Binafsi Kitorondo Naupenda Vibaya sana kuliko hata hiyo Number one ,Yaani Umenibamba kinoma Kijana yupo Juu lazima Utafute soko kwa Watu wa Aina zote ,Wa Nje ya Mipaka , Wa Masaki , Na sisi Wa Mwananyamala + Mtogole hiyo ndio Biashara , Vannesa Mwenyewe Kashituka katoa wimbo wa Mipasho sasa hata sisi wa Mwananyamala Tunamsikiliza ...Diamond Mungu akuzidishie Uzidi Kusimama Imara Mtoto wa Bi Sandraaa
Mi simo! Kwa kuwa ni mara chache kushabikia Bongo fleva( Boxer, Viduku), Diamond nyota yake iko juu, hilo halina ubishi, lakini hiyo haithibitishi kuwa yeye ni mahiri zaid ya Wenzake. Ukiusikiliza huo my number one ( assume haujatoka video, for sure ni makapi), huo unazidiwa na Nitarejea wa kwake Diamond mwenyewe! Kwa hiyo video nzuri ya wimbo my number( uzur wa location za kiulaya ulaya/ south africa ambazo si realistic Tanzania) ndiyo pekee umepaisha wimbo huo. Kwa melody na ladha hauwez kamwe kuufikia wimbo wa Kassim Mganga- I Love U!
Kwa kuhitimisha bado nitaendelea kupenda nyimbo zangu za late 80 s' na 90: Vijana Jazz, Washirika, Bimalee, Msondo, Sikinde, OSS, Wandesa, Maquiz Original nk. Bila kusahau wanamuzik wake mmoja mmoja: Dr Remmy, Mzer Ngurumo, Othaman Momba, Eddie Sheggy, Hamza Kalala( Baba Jane 1&2-Bantu Group Band), Adam Bakar, Fred Benjamin, John Kitime, Shomar Ally, Bennovila Anthony, Bitchuka, Dede Shaban,Shakashia, Abdallah Mgonazero, Toto Tundu( Mhina Panduka), Max Bushoke, Chidumule, Hemed Maneti, Kidah Wazir, Ally Choki na Muumin Mwinyijuma( hawa walikuwepo enzi za Bantu Gruop Band wakiwa Vijana wadogo enzi hizo), TX Moshi, Suleiman Mbwembwe, Mwanyiro na wengine wengi ambao.sikuwataja ambao wengi pia walikuwa ni Wakongo man lakini wakipiga Muziki Tanzania. Kama mr Zomboko,John Kitime na wataalam wengine wanaweza kuja kutoa darsa tosha kuhusu Muziki wa zaman na sasa, kwamba nyimbo.nzuri za sasa huchukua miezi miwili tu, baadae huchuja! Nyimbo za zamani zilidumu sana! Tuchukue mifano hii: Vunja Mifupa- Samba Mapangala, Gojina- Marijan( kama sijasahau) na nyimbo kama Mtaa wa Saba, Shida, Rangi ya Chungwa nk. Nyingi ya nyimbo hizi zina miaka 25-40 hivi lakini ziko poa hadi leo zina hit!