Anguko langu kiuchumi lilianzia hapa. Wakuu tuinuane

Anguko langu kiuchumi lilianzia hapa. Wakuu tuinuane

Kama ni usimamizi dhaifu, usikate tamaa anza tena ila zingatia kitu "usimamizi" . Kama ulikuwa makini na mambo yakawa vile muone Mshana Jr humu JF atakushauri.
 
Pole mkuu ningekusaidia lakin tatizo hata Mimi nimekula mtaji
 
Kifupi tu naona nili panic hivyo sikufanya utafiti. Yaani ile kuingia kichwa kichwa. Kwa upande wa kuku walikua wanakufa sana. Lakin kwenye kilimo msimu haukua mzuri na nililima kilimo cha kutegemea mvua hivyo mavuno yalikua hafifu sana. Kama ningechukua muda kufanya utafiti maana yake labda ningetafuta mashamba ya umwagiliaji. Mtu unapoanza kuanguka kiuchumi kama hautaweza kutuliza kichwa basi utaanguka mpaka chini kabisa. Kwa sababu kuna ile hali ya kutaka kurudi juu kwa haraka na hapo ndipo unaweza kufanya kitu kwa haraka na ukazidi kuporomoka.
pole sana kaka, hiki unachoongea ndio kiliniangusha mimi kiuchumi kuanzia mwaka 2016 mwishoni kufika 17 mwishoni nikawa hoi kabisa..........

ninachowashauri vijana wenzangu kwa sasa ni kwamba ktk jambo lolote linalokupata maishani, hakikisha unapata maarifa mapya ya kukutoa ulipoangukia maana maarifa yaliyokufanya uanguke KAMWE hayawezi kukuinua tena.........

kizazi hiki (au niseme kwenye jamii zetu) tunaishi kama wanyama wa porini, hatuna washauri (mentors) wa kutufanya tutembee vizuri, ni maisha ya kubahatisha wengi ndio tunaishi
 
Mkuu ni vyema uwe unamaliza kusoma mpaka mwisho. Lakini zaidi tujifunze kusoma au kusikiliza ili kuelewa sio kujibu. Shukrani.
Pole na usikate tamaa. Kuna wenye changamoto kubwa zaidi. Wahenga walisema ukitaka kujua una bahati tembelea hospital uone watu wanaoteseka japo fedha wanazo. All in all. Kwa kifupi ulikuwa hujafikia uchumi wa kati hata kidogo. Sema kipindi hicho deal la kubangaiza lilikuwa limekukubali hivyo ukawa unapata visenti vya matumizi vilivyokufanya udhani uko kwenye maisha mazuri.
 
Sikua nabangaiza mkuu, nilikua napata pesa kutokana na vyanzo vinavyoonekana na sio deals za kuzuka. Na nilijijenga kwa muda kufikia hapo ndio maana nasema nilikua kwenye middle class economy. Hata hivyo nashukuru kwa hamasa.
 
Jiwe pia kahusika katika kuua biashara yako. Amini amini nakuambia.
Yule mzee kavuruga sana uchumi wa vijana wengi.
Pole.
Kiukweli siwezi kuelekeza lawama au kumnyooshea mtu kidole kwamba amehusika na anguko langu kwa kuwa sababu ziko wazi. Kwa hiyo mkuu sikuungi mkono katika haya mawazo yako lakini pia sikupingi.
 
pole sana kaka, hiki unachoongea ndio kiliniangusha mimi kiuchumi kuanzia mwaka 2016 mwishoni kufika 17 mwishoni nikawa hoi kabisa..........

ninachowashauri vijana wenzangu kwa sasa ni kwamba ktk jambo lolote linalokupata maishani, hakikisha unapata maarifa mapya ya kukutoa ulipoangukia maana maarifa yaliyokufanya uanguke KAMWE hayawezi kukuinua tena.........

kizazi hiki (au niseme kwenye jamii zetu) tunaishi kama wanyama wa porini, hatuna washauri (mentors) wa kutufanya tutembee vizuri, ni maisha ya kubahatisha wengi ndio tunaishi
Hili ni tatizo kubwa sana kwa kizazi na jamii kubwa ya africa
 
Pambana!!! Wengi tunaoanguka Koo zetu zimegubikwa na umaskini, tukitambua hili tutatoboa.
 
Kawaida hiyo huwa inatokea...mimi nilichojifunza kwenye kufulia kikubwa inatakiwa usipanick...ukipanick tu kwisha habari utapoteza mpaka kile kidogo kilichobakia...
 
Tukiwambiaga muwafungulie wake zenu walau kabiashara mnahis wanaenda kugongwa nje
Shukuru kama wakwako anaendesha biashara ila usifikiria sie wajinga.
Mke unamfungulia biashara lakini Kodi kila mwaka unalipa wewe na hell ya matumizi hatoi.... Ngoja ifike zamu yako hata Mimi nilikua na jeuri ka hizi
 
Ndugu yangu hatuwezi kulaumu wanawake kwa ujumla wao, lakini baadhi yao ni kama watoto. Mtoto anahitaji huduma tu hawezi kuelewa kuhusu mabadiliko yako ya kiuchumi au hali yako mbaya ya kila siku.
Bro linapokuja kwenye ndoa na mna watoto wanasoma, hichi unachosema haki make sense anymore... Biblia inasema mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono miwili, hivyo pia anaweza kuijenga mwenyewe akiamua.

Bro kipindi nina hela nilikua nawaambia wenzangu hawajui kumhandle mwanamke, kwakua mwanamke anataka care,zawadi,time n.k

Nilikua napata respond nzuri (mke) kwakua atataka mitoko ntamtoa sasa nimefulia tushughulike na vipaumbele mwenzako anataka luxuries ashindane na wenzake ikilazimu hata ada za watoto zisilipwe ili fahari yake itimie.

Bro hivi viumbe vipo complecated saana na hakuna mbabe wao isipokua umkute anahofu ya Mungu.
 
Shukuru kama wakwako anaendesha biashara ila usifikiria sie wajinga.
Mke unamfungulia biashara lakini Kodi kila mwaka unalipa wewe na hell ya matumizi hatoi.... Ngoja ifike zamu yako hata Mimi nilikua na jeuri ka hizi
🤣🤣🤸‍♂️🤸‍♂️🤸‍♂️ pole mwamba
 
Dah pole sana kaka, maisha yanasiri sana! Nikikumbuka mwaka 2017/2018 nilikuwa naweza kuingiza faida ya milion 1 kwa mwezi na sasa Sina hata mia. Huwa nasema maisha yetu yanasiri ambayo wengi huenda hatujui. Ukangalia story ya kaka yangu hapa unagunduka hakuna makosa alioyofanya ya kusababisha hali alionayo sasa.

Pole sana kaka, 2019/2020 kwangu mambo yalikuwa hovyo sana kiasi kufikia kulala Na njaa. Mpka sasa mambo sio Powa lakini soon naamini nitarudi katika hali ya miaka miwili iliopita[emoji1317]
 
Back
Top Bottom