Anna Tibaijuka: Ndugai aliniambia kwamba suala la Lissu ni “Maelekezo”

Anna Tibaijuka: Ndugai aliniambia kwamba suala la Lissu ni “Maelekezo”

Lisu alipigania raslimali za nchi hii kabla ya kuwa Rais. Magufuli alisubiri awe rais ndio ajifanye mzalendo. Yaani uzalendo kwake ulikuwa unaletwa na cheo cha urais. Baada ya kuwa rais akawa anataka ionekane yeye ndio mtanzania pekee anayepigania raslimali za nchi hii!
Umjui vizuri
 
Kiongozi anayejitetea kutofanya kitu sahihi kwa sababu ya "amri kutoka juu" ni mtu asiyeelewa uongozi ni nini. Hakutakiwa kuwa kiongo,i. Hana integrity wala strength of character.

Na huo si utetezi, ni kukubali makosa.
Halafu wanataka 'kukiri'' iwe ushujaa. Muhimu zaidi Ndugai aliyafanya mbele za Camera tena akijifaragua kwa dharau na kiburi. Ni mtu aliyechangia sana ubovu na hilo ni lake! hakuwa mtu mwema kwa Taifa, pengine alikuwa kwa marafiki. Ametukosea mambo mengi
 
Mzee Makamba: watu wazuri hawafi.
Watanganyika: 😲😔😡

Rais Samia: kifo ni kifo tu.
Watanganyika: 😯😔😡

Spika Tulia: Ndugai kafariki.
Watanganyika: 😂😅😆
 
Hii imeelezwa na Prof Tibaijuka katika Buriani yake kwa mwendazake Job Ndugai

Aiseee mengi tulikuwa tunadanganywa Kumbe na akina Mwamba

Rip Job Ndugai
"Kwamba Chadema hawakuwa na pesa yeye akamwambia Turfu amlipie"
Sasa huyu mama nae chenga yote hakuyasema leo ndo anasema wakati mtu keshasemwa sana alikuwa wapi kumtetea?

Huyu si ndo yule wa bil pesa ya mboga!
Wanasiasa kujua yupi mkweli na kwa wakati gani ni ngumu.
 
stori ya huyo mbunge aliyetoa pesa ya muda
 
Uzuri wa nchi yetu mataahira yako mengi na huku mitandaoni ndiyo yamejazana. Muovu mmoja, kwa maslahi yake binafsi anaweza kuiaminisha jamii kuwa yeye ni mwema na majority wakamuamini. Tofauti ya huyu Profesa na Polepole ni jinsia tu. Alipokea gawio la TZS 1.6B, huku akituambia kuwa ni tuhela za mboga tu. Leo yeye anataka tumuone mwem? Ni wote ni miongoni mwa wahuni tu.
 
Spika Ndugai. Tunaokufahamu tunakulilia kwa WEMA WAKO. RIP. Familia. Poleni. Suala la Lissu kufukuzwa Bungeni liliniuma sana. Jioni nikamfuata Spika Ndugai nyumbani kwake Kisasa kumuuliza kulikoni? Mwenzetu wote tunajua yaliyompata?. Utasemaje hujui alipo?Spika akanieleza kwa utulivu yafuatayo ambayo IN HIS TRIBUTE (kama heshima kwake) ninayaweka wazi.

Labda yatasaidia kumuelewa kwa waliokerwa na kauli zake za mizaha (dry humor). Ndugai aliniambia "Mama ni Maelekezo. MimI nilichofanya kama Spika ni kujaribu kuokoa maisha yake kwa kumkimbiza Nairobi kutibiwa. Wengine walitaka apelekwe Muhimbili. Hatukuwa na bajeti. CHADEMA hawakuwa na fedha kulipia ndege.

Nikamuomba Mbunge wa CCM mhe Turku (RIP) alipie tutamrefund". Akaendelea "Mama Lissu ni mwanasiasa. Akipona atarejea kupambana kadri Mungu atakavyomjalia. Kwa sasa ninakuwa na tahadhari kusurvive katika siasa ngumu za maelekezo huku naongoza muhimili" .

Soma Pia: Job Ndugai, aliyewahi kuwa Spika wa Bunge afariki Dunia

Sikuwa na la kusema zaidi. Nikajua tuna safari ndefu kama taifa. Jamii haitaki kuangalia misingi ya matatizo yetu kimfumo. Tunabaki kulaumu viongozi (personalities) kana kwamba wana freedom kutekeleza majukumu yao. Mfano Utakuta mbunge analaumiwa kwa kutojenga shule, hospitali, barabara. Kwani hiyo si kazi ya Serikali kuu na Halmashauri wanaotoza kodi?

Tusimlaumu Ndugai kwa mambo yaliyokuwa ya mfumo. Alipokosea Mungu amsamehe lakini kuna mazuri Mengi alifanya. Apumzike kwa amani.

View attachment 3435096
Ulikuwa wapi kuyasema akiwa hai?

Kwanini marehemu hakuyasema akiwa hai?

Acheni siasa.kwenye misiba. Kifo ni kifo tu
 
Mama hatujakuelewa umefumbafumba tu ukweli upo palepale hushangai. Hata wale wa nyumbani kwake wanafurahia utamsafishaje hapo
 
Allegedly, Tibaijuka hawezi msamehe Magufuli sababu za Rugemalila kuwekwa jela.

Anaweza mtungia uongo wowote bila ya ushahidi wa kuthibitisha.
Sio sawa kabisa kusema maneno muda ambao wahusika wote wawili ni marehemu. Huu ni unafiki wa kupitiliza hawa watu waogopwe na wafungwe midogo. Katika akili ya kawaida Ndungai asingweza kusema hivyo direct japo kuwa kila mtu anajuwa ukweli wa lile jambo.
 
Tabia za wanafiki zinafanana ni kutumia mazingira kuhalalisha uongo wao.

Tibaijuka na mama hovyo, sasa siwezi kukuamisha kumuona for what she actually is (her true colours).

Kubwa zaidi ni kilaza (hana uwezo) kichwani.
 
Yeye kama Kiongozi huyo Ndugai kwakuwa alikuwa anaona kuwa yupo ktk serikali inayo ongozwa Kwa maelekezo na sio Kwa kufuata Sheria na katiba Alipaswa kujiweka kando ili Aweze kujisafisha na wananchi wasiweze kumuona kuwa yupo katika sehemu ya uovu

Kitendo Cha kuendelea kuitumia serikali Yenye matendo ya uovu na yeye akiwa ni sehemu ya serikali hiyo kama kiongozi mkuu wa muhimili tena akichangia Kwa kiasi kikubwa kikandamiza wengine

Hiyo twit ya Anna tibaijuka haiwezi kumsafisha Abadan
Ref to comment #7!

Jamaa kaifunga mada na wewe umekuja kuweka cement kuikamilisha!

Maneno yanayotoka katika kinywa cha Anna Tibaijuka(mama wa 'hela ya mboga') fisadi aliyevuna mgao wa mabillion ya Escrow, kutoka kwa mhaya mwenzake Fisadi Rugemalila, kamwe hawezi kuwa na kauli ya kumpamba Magufuli.

Si mtu wa kumwamini kwa chochote kutokana na kauli zake tata anazozitoa kila mara apatapo nafasi ya kufanya hivyo.

Lengo lake ni kuipoka saikolojia ya jamii aonekane kuwa yeye ni 'mtu safi' asiye na mawaa katika jamii, wakati mikono yake inanuka ufisadi uliopitiliza!

Mimi hata ule muda wa kumsikiliza huwa sina.
 
Allegedly, Tibaijuka hawezi msamehe Magufuli sababu za Rugemalila kuwekwa jela.

Anaweza mtungia uongo wowote bila ya ushahidi wa kuthibitisha.
Hayo bila hata Profesa Tibaijuka kuyasema, wenye akili tulijua yote yaliyompata Lisu yalikuwa maelekezo kutoka kwa Magufuli,na ndio kisa cha kuzuia hata polisi kufanya uchunguzi wa unyama ule.
 
Hayo bila hata Profesa Tibaijuka kuyasema, wenye akili tulijua yote yaliyompata Lisu yalikuwa maelekezo kutoka kwa Magufuli,na ndio kisa cha kuzuia hata polisi kufanya uchunguzi wa unyama ule.
Ukiona watu ambao walitakiwa kuwa upande wake kipindi hiki kigumu wanaruka jahazi elewa huyo mtu ni tatizo.

Na wale ambao anawategemea for his rescue wako kimya (jua huyo mtu ni taahira).

Binafsi siku zote nimekuwa nikisema Lissu sio solution; uwezo wake ni mdogo sana.

JF would make you believe otherwise, uhalisia ni kwamba hana uwezo.
 
Back
Top Bottom