Kitu ambacho kimeshangaza wanasayansi wengi ni ile elimu ya kabila la dogoni "THE DOGON TRIBE" kule nchini Mali. Ambapo wao husema kwamba asili yao ni Misri ya kale (Ancient Egypt), na wanasema walihama na kuja Mali. Walihama pia na ujuzi wao wa siri kutoka Misri ya kale. Miaka 70 iliyopita wanasayansi wa mambo ya anga walikutana na chifu wa kabila la Dogoni na kwasababu walimuamini walimpa baadhi ya siri za kabila lao.
Kilichoshangaza sana ni kwamba hawa jamaa walikuwa na michoro ya mfumo wa jua (The Solar System) na sayari zake zote ambao una miaka zaidi ya 2000. Kilichoshangaza zaidi ni kwamba walikuwa na michoro mingine ambayo ilionesha mkusanyiko wa sayari nyingine ambazo ziko nje ya mfumo wetu wa jua. Sayari hizo zinaitwa Sirius, na wakaonesha jinsi zilivyojipanga. Baadhi ya wanasayansi wa NASA walihisi ni uongo labda, lakini miaka 70 mbele wakakuta ile michoro iko sahihi na sayari kweli zimejipanga vilevile.
Ambacho wadogoni wanaamini ni kwamba ule utaalamu walifundishwa na miungu wao maelfu ya miaka iliyopita kule Misri ya kale. Pia Mfumo wa sayari wa Sirius ndiko ambako miungu wao wanaishi. Hili lipo Officially Documented na unaweza kulitafuta mtandaoni na kulipata........
Sasa unachokisema kuhusu imani za Kisumeria na miungu kutokea angani kipo karibia kwenye tamaduni nyingi za kale ambazo hazijawahi kuwa na muingiliano wowote ule. Ukiangalia michoro ya Misri ya Kale, Michoro ya Babeli, Michoro ya Umedi na Uajemi utatambua kuna mambo mengi sana yamefanana. Kuna sehemu utaona binadamu wadogo wakiabudu binadamu wakubwa na warefu kuliko wao waliotokea juu. Au utakuta binadamu ana uso wa mnyama na mabawa.
Meso-America nako ni hivyohivyo: The Aztecs, The Mayans, The Anasazi na wengine wana ushahidi wa kihistoria wa kutembelewa na miungu wao kutokea angani, ambao waliwapa maarifa na ujuzi wa baadhi ya vitu. Ukija kwenye tamaduni za Kiyahudi kwenye kitabu cha Henoko (The Book of Enoch) na Kitabu cha Jasher (The Book of Jasher) unaambiwa kwamba baada ya anguko la Adamu na Hawa, malaika 200 (The Watchers) wakiongozwa na Semyaza walishuka duniani na kuzaa na wanawake binadamu.
Wakazaa nao na kutoa wanefili, halafu wakaanza kuwafundisha elimu za kila aina kama kusoma nyota, miti-shamba, uchoraji, uhunzi, na kutengeneza dhana za kivita. Wasomi wa masomo ya kibiblia wanaenda mbali zaidi na kuzungumzia mambo ya ajabu yaliyofanyika kwenye kitabu uzao wa Kaini kwenye kitabu cha MWANZO 4, ambapo vitukuu vya Kaini yaani Yabali, Yubali na Tubal-Kaini ndiyo waliofanya ugunduzi wa mambo makubwa duniani.
Yabali aligundua mbinu za kilimo, Yubali akagundua muziki na vyombo vyake na Tubal-Kaini akagundua kufua chuma. Sasa ni sawa na kusema leo hii nyumba moja itoe watoto kama Tesla, Einstein na Mozart, jambo linaloshangaza kidogo. Yaani watoto wa Lameki ambaye ni mjukuu wa Kaini ndiyo wagundue kila teknolojia muhimu duniani kwa wakati huo ??? Kuna mambo yanashangaza kidogo.
Mwisho kabisa: Lakini pia vita ya Annunaki, baina ya miungu Enki na Enlil kugombaniana utawala wa dunia hii na nani awe nani. Wanasayansi walichimba mafuvu ya kale eneo la Babeli na kutambua yana mionzi (Radio-Active Carbon Isotope). Najiuliza sana teknolojia ya kinyuklia ambayo sisi tunajivuania kugundulika mnamo karne ya ishirini, iliwezaje kufanana na mionzi ambayo imekutwa kwenye mafuvu ya watu wa Mesapotamia ya kale. Kuna mambo yanafikirisha ati ??? Hili nalo ushahidi wake unaweza kuupata kule Britannica....
Historia na vitabu vitakatifu vya dini kama AGANO LA KALE linakiri uwepo wa hawa miungu wengine huko Babeli, Uajemi na Misri. Biblia inasema kwamba YHW (YAHWEH) alisema kabisa anawachukia sana hawa miungu wengine. Lilikuwa ni kosa la kuuwawa endapo Muhebrania ukikamatwa unafanya ibada za Babeli (Assyrians/Sumerians) au zile za kimisri za kuabudu hawa (Annunaki a.k.a The Ancient Astronauts).
YAHWEH mwenyenye anakiri kwamba hawa viumbe uliowataja "The Annunaki" kuwepo, na amewaita kwa majina mengi kama "malkia wa mbinguni" au "Jeshi la mbinguni" au "mkuu wa uajemi" au "miungu ya misri" lakini kwanini awachukie sana na kukataa kabisa wahebrania kushirikiana nao ???
Ikumbukwe Babeli ya Nimrodi baada ya gharika ya Nuhu walikuwa wanawaabudu "Annunaki" , hii ni moja ya sababu ya YAHWEH kuwatawanya kwa nguvu. Pale sisi tunasema kwamba lugha zilivurugwa lakini kuna mambo mazito yalitokea hadi watu wakaacha kujenga mji na mnara na kukimbia. Hebu tusaidiane wadau...