Tetesi: Ansbert Ngurumo: Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba, wamejivua uanachama wa CCM

Status
Not open for further replies.
Ni kawaida inapokaribia uchaguzi wakongwe kadhaa wanatoka ili kulaghai umma wanaenda upande wa pili akipewa namba wanavuruga uchaguzi baadae anarudi home
Mbinu ya kawaida sana hii
 
Hata kama wanatuhuma (kama ambavyo viongozi wote walivyo nazo) utaratibu ulipaswa kufuatwa.
Hatuwezi chama chetu kukubali kiendeshwe kihuni na kukoseana heshima kwa kuwatumia kina Musiba na Makonda kutukana na kudhalilisha watu.
Julai tunambwaga mwenyekiti (anayepeleka mambo kihuni) kwa kumnyima kubeba bendera uchaguzi 2020 kisha baada ya hapo tunamfyeka. Inatosha sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
Unataka "chama" kifutwe?

Mbona unajiondoa akili kiasi hiki mkuu!

Mwenyekiti ndio mwenye chama sasa hivi, nyinyi nyote ni mateka tu, hamna chenu ndani ya chama.
 
Mimi naona muheshimiwa Abadili katiba ya nchi. Hafu kile kipengele cha serikali tatu akitoe . Mana katiba inayokata upande mmoja sio nzuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mwenye kufuatilua siasa hawa. Mabwana hata wakitoka ,sidhani hata kama ccm itayumba,ccm waliikuta na wataicha,wengi tulijua kuwa mwaka 2015 baada ya Mh lowasa kuikimbia ccm,hapo ndo ilikuwa mwisho wake,cha ajabu hadi sasa ccm inachanja mbuga,

Eti jpm awabembeleze,kwa lipi? Ccm kila siku unavuna wanachama wapya sasa itateteleshwaje na tu watu tuwili?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hao wazee wameonyesha njia lakini watu hawaioni na wabaya wameamua kubaki kimya lakini wanatafuna mithili ya mchwa...ngoja tuone
Fisadi kama kinana ataonyesha njia gani.
 
MAKATIBU wakuu wastaafu wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba, wamejivua uanachama wa chama hicho.

Habari zilizoifikia SAUTI KUBWA zinasema Kinana na Makamba walijiondoa rasmi CCM kwa maandishi. Barua zao, kila mmoja na ya kwake, zilifikishwa ofisini kwa Katibu Mkuu wa CCM tarehe 7 Februari 2020.

Chanzo kinachoaminika kutoka CCM Makao Makuu kimeiambia SAUTI KUBWA: “Barua zao zimefika kwa nyakati tofauti, zimepokelewa. Lakini inaonekana kama walikuwa wameziandika muda mrefu baada ya kushauriana, maana zinafanana na zimewasilishwa siku moja. Taarifa hizi zilipofikishwa kwa Mzee (Rais John Magufuli) zilimvuruga kwa kweli.”

Kwa mujibu wa chanzo hicho, ambacho hakitatajwa hapa, Rais Magufuli, baada ya kupokea ujumbe wa Kinana na Makamba kujivua uanachama, aliwaomba wazee wawili waandamizi – Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na Spika Mstaafu Pius Msekwa – wamsaidie kuzungumza na akina Kinana ili kuwashawishi wabadili msimamo wao.

Hata hivyo, Kinana na Makamba wamegoma kusikiliza ushawishi wa mtu yeyote. Katika barua zao za kujiondoa CCM, kwa mujibu wa chanzo chetu, Kinana na Makamba waliambatanisha pia kadi zao za uanachama.

“Tayari wameturudishia kadi zetu, maana yake wao si wanachama wetu tena,” kimesema chanzo hicho.

Kinana na Makamba ni miongoni mwa makatibu wakuu wanaoheshimika katika CCM, wenye ushawishi, na ambao wametumikia nchi katika nyadhifa mbalimbali kuanzia jeshini hadi serikalini na kwenye chama.

Siku ambayo walikabidhi barua na kadi zao na kutangaza rasmi kujiondoa CCM, ndiyo siku walipotarajiwa kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya CCM iliyoagizwa na Rais Magufuli katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), ili wajieleze kuhusu waraka walioanidika kwa Baraza la Wazee la chama hicho wakilalamikia kubezwa na kudhalilishwa na mhuni mmoja anayetumia jina la rais kudhihaki na kushambulia wakosoaji wa rais na serikali.

Mbali na Kinana na Makamba, mwingine aliyeitwa kuhojiwa na kamati hiyo ni Bernard Membe, waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ambaye aliunga mkono waraka wa wazee hao, na pia alidukuliwa akizungumza katika simu mambo ambayo hayakumfurahisha Rais Magufuli.

Yeye alikutana na kamati hiyo Mjini Dodoma Ijumaa tarehe 7, Februari 2020; na baada ya mahojiano alionekana mwenye kujiamini na mwenye furaha. Mmoja wa wajumbe walioshiriki mahojiano hayo amezungumza na SAUTI KUBWA kwa sharti la kutotajwa, akisema: “Tulijuta kumuita Membe. Kuna maswali amehoji na masuala amezungumza nasi hadi tukahisi yeye ndiye anayetuhoji. Ukweli ni kwamba chama chetu kinahitaji mabadiliko makubwa ya kimsingi, maana kuna shida mahali. Bwana mkubwa anatupelekesha, na watu jasiri wa kumwambia ukweli hawapo, tunaishia kuagizwa tu, hata kutenda mambo yaliyo kinyume cha misingi ya CCM. Membe ametukumbusha yote haya. Kwa kweli, sijui kinachoofuata.”

Hata hivyo, SAUTI KUBWA iliambiwa wiki iliyopita kuwa agizo la kamati kuwahoji wakongwe hao lilikuwa kama igizo tu, kwani Rais Magufuli na watu wake walishaamua kuwa Membe na Kinana wavuliwe uanachama, na Mzee Makamba apewe onyo kali.

Kwa Kinana na Makamba kujivua uanachama na kugoma kuhojiwa, wamewaza hatua mbili mbele ya Magufuli. Chama hakiwezi kuwahoji kwa kuwa wao hawafungwi tena na nidhamu wala maadili ya CCM kwa kuwa si wanachama CCM.

Ingawa barua zao zilipelekewa kimya kimya, na uongozi wa juu wa CCM umekuwa unahangaika kuzuia taarifa hizi kuvuja, zilivuja mapema mno; na kitendo chao cha kutofika mbele ya kamati kuhojiwa kimezua maswali na mjadala mpana ndani nanje ya CCM.

Baadhi ya wadau wa siasa za Tanzania wanasema inawezekana kitendo hiki kikawaingiza wote wawili, au mmoja wao, kwenye matata makubwa, kwani uongozi wa CCM ni wa visasi, unaweza kutaka kuwakomoa na kuwadhalilisha.

Profesa mmoja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema: “Tusishangae sasa kusikia siku moja Kinana au Makamba wametiwa mbaroni na wanashitakiwa kwa utakatishaji fedha, maana hii ndiyo fimbo mpya ambayo inatumika kuumiza wanaotofautiana na watawala. Lakini iwapo watashitakiwa umma utajua kuwa sababu hasa si uhalifu wao bali ni hii barua yao na uamuzi wao.”

Kiongozo mmoja mwandamizi wa CCM ameiambia SAUTI KUBWA: “Kiukweli, Mzee Kinana na Mzee Makamba hawana cha kupoteza. Nadhani sisi ndio tuna cha kupoteza, maana ukisoma waraka unaowasababishia haya yote utagundua kuwa wao ni watetezi wa misingi ya chama chetu. Wanachotetea ndicho wanaCCM wote tunapaswa kutetea, lakini sasa tofauti iliyopo kati yetu na wao ni kwamba wao wameonyesha ujasiri ambao sisi hatuna. Wengi wetu tumebaki kutii maagizo ya bwana mkubwa, huku chama kinaporomoka!”

SAUTI KUBWA inatambua kuwa kuna mtifuano mkubwa ndani ya CCM ambao haujawahi kutokea tangu uwepo wa chama hicho, ingawa wanafanikiwa kuufunika kwa kutishana – kwa kutumia vuombo vya dola.
 
Ndo tunataka iwe ivo maana walituibia sana

Kama wezi mbona hawapelekwi mahakamani?
Acha kuropoka
Duh! Bora angalau angalau Makamba! Lakini Kinana? Kinana ni fisadi mkubwa aliyepora na kujilimbikizia mali kwa kofia ya Katibu mkuu wa CCM! Safishasafisha ya Magufuli ndani ya CCM ilimuacha hoi bin taabani na kuanza fitna! Maji yamewafika shingoni! Kuondoka CCM sio dawa! Dawa ni kurudisha Mali za Chama na hela za umma na kuwaomba wananchi msamaha madharara waliyowasababishia kwa wizi huo! Chini JPM kila jiwa litapinduliwa. Lowassa, Kingunge na Sumaye sasa hivi wako wapi! Usicheze na CCM!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh!, kama ni kweli, hii ni kali ya mwaka, ila mimi ni mmoja katika kundi la kina Tomaso, siamini mpaka CCM wenyewe waseme!.
P
Mkuu P. unamsubili Polepole au Musiba? Polepole akijitokeza na barua ya tarehe 5/2 kuwafukuza hawa wazee uanachama ndiyo utaamini? Musiba akijitokeza tena akisema hawa waezee ni virus ndani ya chama utakubali?. Mungu ibari Tz, Mungu ibariki Afrika.
 
Duh! Bora angalau angalau Makamba! Lakini Kinana? Kinana ni fisadi mkubwa aliyepora na kujilimbikizia mali kwa kofia ya Katibu mkuu wa CCM! Safishasafisha ya Magufuli ndani ya CCM ilimuacha hoi bin taabani na kuanza fitna! Maji yamewafika shingoni! Kuondoka CCM sio dawa! Dawa ni kurudisha Mali za Chama na hela za umma na kuwaomba wananchi msamaha madharara waliyowasababishia kwa wizi huo! Chini JPM kila jiwa litapinduliwa. Lowassa, Kingunge na Sumaye sasa hivi wako wapi! Usicheze na CCM!
Ni mali gani hizo za Kinana zilizochukuliwa? Kama hujui, unabakia kuwa ni mmbea.
 
SAUTI KUBWA wamechafua na kudhalilisha jina lao na kada nzima ya uandishi huru.

Vyanzo vyao vimewaambia Bwana Mkubwa amefedheheka mpaka kutafuta watu wa kwenda kuwabembeleza kina Makamba.

Na vyanzo hivyo hivyo vimewataarifu Mzee alishapanga kuwapiga paranja uanachama na hivi vikao ni ghereaha tu, na wakileta mbwai watafanyiwa mbwai za utakatishaji, usanifu, uratibu na ufadhili wa genge la uhalifu na uhujumu wa uchumi.

Mwandishi si tu anafika aya ya tano keshasahau aya ya pili alidanganya nini bali hata kupitia andiko kabla ya kurusha hewani anasahau.
Nadhani umekosa uelewa wa analysis.

Unataka kutumia njia ya 'divide and rule' ili umwadhibu usiyemtaka. Unaamini ukimwadhibu unayemchukia, utapeleka ujumbe kwa wengine ili wapate woga wa kukemea na kuonya.

Kabla hijuafanya hilo, uliotaka kuwatenganisha, wanaungana, na kuachana nawe. Utafurahia, utachukia, utachanganyikiwa au utaimarika?
 
Kwa mwenye kufuatilua siasa hawa. Mabwana hata wakitoka ,sidhani hata kama ccm itayumba,ccm waliikuta na wataicha,wengi tulijua kuwa mwaka 2015 baada ya Mh lowasa kuikimbia ccm,hapo ndo ilikuwa mwisho wake,cha ajabu hadi sasa ccm inachanja mbuga,

Eti jpm awabembeleze,kwa lipi? Ccm kila siku unavuna wanachama wapya sasa itateteleshwaje na tu watu tuwili?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sidhani sasa hivi kama kuna CCM. CCM imeguzwa kuwa ni Magufuli. Magufuli ndiyo amekuwa chama.
 
CCM ni chama chenye usubutu na chenye kuamini kuwa hakuna aliye zaidi ya chama na chenye kutetea maslahi mapana ya Taifa Kama ni kweli acha waondoke kwani waliondoka wengi wakubwa zaidi yao binafsi niwatakie uzee mwema

Pumbavu, ngoja uwaone walio juu ya chama
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom