Anna Tibaijuka: Ndugai aliniambia kwamba suala la Lissu ni “Maelekezo”

Ref to comment #7!

Jamaa kaifunga mada na wewe umekuja kuweka cement kuikamilisha!

Maneno yanayotoka katika kinywa cha Anna Tibaijuka(mama wa 'hela ya mboga') fisadi aliyevuna mgao wa mabillion ya Escrow, kutoka kwa mhaya mwenzake Fisadi Rugemalila, kamwe hawezi kuwa na kauli ya kumpamba Magufuli.

Si mtu wa kumwamini kwa chochote kutokana na kauli zake tata anazozitoa kila mara apatapo nafasi ya kufanya hivyo.

Lengo lake ni kuipoka saikolojia ya jamii aonekane kuwa yeye ni 'mtu safi' asiye na mawaa katika jamii, wakati mikono yake inanuka ufisadi uliopitiliza!

Mimi hata ule muda wa kumsikiliza huwa sina.
Ni mnafiki peke yake asiyejua Magufuli alivyoingilia mihimili yote kibabe. Muulize Pasco kilichomkuta baada ya kumuuliza swali kwa nini Rais anaiingilia mihimili mingine.
Pamoja na hizo za kina Rugemalira na Tibaijuka,ni nini kilimzuia Magufuli kuwafikisha mahakamani? Kwa nini aliamua kuwatesa tu kwa kuwaweka kizuizini bila ya kuwafikisha mahakamani ikiwa alikuwa na uhakika na ufisadi wao?
Ni kama tu scandal ya Hayati Lowasa,mtu akifikia mpaka kuhama chama na kusababisha Magufuli kuwa Rais wa kwanza kushinda kwa kura kiduchu tangu mfumo wa vya vingi uanze, mbona hakuwahi kufikishwa mahakamani pamoja na kuundiwa mahakama yao ya mafisadi? Utaona watanzania tunabebwa na vitu tunavyoamishwa na wanasiasa na wanatumia ujinga wetu kutuaminisha vitu, halafu wakiwa kwenye nafasi Na mamlaka ya kushughulikia huingia mitini.
 
Ukiona watu ambao walitakiwa kuwa upande wake kipindi hiki kigumu wanaruka jahazi elewa huyo mtu ni tatizo.

Na wale ambao anawategemea for his rescue wako kimya (jua huyo mtu ni taahira).

Binafsi siku zote nimekuwa nikisema Lissu sio solution; uwezo wake ni mdogo sana.

JF would make you believe otherwise, uhalisia ni kwamba hana uwezo.
Kama uwezo wa Lissu ni mdogo na sio solution, solution ni nini hasa?
1. Kumpinga risasi mchana kweupe, huku CCTV zikiwa zimeng’olewa na kamanda wa polisi kupiga picha ya kawaida ya gari na kuonyesha ndio lilihusika?

2. Kuzuia maslahi yake, Spika mpumbavu kudai hajui alipo Lissu na kudai ni mtoro hadi kuvuliwa ubunge?

3. Kuzuia uchunguzi wa tukio lake la kushambuliwa?

Wahusika wakuu wa huo unyama ni mizoga kwa sasa, solution imetoka mbinguni kabisa hiyo.
 
Kubwa zaidi ni kilaza (hana uwezo) kichwani.
Mwenzako aliaminiwa na shirika la umoja wa mataifa akateuliwa kuwa Mkurugenzi mkuu wa shirika la makazi kanda halafu wewe unamuita kilaza?

Anaweza kuwa na madhaifu mengine ila sio ukilaza.
 
binafsi Anna ni moja ya wale nisio weza kuwaelewa tangu ile pesa aseme tusiwaze sana ni ya mboga.
Kwenye ili andiko lake ameendelea kuthibitisha kitu kimoja wanapambania maisha yao kwanza nasii taifa
 
Ukiona watu ambao walitakiwa kuwa upande wake kipindi hiki kigumu wanaruka jahazi elewa huyo mtu ni tatizo.

Na wale ambao anawategemea for his rescue wako kimya (jua huyo mtu ni taahira).

Binafsi siku zote nimekuwa nikisema Lissu sio solution; uwezo wake ni mdogo sana.

JF would make you believe otherwise, uhalisia ni kwamba hana uwezo.
Umeulizwa, je hiyo inahalalisha apigwe risasi? Inazuia uchunguzi wa waliofanya unyama huo! Kamati aliyounda imetoa taarifa gani!

Job Ndugai alitangaza jimbo la Tundu Lissu lipo wazi tena kwa mbwembwe.
Job akamnyima fedha za matibabu na mafao yake.
Ndiyo maana tunasema, waliofaidika na hayo watamuona mwema sana, mbele ya Umma hana wema.

Job hakutenda haki kwa mambo mengi, hakulitendea haki Taifa! wasismsingizie Magufuli
 
Kama uwezo wa Lissu ni mdogo na sio solution, solution ni nini hasa?
1. Kumpinga risasi mchana kweupe, huku CCTV zikiwa zimeng’olewa na kamanda wa polisi kupiga picha ya kawaida ya gari na kuonyesha ndio lilihusika?

2. Kuzuia maslahi yake, Spika mpumbavu kudai hajui alipo Lissu na kudai ni mtoro hadi kuvuliwa ubunge?

3. Kuzuia uchunguzi wa tukio lake la kushambuliwa?

Wahusika wakuu wa huo unyama ni mizoga kwa sasa, solution imetoka mbinguni kabisa hiyo.
Subiri ruzuku iishe kama kuna chama.

Lema kesharuka CANADA na harudi tena.

Tanzania ina matatizo mengi na Lissu ain’t one.
 
binafsi Anna ni moja ya wale nisio weza kuwaelewa tangu ile pesa aseme tusiwaze sana ni ya mboga.
Kwenye ili andiko lake ameendelea kuthibitisha kitu kimoja wanapambania maisha yao kwanza nasii taifa
Ewaaah. 😂🤷🏿‍♂️
Na huo ndio Ukweli wenyewe !
Na ndio maana Bara hili litaendelea kuongoza kwa Umasikini Duniani 😳🙄 !
 
Spika Ndugai. Tunaokufahamu tunakulilia kwa WEMA WAKO. RIP. Familia. Poleni. Suala la Lissu kufukuzwa Bungeni liliniuma sana. Jioni nikamfuata Spika Ndugai nyumbani kwake Kisasa kumuuliza kulikoni? Mwenzetu wote tunajua yaliyompata?. Utasemaje hujui alipo?Spika akanieleza kwa utulivu yafuatayo ambayo IN HIS TRIBUTE (kama heshima kwake) ninayaweka wazi.

Labda yatasaidia kumuelewa kwa waliokerwa na kauli zake za mizaha (dry humor). Ndugai aliniambia "Mama ni Maelekezo. MimI nilichofanya kama Spika ni kujaribu kuokoa maisha yake kwa kumkimbiza Nairobi kutibiwa. Wengine walitaka apelekwe Muhimbili. Hatukuwa na bajeti. CHADEMA hawakuwa na fedha kulipia ndege.

Nikamuomba Mbunge wa CCM mhe Turku (RIP) alipie tutamrefund". Akaendelea "Mama Lissu ni mwanasiasa. Akipona atarejea kupambana kadri Mungu atakavyomjalia. Kwa sasa ninakuwa na tahadhari kusurvive katika siasa ngumu za maelekezo huku naongoza muhimili" .

Soma Pia: Job Ndugai, aliyewahi kuwa Spika wa Bunge afariki Dunia

Sikuwa na la kusema zaidi. Nikajua tuna safari ndefu kama taifa. Jamii haitaki kuangalia misingi ya matatizo yetu kimfumo. Tunabaki kulaumu viongozi (personalities) kana kwamba wana freedom kutekeleza majukumu yao. Mfano Utakuta mbunge analaumiwa kwa kutojenga shule, hospitali, barabara. Kwani hiyo si kazi ya Serikali kuu na Halmashauri wanaotoza kodi?

Tusimlaumu Ndugai kwa mambo yaliyokuwa ya mfumo. Alipokosea Mungu amsamehe lakini kuna mazuri Mengi alifanya. Apumzike kwa amani.

View attachment 3435096
Biblia inatufundisha mtu akitia mkono shambani kisha akaangalia nyuma hafai kwa ufalme wa Mungu,aheri angekubali kuacha cheo au kufa kwa ajili ya haki, ona sasa cheo bado anacho? au uhai anao? heri ufarakane na mtawala au binadamu yeyote kwa ajili ya kutenda jambo la haki la kumpendeza Mungu kuliko kuwa mnafki mwisho wako ni kwenye ziwa la moto.
 
Yeye kama Kiongozi huyo Ndugai kwakuwa alikuwa anaona kuwa yupo ktk serikali inayo ongozwa Kwa maelekezo na sio Kwa kufuata Sheria na katiba Alipaswa kujiweka kando ili Aweze kujisafisha na wananchi wasiweze kumuona kuwa yupo katika sehemu ya uovu

Kitendo Cha kuendelea kuitumia serikali Yenye matendo ya uovu na yeye akiwa ni sehemu ya serikali hiyo kama kiongozi mkuu wa muhimili tena akichangia Kwa kiasi kikubwa kikandamiza wengine

Hiyo twit ya Anna tibaijuka haiwezi kumsafisha Abadan
Kwa ujumla ukiukumbatia uovo wa mwingine nawe pia unakuwa mwovu,dawa pekee ni kujitenga siyo kujali maslahi yako binafsi.
 
Yeye kama Kiongozi huyo Ndugai kwakuwa alikuwa anaona kuwa yupo ktk serikali inayo ongozwa Kwa maelekezo na sio Kwa kufuata Sheria na katiba Alipaswa kujiweka kando ili Aweze kujisafisha na wananchi wasiweze kumuona kuwa yupo katika sehemu ya uovu

Kitendo Cha kuendelea kuitumia serikali Yenye matendo ya uovu na yeye akiwa ni sehemu ya serikali hiyo kama kiongozi mkuu wa muhimili tena akichangia Kwa kiasi kikubwa kikandamiza wengine

Hiyo twit ya Anna tibaijuka haiwezi kumsafisha Abadan
Wengi wachumia matumbo, hawana lolote la kuwasaidia watanzania. Wanajifanya wehu na vipofu ili mkate wao usiingie mchanga.
 
Spika Ndugai. Tunaokufahamu tunakulilia kwa WEMA WAKO. RIP. Familia. Poleni. Suala la Lissu kufukuzwa Bungeni liliniuma sana. Jioni nikamfuata Spika Ndugai nyumbani kwake Kisasa kumuuliza kulikoni? Mwenzetu wote tunajua yaliyompata?. Utasemaje hujui alipo?Spika akanieleza kwa utulivu yafuatayo ambayo IN HIS TRIBUTE (kama heshima kwake) ninayaweka wazi.

Labda yatasaidia kumuelewa kwa waliokerwa na kauli zake za mizaha (dry humor). Ndugai aliniambia "Mama ni Maelekezo. MimI nilichofanya kama Spika ni kujaribu kuokoa maisha yake kwa kumkimbiza Nairobi kutibiwa. Wengine walitaka apelekwe Muhimbili. Hatukuwa na bajeti. CHADEMA hawakuwa na fedha kulipia ndege.

Nikamuomba Mbunge wa CCM mhe Turku (RIP) alipie tutamrefund". Akaendelea "Mama Lissu ni mwanasiasa. Akipona atarejea kupambana kadri Mungu atakavyomjalia. Kwa sasa ninakuwa na tahadhari kusurvive katika siasa ngumu za maelekezo huku naongoza muhimili" .

Soma Pia: Job Ndugai, aliyewahi kuwa Spika wa Bunge afariki Dunia

Sikuwa na la kusema zaidi. Nikajua tuna safari ndefu kama taifa. Jamii haitaki kuangalia misingi ya matatizo yetu kimfumo. Tunabaki kulaumu viongozi (personalities) kana kwamba wana freedom kutekeleza majukumu yao. Mfano Utakuta mbunge analaumiwa kwa kutojenga shule, hospitali, barabara. Kwani hiyo si kazi ya Serikali kuu na Halmashauri wanaotoza kodi?

Tusimlaumu Ndugai kwa mambo yaliyokuwa ya mfumo. Alipokosea Mungu amsamehe lakini kuna mazuri Mengi alifanya. Apumzike kwa amani.

View attachment 3435096
Kama ni hivyo, anastahili kulaumiwa kwa kulidhalilisha bunge ambalo kazi yake ni kuisimamia na kuishauri serikali.Uliona wapi serilkali inatoa maagizo kwa bunge? Tunawalaumu cdm bure wanaposema kuna shida kwenye mifumo yetu
 
Ni mnafiki peke yake asiyejua Magufuli alivyoingilia mihimili yote kibabe. Muulize Pasco kilichomkuta baada ya kumuuliza swali kwa nini Rais anaiingilia mihimili mingine.
Pamoja na hizo za kina Rugemalira na Tibaijuka,ni nini kilimzuia Magufuli kuwafikisha mahakamani? Kwa nini aliamua kuwatesa tu kwa kuwaweka kizuizini bila ya kuwafikisha mahakamani ikiwa alikuwa na uhakika na ufisadi wao?
Ni kama tu scandal ya Hayati Lowasa,mtu akifikia mpaka kuhama chama na kusababisha Magufuli kuwa Rais wa kwanza kushinda kwa kura kiduchu tangu mfumo wa vya vingi uanze, mbona hakuwahi kufikishwa mahakamani pamoja na kuundiwa mahakama yao ya mafisadi? Utaona watanzania tunabebwa na vitu tunavyoamishwa na wanasiasa na wanatumia ujinga wetu kutuaminisha vitu, halafu wakiwa kwenye nafasi Na mamlaka ya kushughulikia huingia mitini.
Nipate muunganiko wa hoja yako kwanza ndiyo niweze kuchangia ninachokifahamu.

Je ufisadi wa Lowasa, ufisadi wa Rugemalila na Singasinga pamoja na kashifa ya mabillion ya Escrow ni habari za kusadikika na wivu wa kike kwa watu wasiopenda maendeleo ya wenzao?

Ukinifafanulia haya ndiyo nitaongea ninachokielewa.
 
Prof. Assad Aliwezaje kukiuka maagizo kutoka juu?? Uadilifu wake ulikuwa wapi akipokea maelekezo ya kutamka maneno ya kinyama dhidi ya TAL?? angekaa pembeni angekumbukwa kama shujaa. Anyway apumzike atakapo pokelewa. Sote njia yetu ni moja. Tujifunze kuthamini uhai/utu wa mtu mwingine
Tukikubali na kuelewa tetezi za aina hii basi kila mtu atajitetea ujinga. Mtu muadilifu yupo tayari kuachia cheo ili kulinda heshima yake na utu wake.

Kama Ndugai hakupenda kufanya hayo basi angegoma kupokea maelekezo ya kijinga na kama angetengenezewa mazingira magumu basi angeachia uspika kama alivyoachia alipopingana na huyu wa sasa.
​
 
Anna Tibaijuka

@AnnaTibaijuka.

Spika Ndugai. Tunaokufahamu tunakulilia kwa WEMA WAKO. RIP. Familia. Poleni. Suala la Lissu kufukuzwa Bungeni liliniuma sana. Jioni nikamfuata Spika Ndugai nyumbani kwake Kisasa kumuuliza kulikoni? Mwenzetu wote tunajua yaliyompata?.
Utasemaje hujui alipo? Spika akanieleza kwa utulivu yafuatayo ambayo IN HIS TRIBUTE (kama heshima kwake) ninayaweka wazi. Labda yatasaidia kumuelewa kwa waliokerwa na kauli zake za mizaha (dry humor).

Ndugai aliniambia "Mama ni Maelekezo. Mimi nilichofanya kama Spika ni kujaribu kuokoa maisha yake kwa kumkimbiza Nairobi kutibiwa. Wengine walitaka apelekwe Muhimbili. Hatukuwa na bajeti.
CHADEMA hawakuwa na fedha kulipia ndege. Nikamuomba Mbunge wa CCM mhe Turku (RIP) alipie tutamrefund". Akaendelea "Mama Lissu ni mwanasiasa. Akipona atarejea kupambana kadri Mungu atakavyomjalia. Kwa sasa ninakuwa na tahadhari kusurvive katika siasa ngumu za maelekezo huku naongoza muhimili".

Sikuwa na la kusema zaidi. Nikajua tuna safari ndefu kama taifa. Jamii haitaki kuangalia misingi ya matatizo yetu kimfumo. Tunabaki kulaumu viongozi (personalities) kana kwamba wana freedom kutekeleza majukumu yao. Mfano Utakuta mbunge analaumiwa kwa kutojenga shule, hospitali, barabara. Kwani hiyo si kazi ya Serikali kuu na Halmashauri wanaotoza kodi? Tusimlaumu Ndugai kwa mambo yaliyokuwa ya mfumo. Alipokosea Mungu amsamehe lakini kuna mazuri Mengi alifanya. Apumzike kwa amani.
Rugemalila team
 
Back
Top Bottom