Anna Tibaijuka: Ndugai aliniambia kwamba suala la Lissu ni “Maelekezo”

Anna Tibaijuka: Ndugai aliniambia kwamba suala la Lissu ni “Maelekezo”

Wapi ww, uzalendo wa cheo sio uzalendo. Kuitwa bulldozer ndio sifa ya kuwa rais? Lisu hajasubiri urais ndii aonyeshe uzalendo wake.
Uzalendo hal8si ni yule aliye mzalendo hata baada ya kuoata mamlaka tumia akili wacha kuwa na uanithi wa akili wengi ubadilika baada ya kupata vyeo au urais
 
Prof. Assad Aliwezaje kukiuka maagizo kutoka juu?? Uadilifu wake ulikuwa wapi akipokea maelekezo ya kutamka maneno ya kinyama dhidi ya TAL?? angekaa pembeni angekumbukwa kama shujaa. Anyway apumzike atakapo pokelewa. Sote njia yetu ni moja. Tujifunze kuthamini uhai/utu wa mtu mwingine
Prof Assad kwenye interview moja alisema aliwahi kushangaa wamefika watu wanamwambia fuata maelekezo ukishindwa tuko na watu wetu nje hapo hatushindwi kuwaleta na kukutoa.

Aliishia tu kusema mkubwa mmoja hakumtaja jina.

Ni ngumu kufanya kazi kwa weledi na ukiwa una uwezo mkubwa kwenye jamii yenye wajinga wengi na udikteta.
 
Prof Assad kwenye interview moja alisema aliwahi kushangaa wamefika watu wanamwambia fuata maelekezo ukishindwa tuko na watu wetu nje hapo hatushindwi kuwaleta na kukutoa.
Mwisho wa siku hakufuata maelekezo na alitoka. Hii ndio maana halisi ya uadilifu. Kuna watu kwao madaraka/pesa ni bora kuliko utu wao, watu wa dizaini hiyo huwezi kuta wanafikiria watu wengine maana yeye binafsi bila cheo fulani anajiona hajakamilika na yuko radhi kufanya lolote hata kutweza utu wake binafsi ilimradi abaki/apate cheo.
 
Mwisho wa siku hakufuata maelekezo na alitoka. Hii ndio maana halisi ya uadilifu. Kuna watu kwao madaraka/pesa ni bora kuliko utu wao, watu wa dizaini hiyo huwezi kuta wanafikiria watu wengine maana yeye binafsi bila cheo fulani anajiona hajakamilika na yuko radhi kufanya lolote hata kutweza utu wake binafsi ilimradi abaki/apate cheo.
Naam katika hili Prof nilimpongeza kwa kukataa udikteta uchwara.

Hadi sasa najiuliza CCM kwanini hawaoni umuhimu wa katiba mpya maana Magufuli alituonyesha ubovu wa katiba hii na hakuna aliyeweza kudeal nae walau Lissu pekee ndio alisimama nae toe to toe.

Walichekelea wapinzani walivyoumizwa hadi pale alipoanza kudeal na kina Nape, Kinana, Membe na Makamba.
 
Uzalendo hal8si ni yule aliye mzalendo hata baada ya kuoata mamlaka tumia akili wacha kuwa na uanithi wa akili wengi ubadilika baada ya kupata vyeo au urais
Kwahiyo huwezi kuwa mzalendo ama kuonyesha uzalendo wako hadi upate madaraka?
 
Spika Ndugai. Tunaokufahamu tunakulilia kwa WEMA WAKO. RIP. Familia. Poleni. Suala la Lissu kufukuzwa Bungeni liliniuma sana. Jioni nikamfuata Spika Ndugai nyumbani kwake Kisasa kumuuliza kulikoni? Mwenzetu wote tunajua yaliyompata?. Utasemaje hujui alipo?Spika akanieleza kwa utulivu yafuatayo ambayo IN HIS TRIBUTE (kama heshima kwake) ninayaweka wazi.

Labda yatasaidia kumuelewa kwa waliokerwa na kauli zake za mizaha (dry humor). Ndugai aliniambia "Mama ni Maelekezo. MimI nilichofanya kama Spika ni kujaribu kuokoa maisha yake kwa kumkimbiza Nairobi kutibiwa. Wengine walitaka apelekwe Muhimbili. Hatukuwa na bajeti. CHADEMA hawakuwa na fedha kulipia ndege.

Nikamuomba Mbunge wa CCM mhe Turku (RIP) alipie tutamrefund". Akaendelea "Mama Lissu ni mwanasiasa. Akipona atarejea kupambana kadri Mungu atakavyomjalia. Kwa sasa ninakuwa na tahadhari kusurvive katika siasa ngumu za maelekezo huku naongoza muhimili" .

Soma Pia: Job Ndugai, aliyewahi kuwa Spika wa Bunge afariki Dunia

Sikuwa na la kusema zaidi. Nikajua tuna safari ndefu kama taifa. Jamii haitaki kuangalia misingi ya matatizo yetu kimfumo. Tunabaki kulaumu viongozi (personalities) kana kwamba wana freedom kutekeleza majukumu yao. Mfano Utakuta mbunge analaumiwa kwa kutojenga shule, hospitali, barabara. Kwani hiyo si kazi ya Serikali kuu na Halmashauri wanaotoza kodi?

Tusimlaumu Ndugai kwa mambo yaliyokuwa ya mfumo. Alipokosea Mungu amsamehe lakini kuna mazuri Mengi alifanya. Apumzike kwa amani.

View attachment 3435096
Hii kauli ya huyu mama makes very big sense...

1. Na hapa ndipo ushauri wa Askofu Josephat Gwajima alioutoa ktk Press Conference yake na kusababisha kanisa lake kufutiwa usajili kiharamia tu unapopata nguvu na maana. KATIBA MPYA inayolinda maadili ya uongozi..!!

2. Askofu Gwajima alitoa ushauri kuwa wakuu wa vyombo vya dola, mihimili ya dola Bunge na Mahakama; taasisi muhimu kama TAKUKURU, Msajili wa vyama vya siasa, Tume ya Uchaguzi nk kulindwa na sheria na katiba ili kazi zao ziwe secured na tishio la kutenguliwa teuzi zao pale wanapokuwa hawakubaliani na mteuzi (Rais) wanaposimamia maamuzi yao ndani ya taasisi zao kwa mujibu wa sheria na katiba...

3. Ni obvious kuwa, Spika Ndugai kwa maelekezo haya ya kishetani angeweza kuyakataa kabisa. Lakini kwa upande mwingine alipoangalia ufahari na marupurupu ya mapesa ya Uspika, akaona heri kuikanyaga HAKI na badala yake akamsujudia shetani ibilisi na uovu wake....

4. Ndiyo kusema sasa kuwa, kanuni ya asili (natural principle) haitoi excuse kwa kukubaliana na kushiriki kutenda dhambi ile ya jaribio la kutoa uhai wa Tundu Lissu....

5. Utetezi wake Spika Ndugai ulikuwa very genuine kibinadamu, lakini pia alikuwa na option ya kukataa na kisha kujiuzulu Uspika kama ishara ya kutokukubaliana na mipango ile miovu..

6. Kama angefanya hivi, angejijengea heshima kubwa sana kwa wanadamu na zaidi kwa Mungu na huyu Mungu asingemtupa kamwe...

7. Unfortunately, he took very wrong decisions na haya yote yaliyomtokea baadae na yanayotokea sasa ikiwemo kifo chake, watu kushangilia badala ya kuhuzunika ni matokeo ya dhambi ile mbaya kabisa...

8. Wote tuna dhambi, hilo halina ubishi. Lakini tofauti ya kila mmoja wetu sisi ktk dhambi zetu, ni namna tunavyofanya timing ya kuzitubu haraka kabla hazijaanza kutuletea madhara (hukumu)...!!
 
Hatuwezi kuamini huo usanii wenu kwa sasa maana hata ndugai mwenyewe hayupo na hajitetei..
Twaweza amini vp kwa sasa?
Huo nao n4 umakolo!
 
Kwahiyo huwezi kuwa mzalendo ama kuonyesha uzalendo wako hadi upate madaraka?
Tumiq akili wewe pimbi ukijifunua tu wahalifu wakina Rostam azizi na wenzie wanakumaliza .....tatizo lako una akili za kuchezea rede na dada zako siyo akili za kijiniasi kuelewa mambo ...wewe ujui kuwa wahalifu wa kiserikali awataki kabisa kumwona mzalendo na adui yao no 1 ni WAZALENDO
 
Kweli Mkuu, haka ka mama sijui ni kachawi?!
Kameona jamaa hayupo, ndo kanakuja na uzushi ili kumchafua hayati JPM.
Allegedly, Tibaijuka hawezi msamehe Magufuli sababu za Rugemalila kuwekwa jela.

Anaweza mtungia uongo wowote bila ya ushahidi wa kuthibitisha.
 
ILIPASWA AYASEME HAYA KABLA YA HUYO MWEHU KUFA !


TOFAUTI NA HAPO HUYO NAYE NDO WALEWALE !
Kama wewe na uanaume wako umeshindwa kupigania katiba na tume huru....then unataka mwanamke afe kisa kusema ukweli?
 
Ila Prof Tibaijuka ni mchonganishi sana kumbe ni WA HOVYO kiasi hiki.
 
Back
Top Bottom