Anna Tibaijuka: Ndugai aliniambia kwamba suala la Lissu ni “Maelekezo”

Umezunguzunguka lakini ukweli unaujua zile pesa zilipigwa kutoka mabenki makubwa. Walitumia formula ya kila aliyeingiziwa kupata milioni 45, waliingiziwa maaskofu wakatoliki, wafanya biashara na baadhi ya, mawaziri akiwemo Mama Tibaijuka.

Hukuwahi kuwasikia maaskofu wakiongelea ufisadi wakati ule, walihusika kuchota ule mpunga. Wameshangaza watu baadhi yao haswa Father Kitima kusikika akiikosoa biashara ya uwekezaji wa DP World kule bandarini wakati anaokula nao kantini pale Kurasini walifaidika moja kwa moja na pesa za yule Mzee wa Kihaya.
 
Tukumbuke kuwa wapinzani walimkosea heshima marehemu tena bungeni wakati shughuli rasmi zikiendelea.

Tunapowaonea huruma wapinzani na hulka zao tukumbuke ubinadamu wa RIP Ndugai akiwa katikati ya kazi kichwa kimepata moto.
Walimkoseajr? Walimkosea yeye binafsi au kanuni za bunge?
 
Magu alikuwa anaendesha nch km familia yake.yule dingi alikuwa na roho mbaya arifu
Roho mbaya yake inasababisha hata mazuri kidogo aliyoyafanya yapotee kabisa
ROho mbaya haifai
 
Tiba hana akili yule kanyigo; kwani yeye alikuwa mhifadhi wosia wa Ndu_gay? Kama alikuwa mweka wosia kwanini auweke kwenye mitandao bila familia ya mwathirika kuridhia? Kwa hiyo huwa wanadanganya Watanzania kwamba bunge ni mhimili unaojitegemea katika kufanya uamuzi kwa niaba ya wananchi kumbe ni idara ya rais?

Tiba ni mnafiki na ni sehemu ya wana mtandao ambao ndio kikundi hatari sana cha siasa hapo Tanzania.

Kiongozi yeyote mwenye wigo wa kufanya maamuzi kwa mjibu wa sheria halafu matendo aliyofanya yakionesha madhara anajitetea kwamba alishinikizwa na mamlaka ya mhimili uliojichimbia ni aibu sana. Ukiwa kiongozi unatakiwa kukubali kuwajibika sio kutupa lawama kwa mtu asiyekuwepo kujieleza kuhusu hooja hiyo.

Tiba ni mnafiki sana na chuki binafsi baada ya kutemeshwa bungo la Rugemalila. Msimsingizie JPM mambo ya kijinga
 
Walimkoseajr? Walimkosea yeye binafsi au kanuni za bunge?
Kutoheshimu kanuni za uendeshaji wa bunge, mbunge hutakiwi kuwa umesimama wakati spika kasimama, unaketi chini.

Wanamheshimu spika mawaziri wakuu sembuse mbunge asiye na cheo chochote!.
 
Tibaijuka anaweza pia akawa yuko kwenye mipango ya kumchafua Magu maana Tibaijuka ni Mwizi amejilimbikizia mapori kizila myaga pale Magu kuna baadhi alinyanganywa nae huyo Tibaijuka bado hajapona anasumbuliwa na mzimu wa Magu Pesa za Escrow huyu mama ni mnufaika pia na King wa hii game ya Escrow ni nani? Ndugai na Magu ilikua ni vigumu kuwatenganisha
 
Kwa usemi huu anataka tuamini kukamtwa na kuzuliwa kesi ya uhaini pia ni maelekezo au ?????
 
Umezunguzunguka lakini ukweli unaujua zile pesa zilipigwa kutoka mabenki makubwa.
Hayo mabenki yalifungua kesi ya kuibiwa hela? Au nani alifungua kesi ya kuibiwa hela na hukumu ikasemaje?

Wewe unatumia basis ipi kusema ile hela iliibiwa, kutoka kwa nani na iliibiwa na Mama Tibaijuka?
Walitumia formula ya kila aliyeingiziwa kupata milioni 45, waliingiziwa maaskofu wakatoliki, wafanya biashara na baadhi ya, mawaziri akiwemo Mama Tibaijuka.
Ni sheria ipi Tanzania inasema ukiingiziwa kiasi chochote cha hela ukiwa mfanyabiashara, askofu au waziri inakuwa ya wizi?
Kwamba hao watu huwa hawafanyi transactions za kupokea?
Hukuwahi kuwasikia maaskofu wakiongelea ufisadi wakati ule, walihusika kuchota ule mpunga.
Hakuna sheria inayosema ni lazima maaskofu wazungumzie hela, ni kazi ya CAG na mamlaka husika. Una elimu gani?
Wameshangaza watu baadhi yao haswa Father Kitima kusikika akiikosoa biashara ya uwekezaji wa DP World kule bandarini wakati anaokula nao kantini pale Kurasini walifaidika moja kwa moja na pesa za yule Mzee wa Kihaya.
Sasa kumbe ni pesa za mzee wa Kihaya.
So, unampangia huyo mzee namna ya kutumia pesa zake? Unapata mamlaka gani za kukataza mtu kugawa hela zake, unahisi kila mtu ni njaa kali na mpiga mihayo kama wewe?

Wewe ukiamua kunywa ulanzi wa elfu tatu, au kula mabumunda ya elfu tano, from nowhere tuseme umeiba hela?
 
Wezi mnatetea wizi. Pesa za escrow zilipigwa zikatoka kwenye akaunti halali zikaingizwa kwenye akaunti za watu binafsi. Maongezi mengi marefu hayana faida, utetezi tu ambao kwa muda huu hauna msaada wowote.

Mnaleta mbwembwe za elimu, wizi na ufisadi haujali elimu, kwa mataifa makini unapelekwa mahakamani na unafungwa.

Kikwete alipowasili uwanja wa ndege anaulizwa kuhusu pesa hizo kupigwa anabakia kujiumauma. Pale alidhihirisha udhaifu katika uongozi wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…