo pekee umepaisha wimbo huo. Kwa melody na ladha hauwez kamwe kuufikia wimbo wa Kassim Mganga- I Love U!

Kwa kuhitimisha bado nitaendelea kupenda nyimbo zangu za late 80 s' na 90: Vijana Jazz, Washirika, Bimalee, Msondo, Sikinde, OSS, Wandesa, Maquiz Original nk. Bila kusahau wanamuzik wake mmoja mmoja: Dr Remmy, Mzer Ngurumo, Othaman Momba, Eddie Sheggy, Hamza Kalala( Baba Jane 1&2-Bantu Group Band), Adam Bakar, Fred Benjamin, John Kitime, Shomar Ally, Bennovila Anthony, Bitchuka, Dede Shaban,Shakashia, Abdallah Mgonazero, Toto Tundu( Mhina Panduka), Max Bushoke, Chidumule, Hemed Maneti, Kidah Wazir, Ally Choki na Muumin Mwinyijuma( hawa walikuwepo enzi za Bantu Gruop Band wakiwa Vijana wadogo enzi hizo), TX Moshi, Suleiman Mbwembwe, Mwanyiro na wengine wengi ambao.sikuwataja ambao wengi pia walikuwa ni Wakongo man lakini wakipiga Muziki Tanzania. Kama mr Zomboko,John Kitime na wataalam wengine wanaweza kuja kutoa darsa tosha kuhusu Muziki wa zaman na sasa, kwamba nyimbo.nzuri za sasa huchukua miezi miwili tu, baadae huchuja! Nyimbo za zamani zilidumu sana! Tuchukue mifano hii: Vunja Mifupa- Samba Mapangala, Gojina- Marijan( kama sijasahau) na nyimbo kama Mtaa wa Saba, Shida, Rangi ya Chungwa nk. Nyingi ya nyimbo hizi zina miaka 25-40 hivi lakini ziko poa hadi leo zina hit!
 
Sababu zingine za dogo kuanguka vibaya hizi hapa;
1. Mda Wote Yupo Angani!
Huyu dogo kila siku yuko bize na shoo, mpaka anafkia stage anakosa mda wa kutunga, na hata kama akpata akili inakuwa imechoka hivyo anashndwa kutengeneza mzki mzuri.
2. Law Of Diminishing Marginal Utility.
Kitu ukikaa nacho mda mrefu unakichoka, hivyo unabidi utafute kingine. Mfano wa hivyo vitu ni Gari, Mke, Nyumba na huyo Diamond Wenu. Wasikilizaji washaanza kumchoka, hivyo wanatafuta radha mpya.
Nakaribisha kejeli kwa wale wagumu kuelewa.
CC Viol
 
Last edited by a moderator:
Binafsi Kitorondo Naupenda Vibaya sana kuliko hata hiyo Number one ,Yaani Umenibamba kinoma Kijana yupo Juu lazima Utafute soko kwa Watu wa Aina zote ,Wa Nje ya Mipaka , Wa Masaki , Na sisi Wa Mwananyamala + Mtogole hiyo ndio Biashara , Vannesa Mwenyewe Kashituka katoa wimbo wa Mipasho sasa hata sisi wa Mwananyamala Tunamsikiliza ...Diamond Mungu akuzidishie Uzidi Kusimama Imara Mtoto wa Bi Sandraaa

Hii ni point kabsaaa...tatizo watu wanafikiri mziki ni kufanya kitu ambacho wachache tu wanakipenda.
Unakfanya kitu watu wengi waridhike.kufanya kazi ili watu wengi iwezekanavyo waridhike.
Nashanga mijitu mingine haina uzalendo na vya kwao.
Dogo anapiga mzigo, chuki zako peleka kuleeee...
 
wabongo wivu sana.....dogo katoka mbali mpaka sahvi yuko level kubwa humu watoto wa mama mnabakia kulalamika tu dogo kakulia tandale
 
achana na kitorondo wewe, lazima utikise kichwa lile dude likipigwa redioni. bonge moja la hit na litasumbua sana kwenye soko la ndani

vp tena kwan kuna m2 kaibiwA.? ThooomAs hahaha mdogomdogo

Sent from my iPhone4 using JamiiForums
 
Sababu zingine za dogo kuanguka vibaya hizi hapa;
1. Mda Wote Yupo Angani!
Huyu dogo kila siku yuko bize na shoo, mpaka anafkia stage anakosa mda wa kutunga, na hata kama akpata akili inakuwa imechoka hivyo anashndwa kutengeneza mzki mzuri.
2. Law Of Diminishing Marginal Utility.
Kitu ukikaa nacho mda mrefu unakichoka, hivyo unabidi utafute kingine. Mfano wa hivyo vitu ni Gari, Mke, Nyumba na huyo Diamond Wenu. Wasikilizaji washaanza kumchoka, hivyo wanatafuta radha mpya.
Nakaribisha kejeli kwa wale wagumu kuelewa.
CC Viol

Ajitahidi amalizie ile nyumba naona ameconcentrate kwenye kile kisima ooopssss ni swiming pool mwaka sasa ... asije kufulia kabla hajahamia gheto lake
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom