Anna Tibaijuka: Ndugai aliniambia kwamba suala la Lissu ni “Maelekezo”

Anna Tibaijuka: Ndugai aliniambia kwamba suala la Lissu ni “Maelekezo”

@Paschalmayala aliyeitwa na bungeni na Ndugai kwa kuandika kuwa bunge analoliongoza si huru.
 
Lisu alipigania raslimali za nchi hii kabla ya kuwa Rais. Magufuli alisubiri awe rais ndio ajifanye mzalendo. Yaani uzalendo kwake ulikuwa unaletwa na cheo cha urais. Baada ya kuwa rais akawa anataka ionekane yeye ndio mtanzania pekee anayepigania raslimali za nchi hii!
Magufuli unajua kwanini aliitwa bulldozer? Tumia akili JPM alijificha asijulikane kuwa ni mzalendo maana wangejua hivyo wasinge mkubali ...
 
Na kusema toa njee Mnyika nisimuone hapa mpaka wiki ijayo
Toa nje Tundu Lissu
Chezea mtu yoyote ila siyo Ndugai.
Ni maelekezo ya nani?
Watanzania wengi siyo reliable....Leo watasema hili na lile but most of the times wengi wakipewa uongozi huwa hawatumii akili zao Wana read minds za leader na kutaka kumfurahisha hata kwakuakanyaga haki za wengine...Hakuna taifa la hivyo kama letu hasa inapokuja kusimamia haki za watu..
 
Wabongo kudai haki zetu wenyewe hatuwezi hata wale wanaojitoa muhanga kwa ajiri yetu pia huwa tunawaacha wenyewe wapambane na hali zao. Ila sasa tunaishia kulaani, kuhukumu, kuombea wengine vifo na kufurahia.

Hayo mambo hayana msaada wa kubadili chochote.
 
Kama alishindwa kujiuzuru Kipindi kile..I wonder what did it take to step down later.
 
Yeye kama Kiongozi huyo Ndugai kwakuwa alikuwa anaona kuwa yupo ktk serikali inayo ongozwa Kwa maelekezo na sio Kwa kufuata Sheria na katiba Alipaswa kujiweka kando ili Aweze kujisafisha na wananchi wasiweze kumuona kuwa yupo katika sehemu ya uovu

Kitendo Cha kuendelea kuitumia serikali Yenye matendo ya uovu na yeye akiwa ni sehemu ya serikali hiyo kama kiongozi mkuu wa muhimili tena akichangia Kwa kiasi kikubwa kikandamiza wengine

Hiyo twit ya Anna tibaijuka haiwezi kumsafisha Abadan
Labda Ndugai Alikuwa Analipia GHARAMA za matibabu Na Pia yawezena kulikuwa na UGAIDI wa kifamilia dhidi yake.

Mungu ndiye Mjuzi Wa Yote

Yesu Alisema "Usihukumu......."
 
Kila mtu atabeba furushi lake siku ya hukumpa hapatakuwa na utetezi eti ulielekezwa
 
Spika Ndugai. Tunaokufahamu tunakulilia kwa WEMA WAKO. RIP. Familia. Poleni. Suala la Lissu kufukuzwa Bungeni liliniuma sana. Jioni nikamfuata Spika Ndugai nyumbani kwake Kisasa kumuuliza kulikoni? Mwenzetu wote tunajua yaliyompata?. Utasemaje hujui alipo?Spika akanieleza kwa utulivu yafuatayo ambayo IN HIS TRIBUTE (kama heshima kwake) ninayaweka wazi.

Labda yatasaidia kumuelewa kwa waliokerwa na kauli zake za mizaha (dry humor). Ndugai aliniambia "Mama ni Maelekezo. MimI nilichofanya kama Spika ni kujaribu kuokoa maisha yake kwa kumkimbiza Nairobi kutibiwa. Wengine walitaka apelekwe Muhimbili. Hatukuwa na bajeti. CHADEMA hawakuwa na fedha kulipia ndege.

Nikamuomba Mbunge wa CCM mhe Turku (RIP) alipie tutamrefund". Akaendelea "Mama Lissu ni mwanasiasa. Akipona atarejea kupambana kadri Mungu atakavyomjalia. Kwa sasa ninakuwa na tahadhari kusurvive katika siasa ngumu za maelekezo huku naongoza muhimili" .

Soma Pia: Job Ndugai, aliyewahi kuwa Spika wa Bunge afariki Dunia

Sikuwa na la kusema zaidi. Nikajua tuna safari ndefu kama taifa. Jamii haitaki kuangalia misingi ya matatizo yetu kimfumo. Tunabaki kulaumu viongozi (personalities) kana kwamba wana freedom kutekeleza majukumu yao. Mfano Utakuta mbunge analaumiwa kwa kutojenga shule, hospitali, barabara. Kwani hiyo si kazi ya Serikali kuu na Halmashauri wanaotoza kodi?

Tusimlaumu Ndugai kwa mambo yaliyokuwa ya mfumo. Alipokosea Mungu amsamehe lakini kuna mazuri Mengi alifanya. Apumzike kwa amani.

View attachment 3435096
Mama Anna TIBAIJUKA ni mnafiki wa hali ya juu.

Kama Job Ndugai hakushiriki kummshambulia Tundu kwa nini aliendelea kukataa kumlipa mafao yake ya ubunge hata baada ya Magufuli kuwa amefariki?

I will not subscribe to this logical fallacy
 
Ukitaka kuishi VIZURI na KUWA na MAHUSIANO MeMA na MUNGU WAKO FANYA TU HIVI. Kaa mbali na mwanasiasa pamoja na mfanya BIASHARA mwenye NDOTO KUBWA. Zaidi ya HAPO nikudanganya WATU una moyo safi kumbe waaapi



Kwishaaa
 
Magufuli unajua kwanini aliitwa bulldozer? Tumia akili JPM alijificha asijulikane kuwa ni mzalendo maana wangejua hivyo wasinge mkubali ...
Wapi ww, uzalendo wa cheo sio uzalendo. Kuitwa bulldozer ndio sifa ya kuwa rais? Lisu hajasubiri urais ndii aonyeshe uzalendo wake.
 
Kwa taarifa yako: Lissu alipokuwa anakimbizwa Nairobi wengi hawakuwa wamejua ni nini hasa kinaendelea na aliyetuma auawe alikuwa hajui kama itafikia hatua ya kukimbizwa hospital hivyo hakuwa ameandaa mkakati wa kukataza watu wasimkimbize hopaital. Yaani ni hivi: Magu alivyopanga ni kuwa alikuwa na uhakika Lissu atauawa pale pale. Hivyo basi hakuwa ameandaa mkakati wowote wa kuhakikisha hafikishwi hospital tena Nairobi. Kwa hiyo unaweza kusema kabisa kama angekuwa amepewa amri kabla kuwa asitoe msaada wowote wa kumpeleka hospital basi angetii.
Sijui kwanini Ndugai alifanya alichofanya kwa TAL akiwa spika na sijui kama Tibaijuka anasema kweli au la.

Ila najua kwamba tukio la TAL ni moja ya miujiza ya kipekee niliyowahi shuhudia.

Ndo maana nikasema, wa kumhukumu wamhukumu, wanaomjua kwa wema wake waomboleze kwa jina lake.
 
Spika Ndugai. Tunaokufahamu tunakulilia kwa WEMA WAKO. RIP. Familia. Poleni. Suala la Lissu kufukuzwa Bungeni liliniuma sana. Jioni nikamfuata Spika Ndugai nyumbani kwake Kisasa kumuuliza kulikoni? Mwenzetu wote tunajua yaliyompata?. Utasemaje hujui alipo?Spika akanieleza kwa utulivu yafuatayo ambayo IN HIS TRIBUTE (kama heshima kwake) ninayaweka wazi.

Labda yatasaidia kumuelewa kwa waliokerwa na kauli zake za mizaha (dry humor). Ndugai aliniambia "Mama ni Maelekezo. MimI nilichofanya kama Spika ni kujaribu kuokoa maisha yake kwa kumkimbiza Nairobi kutibiwa. Wengine walitaka apelekwe Muhimbili. Hatukuwa na bajeti. CHADEMA hawakuwa na fedha kulipia ndege.

Nikamuomba Mbunge wa CCM mhe Turku (RIP) alipie tutamrefund". Akaendelea "Mama Lissu ni mwanasiasa. Akipona atarejea kupambana kadri Mungu atakavyomjalia. Kwa sasa ninakuwa na tahadhari kusurvive katika siasa ngumu za maelekezo huku naongoza muhimili" .

Soma Pia: Job Ndugai, aliyewahi kuwa Spika wa Bunge afariki Dunia

Sikuwa na la kusema zaidi. Nikajua tuna safari ndefu kama taifa. Jamii haitaki kuangalia misingi ya matatizo yetu kimfumo. Tunabaki kulaumu viongozi (personalities) kana kwamba wana freedom kutekeleza majukumu yao. Mfano Utakuta mbunge analaumiwa kwa kutojenga shule, hospitali, barabara. Kwani hiyo si kazi ya Serikali kuu na Halmashauri wanaotoza kodi?

Tusimlaumu Ndugai kwa mambo yaliyokuwa ya mfumo. Alipokosea Mungu amsamehe lakini kuna mazuri Mengi alifanya. Apumzike kwa amani.

View attachment 3435096
Mbona hakusema kabla?
 
Tibaijuka atuambie anaipataje twitter/X au yuko nje ya mipaka ya Tanzania?
 
Back
Top Bottom