Nisubiri kitu gani wakati mkataba umeshakuwa unatekelezwa tangu October 2022?
Hiyo miaka yako 30 unaiweka kwa mapenzi yako tu, niambie umeiona wapi kwenye yale makubaliano yaliyowafanya DP World waanze utekelezaji wao tangu mwaka jana?
Kwenye yale makubaliano ya mwaka jana, Article 23 inazungumzia duration and termination, ambapo hapo hawajaweka muda maalum wa kwisha mkataba, kama ni miaka miwili, tatu, tano, kumi au 100..
Wao wamezungumzia tu kwamba, mkataba unaweza kwisha pakiwepo na permanent cessation of all project activities, sasa hebu niambie, hizo project activities zinaweza seize vipi? au mpaka pale maji ya bahari na maziwa yatapokauka?!
Ok, bado kipengele kidogo cha kwanza kwenye hiyo article 23 niliyokupa kinasema, mwarabu anaweza kuamua kuendelea kuwepo akiona bado anacho cha kuvuna, hata kama maji ya bahari na maziwa yatapokauka!.