Anne Makinda awataka vijana kujitafutia ajira

Anne Makinda awataka vijana kujitafutia ajira

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Kamisaa wa Sensa Kitaifa, Anna Makinda amewataka vijana wasomi kujitengenezea uchumi wao binafsi kupitia fursa zilizoko kwenye maeneo wanayoishi kuliko kutegemea ajira kutoka Serikalini au sekta binafsi.

Akizungumza leo Oktoba 12 na Kamati ya sensa katika kikao cha kutathimini sensa kwa Mkoa wa Arusha, Makinda ambaye pia ni Spika mstaafu, amesema kuwa takwimu hizo ni muhimu kwa nchi kwenda kutengeneza mfumo mzima katika hatua zake za kusaidia jamii hasa kiuchumi.

“Lipo jambo kubwa nililoliona nalo ni kundi kubwa la vijana ambao hawana ajira wala hawajishughulishi na kazi yoyote ya kujiingizia kipato na ukimuuliza anasema amehitimu elimu fulani anasubiri ajira, jamani hili la kuajiriwa mtachelewa sana,” amesema Makinda

Amesema kuwa tatizo la ajira linalotupiwa serikali linaweza kutatulika na muhusika mwenyewe kwa kutazama changamoto zilizoko hata katika jamii na kuliwekea ubunifu mzuri na kuwa fursa ya ajira au kujipatia kipato kuliko kusubiri kuajiriwa.

“Mfano mzuri serikali kwa sasa inetengeneza fursa nzuri kwenye sekta ya kilimo na uzuri nchi yetu ina maeneo mengi wazi, lakini utakuta kijana msomi anasema anasubiri kuajiriwa badala atumie fursa kutengeneza ajira, nawaambia hao sio wasomi wazuri ambao Taifa linaweza kuwategemea,” amesema.

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela amesema kuwa jumla ya kaya 2,724 zilihesabiwa katika vitongoji 1,506 na kazi ilifanikiwa kwa asilimia 99.99.

“Kwenye kazi hii serikali ilitupatia kiasi cha Sh5.9 bilioni na tumefanikisha kazi hiyo na vifaa vyote tulivyokabidhiwa tumerudisha kasoro vishwambi vitano ambavyo vilipotea, lakini jeshi la polisi vinaendelea na kazi ya kuvipeleleza vipatikane,” amesema.
 
Kuna muda ni bora kukaa kimya kuliko kuonesha ni ujinga kiasi gani ulionao kichwani.
Ni lini huyo Mzungumzaji amewahi kuwa na Akili? Mmoja wa Wanafamilia wake (Mwanamke) mwaka 2011 tukiwa Mbezi Beach Maguruwe (wakati Nduguye akiwa Boss Mkuu Bungeni) aliniambia kuwa hakuna Watu anaowachukia na asiowapenda kama Wanaume hivyo kuanzia hapo nami nikaanza Kumpuuza na Kumdharau hadi hivi leo kwani nilijua kuwa tayari "zimeshafyatuka' Kichwani.
 
huyu mama amekuwa kwenye ajira tangu apate akili hadi leo, mbona hakutoka ili akajiajiri?
Ana Hoja ya Msingi juu ya Vijana Kujiajiri na ni Jambo jema ila kwa bahati mbaya ni kwamba hawa Viongozi Waandamizi wanachokosea ni Uwasilishaji wao tu wa hili Jambo kwani wanaliwasilisha 'Kimasimango' zaidi na siyo 'Kistaha' hivyo kujikuta wanapata Mrejesho ya Matusi na Jazba kutoka kwa hao Vijana wasio na Kazi (Ajira) ambao ni Wengi sana.
 
Kama ingekua rahisi angeacha hiko cheo alichonacho afanye mishe zake binafsi. Kwanza yeye si mbunge toka 1975 then akawa naibu spika to spika from 2005 to 2015. Si ashapata mtaji wa kutosha, huyu mama anakatwa na majobless.

Sometimes hawa watu wanataka watukanwe vijana tuonekane hatuna nidhamu.
 
Ni kweli huwa wanayatafuta Wenyewe 'Matusi' ya Kutukuka kutoka kwa Vijana wengi wasio na Ajira ( Kazi ) hivyo wawe makini na Kauli zao na ikiwezekana wawe Wanazipima Kwanza kabla ya Kukurupuka kuzitoa.
 
Sijui hata yeye alijiajiri?

Wasomi wa Tanzania walipofikia wanatoa maneno ya kuudhi kabisa, suluhisho vijana wengi hawana shida na ajira zenu mlizojimilikisha kama ukoo huko serikalini,

Ni mtaji tu ndiyo suluhisho basi tupeni mitaji mtaona kama tutalilia vijinafasi huko serikalini kwenu
 
Serikali ndiyo yenye jukumu la kutengeneza ajira.
Serikali haitengenezi Ajira isipokuwa inaweka Sera nzuri ambazo zitachochea Uwekezaji ambako huko kunaweza kupatikana Ajira nyingi za Kutosha.

Hata hivyo kwa wale Vijana ambao huwa wanapata Fursa za Ajira ( Kazi ) wawe wanajitahidi sana 'Kusevu' Pesa wazipatazo ili hata kama baadae wakikosa Kazi ( Ajira ) basi hizo Pesa walizonazo waweze kuzitumia kama Mtaji wa Kujiajiri.

Na kwa Vijana ambao hawana Ajira ( Kazi ) ambao ni Kundi Kubwa wajifunze kufanya Kazi za Kujitokea ( Volunteering ) katika Taasisi mbalimbali ili kujifunza na hata kupata Uzoefu ili iwarahisishie kuboresha Ufanisi wao na hata kupata Ajira kiurahisi.

Mitaala ya Elimu yetu Tanzania ibadilishwe na Elimu ya Tanzania sasa iwe ni ya Vocational and Research Based na siyo hii ya Kikoloni tuliyonayo ambayo inatengeneza Kundi Kubwa la Wasubiri Ajira za Kuajiriwa na siyo Watengeneza Ajira ( wa Kujiajiri Wenyewe )

Mwisho kwakuwa Tanzania kwa 85% ni Nchi ya Kilimo na bado naambiwa 75% ya Ardhi ya Tanzania ipo tu haitumiki Serikali ijikite hasa katika Kuboresha Sekta ya Kilimo, Kufundisha Vijana Ujasiriamali wa Kilimo na kuifanya Sekta hii kuwa Rafiki na Rahisi ili Kuvutia Vijana wengi na wakianza Kilimo ( Kulima ) itawapatia Kipato kikubwa na kusahau Kusubiri Kazi ( Ajira ) za Serikalini.
 
Kujiajiri ni jambo jema sana kwa maslahi binafsi na ya nchi
Makinda anajua hilo pia pamoja na kwamba yeye mwenyewe hajui kutafuta ajira, hajawahi kutafuta ajira. Amekua mtu wa kupewa ajira kwa kupendekezwa na kuteuliwa tangu akiwa binti mdogo hadi leo

Nadhani sasa kupitia uzoefu wake na alichokiona kwenye sensa amsaidie kijana wa kitanzania kwa kumwekea mifumo na miongozo itakayomsaidia kumjengea uwezo na ari ya kujiajiri kupitia mazingira anayoishi na changamoto mbalimbali
 
Serikali haitengenezi Ajira isipokuwa inaweka Sera nzuri ambazo zitachochea Uwekezaji ambako huko kunaweza kupatikana Ajira nyingi za Kutosha.

Hata hivyo kwa wale Vijana ambao huwa wanapata Fursa za Ajira ( Kazi ) wawe wanajitahidi sana 'Kusevu' Pesa wazipatazo ili hata kama baadae wakikosa Kazi ( Ajira ) basi hizo Pesa walizonazo waweze kuzitumia kama Mtaji wa Kujiajiri.

Na kwa Vijana ambao hawana Ajira ( Kazi ) ambao ni Kundi Kubwa wajifunze kufanya Kazi za Kujitokea ( Volunteering ) katika Taasisi mbalimbali ili kujifunza na hata kupata Uzoefu ili iwarahisishie kuboresha Ufanisi wao na hata kupata Ajira kiurahisi.

Mitaala ya Elimu yetu Tanzania ibadilishwe na Elimu ya Tanzania sasa iwe ni ya Vocational and Research Based na siyo hii ya Kikoloni tuliyonayo ambayo inatengeneza Kundi Kubwa la Wasubiri Ajira za Kuajiriwa na siyo Watengeneza Ajira ( wa Kujiajiri Wenyewe )

Mwisho kwakuwa Tanzania kwa 85% ni Nchi ya Kilimo na bado naambiwa 75% ya Ardhi ya Tanzania ipo tu haitumiki Serikali ijikite hasa katika Kuboresha Sekta ya Kilimo, Kufundisha Vijana Ujasiriamali wa Kilimo na kuifanya Sekta hii kuwa Rafiki na Rahisi ili Kuvutia Vijana wengi na wakianza Kilimo ( Kulima ) itawapatia Kipato kikubwa na kusahau Kusubiri Kazi ( Ajira ) za Serikalini.
Kuweka huko mazingira ndiko kutengeneza ajira. Kwenye kutengeneza ajira, hata ya mtu kujiajiri serikali inaplay zaidi ya asilimia 70.
 
Back
Top Bottom