Anne Makinda awataka vijana kujitafutia ajira

Anne Makinda awataka vijana kujitafutia ajira

Kamisaa wa Sensa Kitaifa, Anna Makinda amewataka vijana wasomi kujitengenezea uchumi wao binafsi kupitia fursa zilizoko kwenye maeneo wanayoishi kuliko kutegemea ajira kutoka Serikalini au sekta binafsi.

Akizungumza leo Oktoba 12 na Kamati ya sensa katika kikao cha kutathimini sensa kwa Mkoa wa Arusha, Makinda ambaye pia ni Spika mstaafu, amesema kuwa takwimu hizo ni muhimu kwa nchi kwenda kutengeneza mfumo mzima katika hatua zake za kusaidia jamii hasa kiuchumi.

“Lipo jambo kubwa nililoliona nalo ni kundi kubwa la vijana ambao hawana ajira wala hawajishughulishi na kazi yoyote ya kujiingizia kipato na ukimuuliza anasema amehitimu elimu fulani anasubiri ajira, jamani hili la kuajiriwa mtachelewa sana,” amesema Makinda

Amesema kuwa tatizo la ajira linalotupiwa serikali linaweza kutatulika na muhusika mwenyewe kwa kutazama changamoto zilizoko hata katika jamii na kuliwekea ubunifu mzuri na kuwa fursa ya ajira au kujipatia kipato kuliko kusubiri kuajiriwa.

“Mfano mzuri serikali kwa sasa inetengeneza fursa nzuri kwenye sekta ya kilimo na uzuri nchi yetu ina maeneo mengi wazi, lakini utakuta kijana msomi anasema anasubiri kuajiriwa badala atumie fursa kutengeneza ajira, nawaambia hao sio wasomi wazuri ambao Taifa linaweza kuwategemea,” amesema.

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela amesema kuwa jumla ya kaya 2,724 zilihesabiwa katika vitongoji 1,506 na kazi ilifanikiwa kwa asilimia 99.99.

“Kwenye kazi hii serikali ilitupatia kiasi cha Sh5.9 bilioni na tumefanikisha kazi hiyo na vifaa vyote tulivyokabidhiwa tumerudisha kasoro vishwambi vitano ambavyo vilipotea, lakini jeshi la polisi vinaendelea na kazi ya kuvipeleleza vipatikane,” amesema.
Kilimo...? mtu analima mboga mboga zake hekari 10 anakaribia kuvuna then serikali inaziharibu kisa kalima sehemu isiyoruhusiwa.... WTH
 
Anne makinda...
20221013_143835.jpg
 
Kamisaa wa Sensa Kitaifa, Anna Makinda amewataka vijana wasomi kujitengenezea uchumi wao binafsi kupitia fursa zilizoko kwenye maeneo wanayoishi kuliko kutegemea ajira kutoka Serikalini au sekta binafsi.

Akizungumza leo Oktoba 12 na Kamati ya sensa katika kikao cha kutathimini sensa kwa Mkoa wa Arusha, Makinda ambaye pia ni Spika mstaafu, amesema kuwa takwimu hizo ni muhimu kwa nchi kwenda kutengeneza mfumo mzima katika hatua zake za kusaidia jamii hasa kiuchumi.

“Lipo jambo kubwa nililoliona nalo ni kundi kubwa la vijana ambao hawana ajira wala hawajishughulishi na kazi yoyote ya kujiingizia kipato na ukimuuliza anasema amehitimu elimu fulani anasubiri ajira, jamani hili la kuajiriwa mtachelewa sana,” amesema Makinda

Amesema kuwa tatizo la ajira linalotupiwa serikali linaweza kutatulika na muhusika mwenyewe kwa kutazama changamoto zilizoko hata katika jamii na kuliwekea ubunifu mzuri na kuwa fursa ya ajira au kujipatia kipato kuliko kusubiri kuajiriwa.

“Mfano mzuri serikali kwa sasa inetengeneza fursa nzuri kwenye sekta ya kilimo na uzuri nchi yetu ina maeneo mengi wazi, lakini utakuta kijana msomi anasema anasubiri kuajiriwa badala atumie fursa kutengeneza ajira, nawaambia hao sio wasomi wazuri ambao Taifa linaweza kuwategemea,” amesema.

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela amesema kuwa jumla ya kaya 2,724 zilihesabiwa katika vitongoji 1,506 na kazi ilifanikiwa kwa asilimia 99.99.

“Kwenye kazi hii serikali ilitupatia kiasi cha Sh5.9 bilioni na tumefanikisha kazi hiyo na vifaa vyote tulivyokabidhiwa tumerudisha kasoro vishwambi vitano ambavyo vilipotea, lakini jeshi la polisi vinaendelea na kazi ya kuvipeleleza vipatikane,” amesema.
Hakuna jambo linaloniudhi mimi kama hawa viongozi kusimama na kuwaambia vijana wawajiajir wenyewe bila ya kuweka wazi ni ajira gani wanazozisema na mtu atawezaje kujiajiri bila ya kuwa na mtaji? Ningelipenda sana tena sana kumsikia huyu bibi akizitaja areas ambazo vijana wataweza kujiajiri bila ya kuwa na kipato. Unategemea mtu aanze kujiajiri kwa kuchukuwa mkopo kutoka benki gani? Ni benki gani nchini ambayo iko tayari kutoa mamilioni ya mkopo kwa kijana ambae hana ajira, hana mtaji wala hata kibanda cha kuishi na hakuna uhakika kuwa mradi wake utaweza kurudisha mkopo? Hivi hawa viongozi wanaambia maneno hayo hayo watoto wao? Au wao ndio huwaendea mbio kila mahali na kutumia umaarufu wao kuwapatia kazi serikalini na katika mashirika ya umma?

Si mlishaambiwa kama ni kweli kujiajiri ni rahisi ni kwa nini nyinyi wenyewe ambao mna ma PhD na madude mengine mumenshindwa kujiajiri na mumekimbilia kwenye siasa? Ni kwa nini maprofesa na wahitimu tele wa fani toka za sheria hadi elimu mnakimbilia nafasi za bungeni na hamuanzishi ajira zenu wenyewe?

Ajira pekee ambayo kijana wa mtanzania mlala hoi ambayo anaweza kujiajiri ni ya kuiba, kutapeli watu, kuuza madawa ya kulevya au kuwa malaya mitaani kwa sababu ajira hizo hazihitaji mtaji kuanzisha. Oh well labda muuza madawa ya kulevya atahitaji mtaji lakini ni mdogo sana wa kuanzia.
 
Mwanao Moris Makinda, ambaye Hata baba yake hajulikani aliko alijitafutia ajira mwenyewe?
Huyo Moris atakuwa mtoto baadaye sana maana huyo mama Makinda wakati yupo UDSM alitoa mimba, wazee wa Punching anawajua sana jinsi walivyomdhalilisha kwa hilo tukio lake.
 
Wakongwe wang'atuke,wameshapata misingi tayari.Huyu kijana amemaliza Chuo hana ardhi wala mtaji, anawezaje kujiajiri na bank wanataka security

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Kwani ajira itapatikana vipi wakati kuna school of law inatema watu, ambao wangejiajiri japo nao wana kasoro zao
 
Moris makinda alikuwa zero akiwa private school moja huko arusha na alimaliza Form four 1987 .
Baada ya hapo alipelekwa ulaya na hana na hawezi kufanya chochote iwe biashara ila ameajiriwa eneo nyeti hapa nchini
Sasa kuna haja gani ya kunianika humu? Hujanitendea haki kabisa.

Kwanza iko wapi picha ya ghorofa arobaini maji ya chai Arusha?
 
Wewe jamaa ulitakiwa uwe mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Harvard huko! adriz mshauri huyu jamaa akachukue PhD yake haraka pale SAUT, ili tuje tumpe nchi!

This fella is a genius, talented and bright! Ona haya madini aliyomwaga hapa jukwaani!
Jamaa GENTAMYCIME yuko vizuri sana,mm binafsi namkubali sana

Ova
 
Siasa zetu hazina weledi. Unawambiaje vijana wajiajiri wakati kuna mlolongo wa kodi, tozo, ushuru yaani mtu anafungua kiduka cha kuuza maji tuu karatasi kibao.

Mazingira yawekwe vijana wote wafanya biashara miaka 3 bila kodi yoyote waone kama vijana hawatajiajiri.
Tena wangeanza kwenye kilimo huko
Waweke nguvu zote,waachane na kujengajenga mambo ambayo hayana faida kwa raia

Ova
 
Nakumbuka nilienda kumpa mkopo mwanae wa kike na kiume wakati wako mikocheni Dsm nikakuta mwanae anamtia vidore Binti mmoja pale kwenye swimming pool saa tatu'' za asubuh uku Kwa pemben wamewasha Tiv na kuweka TBC1 wanaangalia Bingena mama yake ndo alikuwa anaendesha kikao walai kuanzia siku hiyo nilikacha kuniangalia TBC aise Leo mama anasema ujinga huo kabisa
Hahahahahajhahahaja Hahaha
Nmecheka mpaka konyagi imemwqgika hapa

Ova
 
Nilitaka kumtukana lakini kwa kuwa ni Mama basi bora nikae kimya tuu.
Kweli mama wewe ni kusema hivi?
 
Swala la Ajira ni Swala la Serikali wasilikimbie. Nchi kuwa na vijana Jobless ni aibu kwa Serikali.

Wawalazimishe watu wastaafu serikalini kwa wale bmving'ang'nizi wawaweke vijana.

Kama Serikalini nafasi zimejaaa wawalete wawekezaji wengi zaidi na wawapunguzie kodi ila wawekeze kwa Wingi hapa Tz na vijana wote wapate Ajira.

Tukiwa na Ajira vijana wote Serkali itapata Kodi nyingi.
 
Yeye ajira aliitafutia wapi? Tumeanza kumsikia tungali tumboni mwa mama zetu anakula pesa ya serikali mpaka sahizi tunasubilia wajukuu yeye yupo tu au anasubilia mpaka meno yang'oke mdomoni, watu wengine jamani.
 
Mbona yeye ameajiriwa na maraisi wa awamu zote na hajawahi kataa?
Hebu atulie
 
Back
Top Bottom