TANZIA Anne Rwigara afariki dunia. Ni dada wa Diane aliyejaribu kugombea Urais dhidi ya Kagame. Mama asema kifo hicho ni fumbo

TANZIA Anne Rwigara afariki dunia. Ni dada wa Diane aliyejaribu kugombea Urais dhidi ya Kagame. Mama asema kifo hicho ni fumbo

Usiwacheke. Sisi hapa ccm inatusumbua tangu 1977. Heri ya Rwanda Kagame kaanza kuwatesa mwaka 2000
Si bora CCM walau Rais anabadirika baada ya miaka 10, sasa tangu 2000 sura ni ile ile tena anaongoza kwa mkono wa chuma. Waliozaliwa 2000 leo hii wapo Vyuo vikuu hawajui hata kama kuna uwezekano wa Rais akachaguliwa mwingine zaid ya PAKA.

Rwanda na Uganda ni pacha lakini afadhali zaidi Uganda, Museveni siyo mbabe kiwango cha PAKA
 
Kuna kipindi niliwahi ona mipicha picha yake ya bila nguo kwenye makochi na sehemu kadhaa .... nadhani kipindi iko alikuwa anataka wania uongozi fulani na alikuwa tishio sana
 
Yapo yaliyotokea ambayo Amin mwenyewe alikiri hakuhusika nayo. Kwenye mahojiano fulani na BBC nadhani mwaka 2003 aliwahi kuulizwa kuhusu watu kuuawa na kupotea. Alijibu kuwa inawezekana baadhi ya matukio kufanywa na askari pasina idhini ya moja kwa moja kutoka kwake.

La muhimu tambua kuwa kulikuwa na upinzani na njama nyingi dhidi ya Amin na katika mazingira ya kujihami kesi kadhaa za ukiukwaji wa haki za binadamu zinaweza kutokea.

Hakuna mtu aliyekamilika kila mmoja ana mapungufu yake lakini Amin hakuwa kama ambavyo watu wanavyomzungumza kwa ubaya.
Ebu jipe muda utafute taarifa nyingi kumhusu kabla ya kujenga hoja, maana kwa ninavyokuhisi hata suala Entebbe unaweza kusema alisingiziwa!
 
Back
Top Bottom