a4afrika
JF-Expert Member
- Apr 13, 2012
- 1,456
- 1,459
1. Ndio ni facts, lakini Tuhuma ni huu ya maoni yako juu ya hizo facts kwamba ni Mbaya.Hakuna tuhuma kuna facts. Je, Magufuli hakuhimiza kujifukiza ? Lini Magufuli alivaa Barakoa?
Je, hakusema Barakoa zinavitu anajua siri za nchi? Je, hakuhimiza maombi, je hakukutaza chanjo, je hakuagiza banda la kujifukiza Muhimbili, je, hakutuma ndege na Profesa Kabudi kwenda Madagascar, Je hakuzogoa wavaa barakoa kanisani?
Yes kwasababu tunawasiliana kwa sayansi pasi kujuana. Kila unachotumia wewe ni zao la kazi za sayansi. Ninaikubali sayansi na matokeo yake pasi na shaka!
Hujajibu hoja, hayo yanayonihusu yasikusghulishe
Hoja ni hii, taja jambo moja ambalo Magufuli amelifanya na ambalo halijawaji kufanywa na kiongozi mwingine yoyote kwa mujibu wako
Hakuna chuki, hebu tujadili kuna vita ya uchumi kuhusu Corona kwa lipi.
Nani anapigana vita ya uchumi na Tanzania, na vita hiyo imeshaije maana hatusikii tena
Yes zipo hotuba za Magufuli akihimiza kujifukiza. Waziri wake Jafo akatekeleza maagizo ya boss na wengine wakiwemo wabunge na mawaziri wakaunga tela.
Tuna ushahidi pale Muhimbili wa banda la kujifukiza
Jibu hoja usijadili mtu, sisi ni wanadamu tuna udhaifu tu kama viumbe wengine.
Majadala usiwe juu ya madhaifu yetu bali juu ya matokeo ya madhaifu yetu hasa kwa truliowapa dhamana. Tafadhali Jibu hoja, na hapa ni moja tu, je ilikuwa sahihi Rais JPM kusema '' watu wa kaskazini wasubiri''?
Muhimu hapa ni kuwa kila mtu ana uhuru wa kuchagua. Nipo katika rekodi hapa JF nikisema chanjo iruhusiwe asiyetaka asisumbuliwe. Mauti ni tukio la mtu binafsi.
Kisichotakiwa ni kuingiza imani za watu kwa wengine na kuwanyima haki ya wanachotaka
Waliokufa wakitamani chanjo hawakutendewa haki.
Kuzuia chanjo kwa imani ya mtu binafsi ima kidini au kutoamini sayansi au kutoamini mabeberu haukuwa uungwana. Kuzuia takwimu watu wasijue nini kinatoke haikuwa sahihi. Kuzuia watu wasitamke ugonjwa ilikuwa collective imbecilisation ya hali ya juu. Haikuwa sahihi ! period
Ni maoni yako yaheshimiwe, lakini pia wanaopinga yako hawawezi kuwa wapumbavu kwasababu huna hati miliki ya maoni!
Wengi kwa takwimu zipi? Kumbuka kuna Quantity and Quality
2. Tunachokuambia ni kuwa IPO sayansi beyond hii yako ya maabara hizi. Kibaya ni kuwa, hutaki kuruhusu macho yako kufika huko.
3. Juu ya vita ya Uchumi sitakujibu tena, maana najisikia aibu Mimi.
4. Uongo si Magufuli kuhimiza kujifukiza, Bali kusema Magufuli amewataka watu wajifukize nyasi (Luna mahali uliziita nyasi za hovyohovyo) Huo ni uongo.
5. Udhaifu wako wakati Fulani ni muhimu kusemwa ili kukusaidia kuwa huru katika hoja zako.
6. Haikuwa Sahihi kusema watu Fulani watasubiri. Nami nakuuliza, Je, walisubirishwa katika nini? Kwanini hawakusubirishwa reli, hospital, shule, Barbara na hata soko?
7. Hoja kwamba Kila Mtu ana Uhuru wa Kuchagua ni danganyia Toto, nashangaa mnapozibeba kama zilivyo na kuzishupalia shingo.
Uhuru ni KiiniMacho. AMKA UNAACHWA.
8. Wengi huanzia wawili. Na sijasema kuwa ni wengi kuwazidi ninyi, ila niwazi idadi imeongezeka kwa ninaowafahamu Mimi.
*Kuna wanaokufa kwa kutamani Ushoga pia. Wapo wafao wakitamani mauaji pia.
Matamanio ya mtu si factor kubwa katika maamuzi.