Annunaki created Man: Binadamu tunaoishi sasa tulitengenezwa (tuliumbwa) na Annunaki

Sawa Mkuu asante. Ningependa kufahamu hao Annunak ni watu?
Kama mabaki ya giants ambao yanasemekana ni ya hao Annunaki yamegunduliwa sehemu mbali mbali duniani na vina saba vyake vinafanana na vya kwetu, na kama inavyosemwa tumetokana na wao, mimi naweza kusema ni viumbe watu kama sisi, isipokuwa kuwa wao ni beyond extraordinary level ukilinganisha na sisi
 
Shetani ana wivu mbaya! Hapendi kabisa tunavyomuabudu Mungu wa kweli! Anatamani sana tuache kumuabudu Mungu tumuabudu yeye! Tusipokuwa makini tutaangushwa kiimani! Annunak siyo Mungu!!! Hajaumba chochote!! Yeye mwenyewe ni kiumbe! Mungu siyo kiumbe! Hajaumbwa na yeyote!
 
Shetani ni nani na Mungu ni nani?
Tuthibitishie uwepo wao na pia tunaomba uthibisho wa Annunak kutoumba kitu tafadhari
Maana naona umekuja na maneno matupu bila fact!
 
Lakini hawa jamaa wanaoitwa kwa jina la heshima malaika (ili kututofautisha na sisi) waliweza kuzaa na sisi japo si viumbe wa kingdom moja.! Hii ni shida
Labda tuseme hivi ; kwa mujibu wa Biblia sisi wanadamu tumeumbwa kwa mfano wake Mungu!! so sisi ni miungu!! pia sababu tumetokana na Mungu! tunaweza kuwatumia malaika chochote! na wakatii, mpaka leo. hii ndo zawadi alio tupa Mungu tuna amri hiyo!

Tunaweza kuumba chochote na kikawa, kikatutumikia mfano watoto, meli, gari , ndege, rocket nk! n wanyama tunawatawala! na Malaika vile vile ni watu pia! ila wao hawana dhambi,

lkn hao walio kuja ( the watchers) walikuja kumfundisha mwanadamu matumizi mbalimbali ya mimea , madawa, kuunda siraha nk lkn walianguka dhambini !! jua malaika ni binadamu kabisaaa!...hata hapo wewe ni roho.....km hujaelewa

fikiria tu unapoootaga sometimes ndoto za ajabu ajabu, jiulize tu ni nani yule huwa anatembea ndoton? tena unakuwa na kumbukumbu nazo unaweza cheka kwa zile ndoto za ajabu wengine huwaga wanaota na yanatokea kweli!

Kama huotagi sasa wewe utakuwa na kundi lako lipo ebu nikuulize mkuu umewahi kuota?

so wakazini na wanadamu sababu waliona mabinti za wanadamu ni njema kwao wakazaa nao!!! kitabu cha mwanzo utaipata hii! na walikuwa na majina yao kabisaaa!! nakumbuka mmojawao aliitwa Semjaza!!
 
THE BOOK OF ENOCK/TAFSIRI ISIYO RASMI YA KISWAHILI.

SEHEMU YA KWANZA


Kwa wanaopenda kuongeza maalifa zaidi kuhusu (annunaki/watchers/fallen angels / giants ) nimetoa tafsiri isiyo rasmi kutoka kingereza kuja kiswahili kwa msaada wa Google translate, kukitafsiri kitabu cha Enoko/The Book of Enock

Hii simulizi ya wanefili/giants/annunaki/fallen angels imeelezwa kwenye kitabu cha Mwanzo japo kwa ufupi sana, ambapo haiwezi kutoa picha halisi kwa kilicho tokea enzi hizo kabla ya gharika ya nuhu, na nini kilisababisha Mwenyezi Mungu alete gharika, tofauti na masimulizi tunayo fundishwa makanisani/misikitini.

Nimeanza na nukuu kutoka kitabu cha Mwanzo sura ya 6,

"1 Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, 2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.

3 Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.
4 Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile;tena ,baada ya hayo ,wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao wana;
hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani ,watu wenye sifa.


Hapa chini nimeambatanisha tafsiri siyo rasmi ya kitabu cha enoko/The Book of Enock, kinacho elezea kwa undani kitabu cha Mwanzo sura ya 6.

6.1 Ikawa wanadamu walipozidi kuongezeka, katika hizo siku walizaliwa kwao binti wazuri na wazuri. 6.2 Na Malaika, wana wa Mbinguni, wakawaona na wakawatamani. Na wakaambiana: Njooni, tujichagulie wake kutoka watoto wa watu, na tuzae, kwa ajili yetu wenyewe, watoto."

6.3 Naye Semyaza, mkuu wao, akawaambia, Je! “Ninahofia kwamba msije mkatamani kitendo hiki kifanywe na mimi peke yangu, kwa kuwa nitalipa kwa dhambi hii kubwa."
6.4 Wakamjibu wote, wakasema, "Sote na tuape kiapo, na kufungamana sisi kwa sisi kwa laana, ili tusibadilike. mpango huu, lakini kutekeleza mpango huu kwa ufanisi."
6.5 Ndipo wakaapa wote pamoja, na wote wakafungamana kwa laana 6.6 Na hao wote walikuwa mia mbili, wakashuka Ardis; ambao ni kilele cha Mlima Hermoni. Nao wakauita mlima Hermoni kwa sababu juu yake waliapa na kufungiana kwa laana.

6.7 Na haya ndiyo majina ya wakuu wao; Semyaza aliyekuwa kiongozi wao, Urakiba, Ramiel, Kokabiel, Tamiel,Ramieli, Danieli, Ezekieli, Barakieli, Asaeli, Armaros, Ananeli, Zaqiel, Samsiel, Satael, Turiel, Yomiel, Araziel.

6.8 Hao ndio wakuu wa wale Malaika mia mbili na wa wale wengine wote pamoja nao.

7.1 Wakajitwalia wake, na kila mtu akajichagulia mmoja kila mmoja. Na wakaanza kuingia ndani yao na kufanya uasherati na wao.
Na wakawafundisha hirizi na siga, na wakawaonyesha kukata mizizi na miti.

7.2 Wakapata mimba, wakazaa Majitu makubwa. Na urefu wao ulikuwa dhiraa elfu tatu.

7.3 Hawa wakawatumikisha wanadamu; mpaka wanadamu wakashindwa kuwatosheleza

7.4 Na hao Wanefili wakawageukia ili kuwala watu. 7.5 Wakaanza kutenda dhambi juu ya ndege, na wanyama, na juu ya wanyama

watambaao, na juu ya samaki, wakaanza kulana nyama wao kwa wao, na kunywa damu zao

7.6 Kisha nchi ikawalalamikia uasi wao.

8.1 Naye Azazeli akawafundisha watu kutengeneza sword, na visu, na mapanga na ngao, Naye akawaonyesha mambo baada ya haya, na ufundi wa kutengeneza; vikuku, na mapambo, na jinsi ya kuremba/kupamba kope za macho; na vito vya thamani, na kila aina ya rangi . Na ulimwengu ulibadilishwa.

8.2 Kukawa na uovu mkuu, na uasherati mwingi; Wakatanga mbali, na njia zao zao zote zilionekana kua mbaya.

8.3 Amezaraki akawafundisha wote wanaoroga na kukata mizizi, Armaros akawafundisha uchawi wa kutumia maneno, Baraqiel unajimu, na Kokabiel aliwafundisha utabiri, na Tamiel alifundisha unajimu, na Asradel alifundisha njia ya Mwezi/path of the moon

8.4 Na sauti za vilio vya wanadamu zilifika Mbinguni.

9.1 Kisha Mikaeli, Gabrieli, Surieli na Urieli, wakatazama chini kutoka Mbinguni na kuona wingi wa damu iliyokuwa ikimwagwa juu ya nchi na uovu uliokuwa ukifanyika duniani.

9.2 Wakaambiana, sauti ya vilio vya wanadamu, na kilio cha Nchi iliyoharibiwa na ipae kwa sauti kubwa; mpaka Lango la Mbinguni.

9.3 Na sasa kwenu, Enyi Watakatifu wa Mbinguni, roho za wanadamu zinanung'unika; wakisema: "Tupelekee vilio na mateso yetu mbele ya Aliye juu."

9.4 Na wakamwambia Mola wao Mlezi, Mfalme: Mola Mlezi wa Miungu, Mungu wa miungu! Mfalme wa wafalme! Kiti chako cha enzi kitukufu chadumu vizazi vyote vya Mwenyezi-Mungu, ulimwengu, na kubarikiwa na kusifiwa!

9.5 Wewe ndiye umefanya kila kitu, na uwezo juu ya kila kitu ni chako. Na kila kitu kimefunuliwa, na kipo wazi, mbele yako, na unaona kila kitu, na hakuna kitu ambacho kinaweza kufichwa kutoka kwako.

9.6 Basi angalieni alivyofanya Azazeli; jinsi alivyofundisha maovu yote juu ya dunia, na kufunua siri za milele za Mbinguni.

9.7 Na Semyaza amewafundisha wanadamu uchawi wa kutumia maneno, uliyempa mamlaka kuwatawala wale walio pamoja naye.

9.8 Wakaingia kwa binti za wanadamu pamoja, wakalala na wanawake, wakawa najisi, na kuwafunulia dhambi hizi.

9.9 Na hao wanawake wakazaa Majitu, na kwa hayo dunia nzima imejawa na umwagaji damu na uovu

9.10 Na sasa tazama roho zilizokufa zinalilia na zinalalamika Nje ya lango la Mbinguni, na maombolezo yao yamepaa, wala hawawezi kutoka mbele ya uovu unaofanywa duniani.

9.11 Nanyi mnajua yote kabla hayajatokea, nanyi mnajua haya, na kinachomhusu kila mmoja wao. Lakini husemi chochote kwetu. Tunapaswa kufanya nini kuhusu hili?"
 
"Mungu ni nani?, uwepo wa Annunaki umethibitishwa kwa facts, Mungu tunamthibitishaje
Hakuna kitu rahisi sana, kama kumjua Mungu wa kweli, tena ukimtaka utamjua tu! ila sasa ni udumu kwa sara na Maombi!! kukwambia tu kwa mdomo wangu na kwa kupitia imani yangu ni ngumu kuelewa ndg!

Fikiria tu kuna watu hawakumwamini Yesu miaka hiyo, mpaka leo watu wengine wanampinga bado!! ni mpaka ajifunue kwako na Biblia inasema ivi imani si Mali ya kila mtu!

Yeye ataona na kutambua imani ya moyo wako!! wala hachelewi ... kumbuka kuna wachungaji kila kona ya Dunia hii wanahubiri usiku na mchana lkn bado watu hawajui uwepo wake!

Maandiko yanasema siyo kila aniitae Bwana bwana ataingia ktk ufalme wa mbinguni kwa maana kuwa kuna watu hawataingia huko japo leo ni mapadre, wachungaji hatare! hekima ya Mungu atakupa yeye ukimtafuta kwa bidii!
 
nimeikubali san hii akhsante mkuu daaa!
 
mkuu natafuta hiki kitabu cha kiswahili
 
Kwanza nitangulize samahani kwa member Dumas, wewe ni ndumilakuwili sana mkuu!

Kuna uzi humu ulibishana mpaka ukatokwa na mishipa kwa kusisitiza binadamu hakuumbwa bali alitokana na bacteria na blah blah kibao za big bang theory 😂

Hapa unakubali binadamu kaumbwa na Anunaki, mkuu binadamu ametokana na bacteria kwako ni fact, binadamu kaumbwa na Anunaki pia kwako ni fact, tuambie which is which

Nimegundua hawa atheists wapo tayari kuamini masimulizi yoyote tofauti na Biblia ili kujifurahisha tu 😂😂
 
Nmekuuliza swal huko juu hunajib mpaka muda huu...naona unachanganya sana mada mkuu. Haya mambo hebu yaache naona unaanza ongea vtu vingne sasa...

Nmekuuliza swal rahis kabisa. Hao malaika unasema hawana dhamb...maara wakaja tamani mara walikuna fundisha elimu ya mimea etc...nmekuuliza...kama waliweza tamani wanadamu na wakazaa nao ina mana malaika wana via vya uzazi?..wana matamanio? Inamana miili yao inayengeneza sperm etc...si ndio?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
THE BOOK OF ENOCK/TAFSIRI ISIYO RASMI YA KISWAHILI.

SEHEMU YA PILI


10.1 Ndipo Aliye juu, aliye Mkuu, na Mtakatifu, akanena na kumtuma, Arsyalauri kwa mwana wa Lameki, akamwambia,

10.2 Mwambie kwa jina langu, ujifiche, ukamfunulie, kwa sababu dunia yote itaharibiwa. Gharika itakuja juu ya dunia yote; na vyote vilivyomo ndani yake vitaangamizwa.

10.3 Basi sasa mfundishe, apate kuokoka, na uazao wake wapate, kuishi "

10.4 Kisha Bwana akamwambia Rafaeli, Mfunge Azazeli kwa mikono yake, na miguu yake na kamtupe gizani. Kapasue jangwa, ambalo Lipo Dudael, na umtupe huko.

10.5 Na mtupieni mawe yaliyochongoka, na mfunikekwa giza. Na akae huko milele. Na mfunike uso wake ili asiweze kuona mwanga.

10.6 Na ili siku ile iliyo kuu ya Hukumu, atupwe ndani moto.

10.7 Na uirudishe ardhi waliyo iharibu Malaika walio hasi . Na kutangaza urejesho wa Dunia mpya. Kwa maana nitairejesha dunia ili

wanadamu wasiangamie kwa sababu ya ujuzi na maarifa waliyo fundishwa.

10.8 Na dunia nzima imeharibiwa kwa mafundisho ya kazi za Azazeli; na juu yake andika: WOTE WANA DHAMBI.

10.9 Bwana akamwambia Gabrieli, Nenda mbele ya hao wana haramu, na hao wana wa malaika waliokataliwa, na juu ya wana wa wazinzi, ukawangamize watoke miongoni mwa wanadamu. Na wapeleke nje, wauwane wao kwa wao, na waajiangamize, wenyewe katika vita; kwa maana hawatakuwa na siku nyingi.

10.10 Nao watakuomba, lakini hawata samehewa, kwa maana wanatumaini wapate uzima wa milele, na kwamba kila mmoja wao apate kuishi kwa miaka mia tano."

10.11 Bwana akamwambia Mikaeli, Nenda ukamjulishe Semyaza, na hao wengine; pamoja naye, ambao wame ingiliana na wanawake na kujiharibia katika unajisi wao wote.

10.12 Wana wao wote watakapo uana wao kwa wao, na waonapo uharibifu wa wapendwa wao, uwafunge kwa jeneresheni sabini chini ya milima ya dunia, mpaka siku ya hukumu na utimizo wao, mpaka siku ya mwisho wa hukumu, ambayo ni ya milele.

10.13 Na siku hizo watatupwa mpaka kuzimu; katika mateso, na watafungwa milele.

10.14 Na kisha Semyaza atateketezwa, milele na milele,

10.15 Na kuziangamiza roho zote za matamanio, na wana wa malaika/watchers; kwa kuwakosea wanadamu.

10.16 Vunjeni uovu wote juu ya uso wa dunia na kila uovu wote utakwisha

10.17 Na wenye haki wote watakuwa wanyenyekevu, nao wataishi Na kuzaa maelfu. Na siku zote za ujana wao, na sabato zao, zitatimia kwa amani.

10.18 Na siku hizo dunia yote itakuwa yenye haki na Dunia yote itapandwa miti, nayo itajazwa baraka.

10.19 Na mizabibu ya kupendeza itapandwa juu yake, na kupanda juu .Na mzabibu iliyopandwa juu yake itazaa matunda kwa wingi;

na kila mbegu iliyopandwa juu yake, kila kipimo kitatoa elfu, na kila kipimo cha zeituni kitatoa bathi kumi za mafuta.

10.20 Na unaisafisha dunia na uovu wote, dhambi yote, na uchafu wote, na uchafu wote ulioko ulioletwa duniani.

10.21 Na wanadamu wote watakuwa wenye haki, na mataifa yote yatanitumikia na kunibariki na kuniabudu.

10.22 Nayo nchi itasafishwa na uharibifu wote, na dhambi zote; na kutoka katika ghadhabu yote na mateso yote; wala sitaleta mafuriko tena juu yake, kwa vizazi vyote, hata milele.

11.1 Na siku zile nitafungua akiba za Baraka, ambazo zipo mbinguni, ili niwateremshie juu ya nchi, na juu ya kazi, na juu ya taabu za wanadamu.

11.2 Amani na kweli zitatawala, siku zote na kwa vizazi vyote milele na milele.
 

Attachments

Nina rafiki yangu wa Kike Raia wa South Africa, majuzi kwenye Mazungumzo yetu, akanambia anaomba nimsindikize nchi ya Mali, nikamwambia Mali si salama sana, anataka kwenda kufanya nini...!?

Akanambia anataka kwenda kuwatembelea kabila la Dogon, kuna vitu anataka kwenda kujifunza....!

Alipozungumzia Dogon nikakumbuka hii mada, nikakumbuka kuna mdau kazungumzia kwa uchache kuhusu Dogon tribe, nika share na yeye kuhusu comment ya mdau.... Akanambia hiyo ndo sababu anataka kwenda Mali...!

Nikaanza kumweleza kuhusu huu Mjadala na baadhi ya michango ya wadau, kuna kitu akanambia.....!

Anasema miaka kadhaa nyuma alikua akienda Kazini asubuhi saa 1, amepanda kwenye Taxi, anasema ghafla Redio iliyokua inapiga mziki ikaanza kutoa sauti zilizovurugika, kama Mtu akiwa anatafuta channel, anasema alipotizama nje, akaona Chombo kikubwa sana Angani, kikiwa kinatembea Chini chini, anasema ni kikubwa kama Ukubwa wa Uwanja wa Mpira, akataka kuongea akaona hawezi, kama kashikwa bumbuazi, baada ya muda kile chombo kikapotea, akajaribu kumuuliza abiria mwenzake jirani kama aliona kile alichokiona, akasema hakuona chochote.....!!!
 
Ok. kwahiyo Mungu anayeabudiwa hajulikani?
 
Kama unasema tumeumbwa kwa mfano wake na sisi ni miungu basi naye ni mmoja wapo wa miungu. Na ukisema ni gods basi tablets kutoka sumerian zitakuwa sahihi kusema tumetengenezwa na Annunaki ambao ni miungu pia.
 
Asante sana. Jambo moja niongezee, ukisema kuna Mungu wa kweli na Mungu wa uongo, maana yake kuna Mungu zaidi ya mmoja. Neno Mungu limetoka sumerian, maandiko ya vitabu vitakatifu source yake ni sumerian, na wenyewe waliabudu miungu. Na kama Mungu aliwatuma hao malaika (gods) kuja duniani huende hawakumkta mwanadamu kama huyu leo/wa sasa, labda walikuwepo binadamu wengine tofauti kabisa na sisi homo sapiens wa leo, kwahiyo hao miungu walipofika duniani wakazaa na hao viumbe watu waliowakuta duniani na ikapelekea kutokea kwa homo sapiens binadamu wa sasa. Kwa nadharia hii itakuwa ni wazi kwamba tablets kutoka sumerian zitakuwa sahihi kusema tumetokana/tumetengenezwa na Annunaki ambao ni moja wapo wa hao Miungu uliowasema.
 
Haya mambo yapo sana ndugu, sema ndio hivyo stori zake hazivumi sana. Na hilo kabila Dogon civilization yao chimbuko lake ni sumerian, ukitaka kupata taarifa nyingi za ukweli kuhusu sumerian, Dagon ni moja wapo ya kabila lenye rekodi mbali mbali kutoka sumerian.
 
Ukisoma kitabu cha Enoko/The book of Enock kwa umakini utaanza kupata majibu ya baadhi ya maswali ambayo uko nyuma yalikuwa hayana majibu hasa kwa jamii za watu weus/Uzao harisi,(nimetumia watu weusi ili niweze kueleweka zaidi)
Kuna mdau uko nyuma aligusia kwanini jamii zote hapa Duniani, Wazungu, Wahindi, Waarabu, Wachina, wanawachukia sana watu weusi.
Magonjwa ya kutengenezwa, HIV, EBOLA, KIMETA, CORONA , CANCER, nk, yote kinaletewa kizazi cha watu weusi, vita, Madawa ya uzazi wa mpango, kutugombanisha tuuane sisi kwa sisi, yote yanafanywa kukifuta kizazi cha watu weusi Duniani.
Wote tulikiskia jinsi Bill Gate alivyo kuwa akitabilia mabaya kipindi cha COVID 19., kwamba watu weusi mamilioni wataangamia.

Hizi chuki hazijaanza leo, ni tangu enzi nyingi, Ukisoma kitabu cha Enoko unaweza kuaunganisha doti na kupata picha harisi.
Kitabu cha Ethiopia Book of Enock,kinaelezea jinsi Watchers/Anunaki/Malaika walio hasi, Walivyo watamani Binti za Watu/watu weusi na wakazaa nao, Hawa watchers wakawafundisha watu siri za mbinguni,/teknolojia mbali mbali, ambazo hawakupasa kuzitoa kwa watu, kwani zingeleta maangamizi kwa watu.
kikatokea kizazi cha Majitu/Giants/Wanefili. Hichi kizazi cha Wanefili ndicho kilikuwa kizazi chenye sifa enzi izo. Yalikuwa majitu makubwa yenye miili ya kutisha, yenye akili. Haya Majitu yakaanza kuwatumikisha watu wa asili wa Dunia hii. Yakaanza kuingiliana kimwili na wanyama, Ndege, na samaki, apa ndio tukatokea kizazi hybrid, nusu mnyama nusu binadamu, samaki mtu, nusu nyoka nusu binadamu. nk

Baadaye hichi kizazi cha Majitu kilikuja kuondolewa kipindi cha gharika, ila kuna yaliyopona, mfano Goliati, Ogu, nk, pia kuna yaliyo kimbilia kwenye mapango ardhini, na miji ya ardhini./Under ground cities
Sasa zile roho za haya majitu, yaliyo kufa kipindi cha Gharika, kutokana na kitabu cha enoko ndio roho zinazotesa watu kwa kuwaingilia kama mapepo.
Pia kuna Roho zinazo reincarnate/kuzaliwa upya kupitia kwa Binadamu wasio na NAFSI, apa naongelea jamii nyingi za watu wa Ulaya na Asia, Wengi mmesha wahi kuzisikia na kuziona hasa kwa jamii za wahindi kupitia Movie zao. Mtu anakufa baadae anazaliwa tena.

Unapo ona jamii za watu wa Magharibi na Asia zinawatendea watu weusi unyama/Utumwa/Chuki/magonjwa ya kutengeneza/ nk, ni zile roho za enzi ya Gharika zinakuja kulipa kisasi kwa kizazi cha watu weusi, wanadai jamii ya watu weusi ndio walisababisha watchers/annunaki wakapata Ukumu ya milele,wakafukuzwa juu ya uso wa Dunia, wasiweze kuona mwanga(Fatilia movie za Vampire wanazo igiza wazungu utanielewa, kwanini vampire hawapatani na mwanga wa jua) na roho za watoto wao/wanefili/giants/ zikafungwa Kuzimu, na wakaondolowa uwezo wa kuishi milele.

Wale malaika waasi/Annunaki/ wengine wakiongozwa na Kiongozi wao Semyaza, wao walifungwa kwa generetion 7, watafiti wanadai walifungwa kwenye Bara la Antarctica, ndio hao wanashirikiana na jamii za watu wa Magharibi na Asia (Vizazi vya watchers) kuwapa teknolojia mbali mbali unazoziona apa Duniani.
Hawa watchers wanajiandaa kurudi Duniani, kuendeleza utawala wao(New World Order), sasa ivi wana wanandaa watu kisaikolojia kupitia Holly Hood/ Television na vyombo vya Habari, mambo ya Alliens/UFO kipindi hiki yameshika kasi tofauti na miaka ya nyuma.

Kwa jicho langu la mbali linaona watu weusi uko mbeleni watapata dhiki ya ajabu ambayo haijawai kutokea toka kuwepo misingi ya Dunia, unganisha doti.
 
Ndiyo watarudi na mimi nshasema humu. Kwahiyo wazungu na wa Asia wameisha hukumiwa milele na Mungu ila weusi bado?. Kwahiyo Mungu alimuumba mtu mweusi tu?. Hapa ndipo vitabu vitakatifu vinapo onyesha uwalakini sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…