Anguko langu kiuchumi lilianzia hapa. Wakuu tuinuane

Anguko langu kiuchumi lilianzia hapa. Wakuu tuinuane

Dah pole sana kaka, maisha yanasiri sana! Nikikumbuka mwaka 2017/2018 nilikuwa naweza kuingiza faida ya milion 1 kwa mwezi na sasa Sina hata mia. Huwa nasema maisha yetu yanasiri ambayo wengi huenda hatujui. Ukangalia story ya kaka yangu hapa unagundua hakuna makosa alioyofanya ya kusababisha hali alionayo sasa.

Pole sana kaka, 2019/2020 kwangu mambo yalikuwa hovyo sana kiasi kufikia kulala Na njaa. Mpka sasa mambo sio Powa lakini soon naamini nitarudi katika hali ya miaka miwili iliopita[emoji1317]
 
Pole sana mkuu ni wengi sana tunakabiliwa na changamoto za namna hiyo,cha muhimu ni kutokata tamaa.
Mkuu kwema. Nimesoma uzi wako. Na mm napitia wakati km wa wakwako. Upo wapi japo tubadilishane uzoefu kuona tunachomokaje mkuu wangu
 
Usiyoyajua
Nyumba hizi za kupanga baadhi zina mikosi au neema. Unaweza kukaa kwenye mambo yako yakaenda mrama ila ukaondoka ukaenda sehemu nyingine mambo yakanyooka.
Km bado upo hapo, hama kwanza maana hata ukiwezeshwa bado hautafanikiwa.
Kifupi tu naona nili panic hivyo sikufanya utafiti. Yaani ile kuingia kichwa kichwa. Kwa upande wa kuku walikua wanakufa sana. Lakin kwenye kilimo msimu haukua mzuri na nililima kilimo cha kutegemea mvua hivyo mavuno yalikua hafifu sana. Kama ningechukua muda kufanya utafiti maana yake labda ningetafuta mashamba ya umwagiliaji. Mtu unapoanza kuanguka kiuchumi kama hautaweza kutuliza kichwa basi utaanguka mpaka chini kabisa. Kwa sababu kuna ile hali ya kutaka kurudi juu kwa haraka na hapo ndipo unaweza kufanya kitu kwa haraka na ukazidi kuporomoka.
 
Wakuu poleni na harakati za maisha.

Mpaka kufikia mwaka 2018 maisha kwangu yalikua tambarare kabisa, sikua na uchumi wa juu lakini nafikiri nilifikia uchumi wa kati wa juu. Biashara ya kuingiza pesa kila siku ambayo niliisimamia mwenyewe na nyingine hizi za kuleta hesabu kwa wiki kama boda boda zilinifanya niweze kumudu maisha kwa kiasi chake.

Kutokana na umri wangu na vile vile niliona kila kitu kinaenda vyema nikaazimia mwaka 2019 mwishoni nioe. Lakini mwaka 2019 ulipoanza tu mambo yakaanza kubadilika. Nyumba ambayo nilipanga kwa ajili ya biashara ilitakiwa kuvunjwa ili kujengwa kisasa zaidi hivyo nikalazimika kuhama, na huko nilikohamia ndiko kila kitu changu kiliharibika. Nilihamia mtaa mpya, biashara ikawa mbaya na hatimae mauzo yakakata dukani.

Ili kujaribu kuinuka nikauza pikipiki zangu na kuongeza mtaji, lakini bado nikashindwa, na hatimae nikafunga biashara. Wakati biashara inasumbua na mchumba nae akaanza kusumbua, tukawa hatuelewani. Suala la kuoa likawa limeota mbawa kwa muda na kutokana na huduma kukata mchumba akakimbia.

Mwaka 2020 nilipata hela kdg nikashauriwa na kushaurika niingie kwenye ufugaji wa kuku, na pia nililima mpunga huko ifakara. Huko nako nilichoma hela maana hakuna nilichoambulia hivyo mwaka 2020 ukaisha vibaya tena.

Wakuu niko hapa kuomba yeyote ambae anaweza kunisaidia kazi yoyote nitashukuru na kufanya kwa moyo wote. Kifupi ndani ya miaka mitatu nimepoteza kila kitu kiasi kwamba ilifika point ningeweza kuwa homeless hapa mjini kwa sababu kodi ya nyumba ilikua tatizo pia.

Kabla ya kuanza kufanya biashara zangu huko nyuma mimi ni kinyozi mzuri tu na hata sasa ndio kazi inayoniweka mjini japo ninafanya kazi kwenye salon hizi ndogo ndogo tu ili nipate hela ya kula. Lakini maisha haya sio ya kutafuta hela ya kula tu ukizingatia kuwa umri unaenda. Pia nina uwezo wa kusimamia miradi na nina wazo kubwa la biashara ambalo utekelezaji wake ni lazima mtu uwe na pesa.

Mimi ni kijana wa miaka 36 na ni baba wa mtoto mmoja.

Kwa atakae kuwa tayari kunisaidia nina mdhamini ambae kuhusu suala la uaminifu wangu yeye atasimama kati yetu.

Shukrani!
Kosa kubwa ulilolifanya ni kuua vyanzo vingine vya mapato ili uinue chanzo chako cha mapato kilichokuwa kinatetereka.
 
Pole sana, ukiona biashara inashamiri fungua tawi lingine liite B . A ikibomolewa hamishia bidhaa B . Uwe na nidhamu ya hali ya juu kuhusu pesa. Niulize, huyo mwanamke alikuwa anakupa ushauri gani kibiashara? Inaweza ikawa ndio chanzo cha kufilisika. Jua tu kuoa ni mtihani mkubwa sana, maombi ya hali ya juu yanatakiwa wakati wa kuoa.
 
Back
Top Bottom