a4afrika
JF-Expert Member
- Apr 13, 2012
- 1,456
- 1,459
1. Kukiuka Katiba si sawa na Rule of Jungle. Hakuna Katiba Kamilifu, zote zina mipaka ya muda na mazingira. Hilo linahalalisha Ukiukwaji wake pale inaposhindwa Kulinda Maslahi ya Umma kutoka na Udhaifu wake.Ni kosa kubwa sana! Katiba ni makubaliano na mwongozo wa jamii. Kwamba , kuna taratibu zinapaswa kufuatwa ili tuishi kama jamii. Katiba imetoa nafasi 'kukiukwa' katika msingi ya kikatiba. Mfano, Rais akapewa haki ya kumsamehe muuaji aliyethibitishwa na mahakama
Rais kapewa haki ya kuingiza nchi vitani kwanza lakini pia kuna utaratibu wa kufanya hivyo
Katiba imempa haki Rais juu ya umiliki wa ardhi ya MTU anaweza ku revoke hati ya mali ya mtu
Kwahiyo mfumo mzima wa katiba unatoa taratibu ikiwemo 'ukiukwaji wake'' lakini siyo open season kwamba anaibuka mwendawazimu anakiuka katiba tunajenga uhalali.
Uhalali wa ukiakwaji wa katiba upo ndani ya katiba siyo
Hata Simba na Tembo wanaishi kama jamii, tofauti baina yao na sisi ni weledi! Sisi tunaishi kwa taratibu ili kuepuka 'rule of the jungle'' . Kutofuata taratibu tulizojipangia kwa njia ya katiba ni kufuata mfumo wa rule of the jungle ambao 'tumeujaribu'' hivi karibuni na tunajua matokeo yake.
Siyo tuhuma hewa, tuhuma zilikuwepo na utawala wa JPM unajua hilo. Kilichotakiwa ni kueleza zipo wapi pesa za walipa kodi, hadi anaingia kaburini hakuwahi kujibu. Wasaidizi wake akiwemo mtoto wa Dada yake hakuna anayesema 'ni tuhuma za uongo'' . Kwavile hakuna anayekanusha basi aliyesema anabaki kuwa mkweli, hazijulikani zilipo 1.5T, CAG Assad
Ni sawa na anachosema Zitto hakuna maelezo ya 70B zilizokwenda Mwanza! CAG Kichere
Kumstaafisha kwa lazima ilikuwa kuondoa ''udhia'' ili asije ibua tena madudu mengine
Kumuondoa hakujibu hoja wapi zilipo 1.5T . Kabla ya jibu wapo wanaouliza 70 Bilioni zilikuwa za nini. Chuki haikuwahi kujibu tuhuma ndio maana siku za karibuni rekodi ya Magufuli inawekwa wazi na wapo wasiotaka kama wewe kwa kujua yapo mengi katika rekodi!!!
Kuna aina mbili za usomaji, kusoma maandiko kwasababu tunaziona herufi na kusoma maandiko kwa kuyaelewa. Nina shaka sijui upo wapi katika makundi hayo
Katiba haielengi kueleza usahihi wa taarifa za CAG. Katiba inalenga kuzuia upuuzi kama ule wa kumstaafisha CAG ili kuendelea kufanya watakavyo.
Tuliishi kwa mazoea ya viongozi waliotangulia wakiogopa taratibu tu kwa uadilifu
Tumejifunza kuwa kila 'kiingacho si dhahabu' . Tuipitie katiba ili kuzuia ubazazi usijitokeze tena
Ndio maana nasema maoni ya watu hayawezi kuwa chuki na siwezi kukubaliana nawe eti nisiwe na chuki. Kwani shutuma nizitoa dhidi ya Magufuli ni zipi? Mbona huelezi ili tuweke ushahidi!
Siwezi kuweka ushahidi bila tuhuma, weka tuhuma mezani kwanza !
Rekodi ya Magufuli ndicho kitu pekee kitakachosaidia legacy yake.
Watetezi wake wajikite kuieleza rekodi yake, wasiokubaliana naye wanajenga hoja zenye mantiki, zijibiwe kwa mantiki
Hakuna mtu mwenye mamlaka ya ustawi wa umma. Ustawi wa Umma ni jukumu la Umma na ni wajibu wa Umma na haki ya Umma. Kilichotokea kwa watu kujivika joho la Tanzania ulikuwa uzuzu 'imbecile'' . Tukatae uzuzu huo na hapa ndipo tunahitaji rekodi .
Rekodi ya kudhani Tanzania ni mtu na rasilimali za nchi za kikundi ni mbaya ndiyo inajadiliwa!
Kudhani ustawi wa jamii unahitaji kuigawa jamii katika misingi ya udini, ukabila na ukanda ni jambo la kulaaniwa na wenye akili timamu. Hilo haliondoi haki ya ' collective imbecilisation'
Kwamba Marehemu anasemwa kwa flyover, JNHP , SGR tu! hatusemi rekodi nyingine kwa kisingizo cha Marehemu hasemwi ili kuficha lundo la uchafu na uvundo linalonuka
Uvundo haupuuliziwi ubani unaondolewa na huwezi kuuondoa kama husemi upo wapi
Kuna watu wamedhulumiwa wanadai haki zao japo kuombwa radhi. Kuna watu hatujui wapo wapi, hakuna wa kuwasema isipokuwa tunaamini marehemu hasemwi.
Naam ni jukwaa la wote na tuwaache wenye nyongo zao wateme.
Wanotetea nyongo nao wana haki lakini tusijifiche chini ya kapeti linalovunda kwa kisingizio cha Marehemu hasemwi! Ni marehemu gani huyo ? Nyerere ? Mkapa? au Magufuli?
Kwanini Magufuli? nini kinafichwa !
2. Wewe lete Ushahidi kwamba 1.5t zilikuwepo kweli, na si kwamba ni Tuhuma hewa kama uwezekano mwingine. TUPE USHAHIDI HAPA.
Kwamba "Kumstafisha ni kuondoa udhia, asije kusema madudu mengine."
Nadhani umekuwa mpiga ramli sasa. MATAMANIO yako zao la Hisia zako hayatoshi kutetea hoja yako. Hata Mimi naweza sema kama hizo, mfano, Assad alinunuliwa kumchafua Magufuli, kwa busara Magufuli alimstaafisha bila kumfunga. (huo ni mfano sawa na hoja yako)
3. Tuhuma zisizo na Ushahidi, Ni Chuki. Ulitaja kwa kuunga mkono tuhuma za Udini, Ukanda, Ukabila, Ufisadi, nk... Je, ulileta ushahidi?
4. Acha kujidanganya, Ustawi wa Umma u mikononi mwa kila RAIA kulingana na nafasi yake. Nafasi ya Rais haiwezi kuwa sawa na mjumbe wa nyumba kumi. Hekima ni kutambua na Kuheshimu wajibu wa kila RAIA kulingana na nafasi yake.
Uzuzu ni kujaribu kukataa nafasi yako na kujilinganisha na wengine. Na hicho ndicho cha kupigwa vita. (Kwa bahati mbaya wasomi Wetu, wastaafu, WanaCCM, Wapinzani, Watu wa Dini, nk...mmechagua upande wa kupigwa vita) Magufuli ametufundisha kutowaonea aibu tena. Tutawapiga Vita.
5. Humu ndani hakuna anayekupangia cha kusema juu ya marehemu. Hivyo usiirudierudie manung'uniko yako. TEMA NYONGO NDUGU. Nasi tupo tutakusikiliza na kujibia zile utakazopotosha au kuhitaji hoja za upande mwingine. Usilielie.
6. "Kwanini Magufuli?"
JIBU: Ni Mtu wenye Matunda. Na werevu ni wachache sana kuliko wapumbavu!
Hotep!