Anne Makinda awataka vijana kujitafutia ajira

Anne Makinda awataka vijana kujitafutia ajira

Hata ukipewa mtaji kwa hali ya kibiashara ya Bongo tabu tupu. Labda ufanye biashara isiyo rasmi ukijidanganya kurasimisha tu unakutana na rungu la TRA na nduguze.
Tusipende kulaumu sana wakitupa mitaji tuchangamkie fursa.

Kwa sababu ni wasomi haohao ndio wenye kupanga viwango sasa ngoja nao waone ubaya wa kukaa ofisini na kupanga bila kujua uhalisia.
 
Tusipende kulaumu sana wakitupa mitaji tuchangamkie fursa.
Bongo ukitaka kutoboa kama huna pesa ya kujitosheleza anza kufanya biashara isiyo rasmi. Ukijiingiza tu kwenye system huku biashara haijasimama ni kujikaanga.
 
Bongo ukitaka kutoboa kama huna pesa ya kujitosheleza anza kufanya biashara isiyo rasmi. Ukijiingiza tu kwenye system huku biashara haijasimama ni kujikaanga.
Unafiki wetu ndio unaotuangamiza msomi akipata kazi TRA anakandamiza Wafanyabiashara akikosa kazi ya Serikali anaogopa kujiajiri kwa kujua TRA itakuja kumkandamiza na Kodi zake za kinyonyaji.

Unafiki ndio unaotumaliza.
 
Bro I speak from experience nipo na mwanangu tumeanzisha kikampuni chetu, hizo gharama tulizoingia kuanza kurasimisha from registration mpaka kupata leseni, then kumaliza na mambo ya TRA. Ni mchakato mrefu sana na unachosha kuna muda tunasema bora tungeanza kibubububu kwanza.
 
1665637596693.png

Kamisaa wa Sensa Kitaifa, Anna Makinda amewataka vijana wasomi kujitengenezea uchumi wao binafsi kupitia fursa zilizoko kwenye maeneo wanayoishi kuliko kutegemea ajira kutoka serikalini au sekta binafsi.

Akizungumza leo Oktoba 12 na Kamati ya sensa katika kikao cha kutathimini sensa kwa Mkoa wa Arusha, Makinda ambaye pia ni Spika mstaafu, amesema kuwa takwimu hizo ni muhimu kwa nchi kwenda kutengeneza mfumo mzima katika hatua zake za kusaidia jamii hasa kiuchumi.

“Lipo jambo kubwa nililoliona nalo ni kundi kubwa la vijana ambao hawana ajira wala hawajishughulishi na kazi yoyote ya kujiingizia kipato na ukimuuliza anasema amehitimu elimu fulani anasubiri ajira, jamani hili la kuajiriwa mtachelewa sana,” amesema Makinda

Amesema kuwa tatizo la ajira linalotupiwa serikali linaweza kutatulika na muhusika mwenyewe kwa kutazama changamoto zilizoko hata katika jamii na kuliwekea ubunifu mzuri na kuwa fursa ya ajira au kujipatia kipato kuliko kusubiri kuajiriwa.

“Mfano mzuri serikali kwa sasa inetengeneza fursa nzuri kwenye sekta ya kilimo na uzuri nchi yetu ina maeneo mengi wazi, lakini utakuta kijana msomi anasema anasubiri kuajiriwa badala atumie fursa kutengeneza ajira, nawaambia hao sio wasomi wazuri ambao Taifa linaweza kuwategemea,” amesema.

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela amesema kuwa jumla ya kaya 2,724 zilihesabiwa katika vitongoji 1,506 na kazi ilifanikiwa kwa asilimia 99.99.

“Kwenye kazi hii serikali ilitupatia kiasi cha Sh5.9 bilioni na tumefanikisha kazi hiyo na vifaa vyote tulivyokabidhiwa tumerudisha kasoro vishwambi vitano ambavyo vilipotea, lakini jeshi la polisi vinaendelea na kazi ya kuvipeleleza vipatikane,” amesema.
 
huyu mama amekuwa kwenye ajira tangu apate akili hadi leo , mbona hakutoka ili akajiajiri ?
Yaani tangu ujana wake, tangu enzi za utawala wa Mwalimu Nyerere! mpaka leo ni bibi kikongwe! Bado anakula tu hela za serikali. Halafu eti mtu huyo huyo leo anapata kabisa ujasiri wa kuwashauri vijana kujiajiri!

Maajabu ya dunia haya.
 
Serikali haitengenezi Ajira isipokuwa inaweka Sera nzuri ambazo zitachochea Uwekezaji ambako huko kunaweza kupatikana Ajira nyingi za Kutosha...
Wewe jamaa ulitakiwa uwe mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Harvard huko! adriz mshauri huyu jamaa akachukue PhD yake haraka pale SAUT, ili tuje tumpe nchi!

This fella is a genius, talented and bright! Ona haya madini aliyomwaga hapa jukwaani!
 
USHAURI KWA SERIKALI.

kwanini isifanye na vyuo vya ufundi kusoma BURE Kama wanavyofanya kwa shule za msingi na secondary?

Unamwambia mtu ajiajiri lakini haujampa UJUZI wowote.

Hawa panya road wangekuwa na ujuzi wasingehangaika.

Ni muda sasa kwa serikali kuturuhusu kuingia huko hata kwa kozi fupi zitatusaidia.
 
Arusha. Kamisaa wa Sensa Kitaifa, Anna Makinda amewataka vijana wasomi kujitengenezea uchumi wao binafsi kupitia fursa zilizoko kwenye maeneo wanayoishi kuliko kutegemea ajira kutoka serikalini au sekta binafsi.

Akizungumza Oktoba 12, 2022 na Kamati ya sensa katika kikao cha kutathimini sensa kwa Mkoa wa Arusha, Makinda ambaye pia ni Spika mstaafu, amesema kuwa takwimu hizo ni muhimu kwa nchi kwenda kutengeneza mfumo mzima katika hatua zake za kusaidia jamii hasa kiuchumi.

“Lipo jambo kubwa nililoliona nalo ni kundi kubwa la vijana ambao hawana ajira wala hawajishughulishi na kazi yoyote ya kujiingizia kipato na ukimuuliza anasema amehitimu elimu fulani anasubiri ajira, jamani hili la kuajiriwa mtachelewa sana,” amesema Makinda.

Amesema kuwa tatizo la ajira linalotupiwa serikali linaweza kutatulika na muhusika mwenyewe kwa kutazama changamoto zilizoko hata katika jamii na kuliwekea ubunifu mzuri na kuwa fursa ya ajira au kujipatia kipato kuliko kusubiri kuajiriwa.

“Mfano mzuri serikali kwa sasa inetengeneza fursa nzuri kwenye sekta ya kilimo na uzuri nchi yetu ina maeneo mengi wazi, lakini utakuta kijana msomi anasema anasubiri kuajiriwa badala atumie fursa kutengeneza ajira, nawaambia hao sio wasomi wazuri ambao Taifa linaweza kuwategemea,” amesema.

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela amesema kuwa jumla ya kaya 2,724 zilihesabiwa katika vitongoji 1,506 na kazi ilifanikiwa kwa asilimia 99.99.

“Kwenye kazi hii serikali ilitupatia kiasi cha Sh5.9 bilioni na tumefanikisha kazi hiyo na vifaa vyote tulivyokabidhiwa tumerudisha kasoro vishwambi vitano ambavyo vilipotea, lakini jeshi la polisi vinaendelea na kazi ya kuvipeleleza vipatikane,” amesema.

Chanzo: Mwananchi
 
inashangaza sana kwa kiongozi kama yeye kutamka hayo maneno kama hayo.yeye aliishakuwa spika na bado yuko kwenye utumishi halafu anawadanganya vijana wakalime tena kilimo cha kutegemea mvua!kuna scheme ngapi za umwagiliaji walizozianda?

Masoko ya mazao watakayolima yako wapi?je mitaji ya kuanzisha hizo biashara wanapata wapi wakati hata mikopo hiyo ya halmashauri inaenda kwa watu ambao si sahihi bali kwenye vikundi chawa vya kisiasa.vijana wakitaka kuwa maskini waende huko.na je hao ambao wako mijini wamewaanda vipi kwenye hizo fursa?wanasiasa ndo chanzo cha yote hayo tunayoyaona kwa vijana kukosa shughuri za kufanya.
 
Siasa zetu hazina weledi. Unawambiaje vijana wajiajiri wakati kuna mlolongo wa kodi, tozo, ushuru yaani mtu anafungua kiduka cha kuuza maji tuu karatasi kibao.

Mazingira yawekwe vijana wote wafanya biashara miaka 3 bila kodi yoyote waone kama vijana hawatajiajiri.
 
Back
Top Bottom