KUTOKANA NA MAELEZO HAYO APO JUU NI DHAHIRI KUWA WANADAMU/WATU WANA ASILI TOFAUTI
Kabla swali lako halijajibiwa tayari umeshajipa majibu kwa swali ambalo mwenyewe umeuliza,hii inaonesha hata uambiwe nini huwezi kuelewa kwa sababu yatari una misimamo yako.
Kama wote wana wanadamu tumotokana na Adam na Hawa, kwanini tuwe na utofauti mkubwa katika makundi ya dam
Kama ulimsoma vizuri mtoa mada,nimesahau sehemu ya ngapi.
Mtoa mada alisema kwamba mazingira anayoishi mtu na mabadiliko anayopitia yanaweza kubebwa na DNA na mabadiliko hayo yakapita mpaka kwa mtoto.
Akatolea mfano wa mtu anayeogelea kwamba akifanya mazoezi sana kuna mambo atabadilika na mambo hayo yanaweza kupita mpaka kwa watoto.
Hivyo mazingira yanavyotuathiri yanaweza kubadilisha hata maumbile yetu na tukawa watu tofauti.
Hivyo kwa hoja hii ni wazi kwamba kutoka katika asili moja sio hoja kwwmba tusitofautiane.
Kwa sababu tumetoka katika asili moja lakini tumetawanyika na kuishi maeneo tofauti,na kula vitu tofauti kabisa.
Na hivyo vitu vinaweza kubadilisha physiology ya mtu akawa tofauti na wengine.
Kwa hivyo kuwa na rhesus tofauti baina ya mama na baba ni jambo la kawaida kwa sababu tulishaathiriwa na mazingira tofauti.
Kwanini mama mwenye kundi la Damu lenye Rh negative akibeba mimba ya kwanza mtoto akawa na kundi damu lenye Rh positive, mama anatengeneza antibodies/Kinga dhidi ya mimba zinazofuata, endapo mimba zinazofuata mtoto akiwa na Rh positive na damu zao zikaingiliana pindi mtoto akiwa tumboni mtoto anadhurika, kama kweli wote chanzo chetu ni kimoja, Adam na Hawa
Mkuu kuna uwezekano mkubwa wa sisi kuwa tofauti kwa sababu tumeishj mazingira tofauti.
Kwa sababu hiyo mwili unaadapt mabadiliko ya mazingira.
Na mabadiliko hayo ambayo yanatokea katika miili yetu inapita moja kwa moja kwa vizazi vyetu.
Ikiwa utakataa majibu haya maana yake pia ukatae k2amba hata annunaki hajamuumba mtu kwa sababu ingelikuwa tumeumbww na annunaki sisi wote tusingekuwa na utofauti.
Haiwezekani mimi niwe mfupi alafu hashim thabiti awe mrefu wakati sote tumeumbwa na annunaki.
Haiwezekani mimi niwe na macho makubwa alafu jirani yangu awe na macho maduuchu wakati tumeumbwa na annunaki.
Kwa msingi huo mkuu hoja uliyoitumia mkuu unapaswa kuitetea katika hadhra hii.