Another disappointment performance from Aziz Ki

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Nimeshamuongelea mara kadhaa siku za nyuma na nisingependa kurudia saana! Kuna watu hawakunielewa kabisa nadhani jana Nabi kawaonyesha panapovuja.

Kwa kifupi Aziz amebaki kuwa mchezaji wa "moment" yaani kupiga mijishuti tu basi zaidi ya hapo hana maajabu tena. Namba 10 gani unapoteza takriban kila mpira?

Tulitegemea baada ya Fei kuondoka adhihirishe ubora wake lakini kashindwa. Nawashauri Yanga wafanye mpango kumchukua Gomez wa Singida BigStars kama replacement ya Fei ila sio huyu jamaa kupwa na kujaa. Im very disappointed with his performance. Anapoteza sana mpira, pasi mkaa nyingi na hasaidii wenzake kukaba anazurula tu.
 
Nimeshamuongelea mara kadhaa siku za nyuma na nisingependa kurudia saana! Kuna watu hawakunielewa kabisa nadhani jana Nabi kawaonyesha panapovuja...
Naungana na wewe kabisa, huyu Aziz Ki simuelewi kabisa. Hata mechi ya kule mali alivyoingia akaharibu kabisa uchezaji wa timu. Kama unavyosema kupoteza mipira hovyo, pasi mkaa. Anyway tuendelee kumpa muda.
 
ukiwa nje ya uwanja siku zote unakuwa mchezaji bora kabisa. Sasa na wewe hebu nenda ukajaribu tuone hiyo performance yako uwanjani.
 
ukiwa nje ya uwanja siku zote unakuwa mchezaji bora kabisa. Sasa na wewe hebu nenda ukajaribu tuone hiyo performance yako uwanjani.
Ndio mana kocha anatakiwa awe nje ya uwanja ndo ataona makosa Kwa uzuri , na hata baada ya mechi huwa wanaenda kuangalia video Kwa mchezaji mmoja mmoja ili kurekebisha na kuona Kwa uzuri zaidi makosa yalipo Kwa kila mchezaji ... Mtu aliyeko nje ndo anaweza ona Kwa usahihi , watu husema sifa sahihi hutoka nje sio ndani ....
 
Naungana na wewe kabisa, huyu Aziz Ki simuelewi kabisa. Hata mechi ya kule mali alivyoingia akaharibu kabisa uchezaji wa timu. Kama unavyosema kupoteza mipira hovyo, pasi mkaa. Anyway tuendelee kumpa muda.
Yaani Match Analyst Jana anasema Aziz ki alikuwa kama abiria uwanjani,ha ha ha
 
Yaani Match Analyst Jana anasema Aziz ki alikuwa kama abiria uwanjani,ha ha ha
Hawakumtukana ila watamtukana mtoa mada, Azizi kwanza hana pumzi huhema sana.Nijuacho ni mchezaji mzuri lakini mwenye majivuno na mbwembwe.
 
Aziz Ki Stephanie sijui nini kimempata, yaani perfomance yake uwanjani ni below 50%. Nahisi hana shida inamsumbua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…